UFUFUO WA WAFU

 ZACHARY KAKOBE

Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

 

SOMO LA 7 :  UFUFUO WA WAFU

Leo tena , tunaendelea na mfululizo nwa masomo ya matukio ya mwisho wa dunia. Somo la leo “UFUFUO WA WAFU”,tutaligawa katika vipengele vinne:-

( 1 ). MAHALI ANAPOKWENDA  MTU BAADA YA KUFA

( 2 ). UHAKIKA WA UFUFUO WA WAFU

( 3 ). UFUFUO WA WAFU UNAVYOFANYIKA

( 4 ). AINA MBILI ZA UFUFUO WA WAFU

( 1 ). MAHALI ANAPOKWENDA MTU BAADA YA KUFA.

Mtu anapokufa, moja kwa moja anakwenda kukutana na hukumu yake ( WAEBRANIA 9:27 ). Kama mtu amekufa akiwa ameokoka na kuishi katika utakatifu  mpaka dakika yake ya mwisho, sekunde ileile anakwenda peponi yyaani mbinguni ( LUKA 23:39-43; MATENDO 7::54-59; WAFILIPI 1:21-23 ). Ikiwa mtu amekufa akiwa hajaokoka, sekunde ileile anakwenda katika mateso ya moto Jehanum ( LUKA 16:19-28 ). Ingawa mwili wa mtu anayekufa, unabaki kaburini, roho yake pamoja na nafsi yake vinaambatana na mwili mpya. Kuna miili ya duniani, tena kuna miili ya mbinguni            ( 1 WAKORINTHO 15:40-44; AYUBU 19:25-27; MHUBIRI 12:7 ). Katika mwili mpya mtu anakwenda motoni au binguni. Akiwa huko , atajijua kabisa. Atakuwa  anaona, kuhisi , kusikia na kuwa na kumbukumbu hata ya ndugu zake waliobaki duniani ( LUKA 16:27-31 ).

 

( 2 ). UHAKIKA WA UFUFUO WA WAFU

Ufufuo wa wafu, ni moja kati ya masomo ya msingi sana  katika Ukristo na ni mafundisho ya kwanza  ambayo kila Mkristo  inampasa kuyafahamu ( WAEBRANIA 6:1-2 ). Kiyama ya wafu au Ufufuo wa wafu, umetabiriwa  mapema  katika Neno la Mungu ( LUKA 14:13-14;  YOHANA 5:28-29; WAFILIPI 3:10-11; 1 WATHESALONIKE 4:16 ). Yesu Kristo ndiye kielelezo cha wafu na uhakika wa ufufuo wa wafu kwa watu wote ( 1WAKORINTHO 15:21, 20-23). Yesu kristo alitabiri mapema juu ya kufufuka kwake kabla hata hajafa (MATHAYO 16:21; 17:22-23; 20:17-19; MARKO 8:31-32; 10:32-34; LUKA 9:20-22; 18:31-34). Yesu Kristo huyuhuyu alitabiri juu ya kufufuka kwake na ikawa hivyo, ndiye pia aliyetabiri juu ya ufufuo wa watu wote ( YOHANA 5:25-29 ). Ni muhimu kufahamu kwamba walikuwepo watu wenye mashaka, ambao hawakuamini kwamba Yesu angefufuka kama alivyosema           ( LUKA 18:31-34 ); lakini kutokuamini kwao hakukuzuia kufufuka kwa Yesu. Vivyo hivyo leo, pamoja na kuwapo watu wasioamini kwamba kutakuwa na ufufuo wa wafu, kutokuaminii kwao hakutaweza kuzuia jambo hilo kutokea ( WARUMI 3:3-4 ). Uongo wa askari Walinzi wa kaburi la Yesu, waliutawanya baada ya kupokea rushwa na kufundishwa kusema uongo, kwa kuabiwa “ semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala “, ni uongo ulio dhahiri ( MATHAYO 28:11-15 ). Ikiwa walinzi walikuwa wamelala usingizi, waliwaona namna gani watu waliokuja kuuiba mwili wa Yesu na kufahamu kwa hakika ni wanafunzi wake? Na kama waliwaona kwa nini waliwaacha wakauiba mwili huo na wasiwazuie kufanya hivyo? Ni uongo ulio wazi. Ni jambo lililo dhahiri kwamba Yesu alifufuka! Kwa jinsi hiyohiyo, ufufuo wa wafu wote ni jambo lililo dhahiri kabisa kutokea.

( 3 ) . UFUFUO WA WAFU UNAVYOFANYIKA

Ufufuo wa wafu, ni kama kuvua nguo mpya na kisha ukavaa nguo ya zamani. Kama jinsi ambavyo mtu alivyokufa na kuuacha mwili wake, duniani, ndivyo itakavyokuwa tena. Katika ufufuo wa wafu mtu atatoka katika Jehanum ya moto na kuurudia mwili wake wa duniani au atatoka peponi au mbinguni na kuurudia mwili wa duniani. Hata kama mwili ule umekuwa udongo baada ya mingi, ni muhimu kukumbuka kwamba Mungu aliyemwumba mwanadamu kutoka katika mavumbi, hashindwi kuufanya mwili uliokuwa udongo urudie hali ya mwili tena ( 1WAKORINTHO 15:42-44 ).

 

( 4 ) . AINA MBILI ZA UFUFUO

Katika mpango wa Mungu wa ufufuo wa wafu, kuna aina mbili za ufufuo wa wafu:-

 

  1 . Ufufuo wa kwanza au ufufuo wa uzima

Ufufuo huu pia unapewa majina mengine katika Biblia –ufufuo ulio bora au ufufuo wenye haki ( YOHANA 5:28-29; UFUNUO 20:4-6; LUKA 14:13-14; 1WATHESALONIKE 4:16 WAEBRANIA 11:35 ). Ufufuo wa kwanza unajumuisha wale wote waliokufa na kwenda mbinguni yaani wenye haki au watakatifu. Hawa ndio wenye sehemu katika ufufuo wa kwanza. Huu ni ufufuo wa uzima kwa sababu wale wote watakaokuwa katika ufufuo huu, watakuwa katika uzima wa milele katika Mbingu Mpya na Nchi Mpya. Huu ndio ufufuo ulio bora. Ufufuo huu uko katika sehemu mbili:-

( a ) Ufufuo wa watakatifu wote walio mbinguni wakati wa kunyakuliwa kwa Kani

sa. Hawa watafufuliwa kwanza kisha kufumba na kufumbua miili yao itabadil

ishwa tena na kuungana na wale walio hai ambao nao miili yao itabadilishwa

na kuwa ya utukufu, kisha wote kwa pamoja watakwenda kumlaki Bwana Yes

u mawinguni ( 1WATHESALONIKE 4:16 ).

          ( b ).Ufufuo wa Watakatifu wa wakati wa Dhiki  Kuu- Hawa ni Waisraeli ambao

Hawakumsujudia yule mnyama yaani mpinga Kristo  wala sanamu yake na

Kukataa kabisa kupokea chapa ya 666 katika vipaji vya nyuso zao., na hivyo

Kukatwa vichwa na kuuawa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu na neno la Mungu

Wakati wa Dhiki Kuu. Hawa watafufuliwa wakati wa kuja kwa Yesu Kristo

mara ya pili pamoja na Watakatifu wake walionyakuliwa. Waisraeli hawa

baada ya kufufuliwa huku, moja kwa moja watatawala pamoja na Kristo miaka

elfu  duniani ( UFUNUO 20:4-6 ). Waisraeli ndio wanaopewa onyo la

kukwepa uhusiano wowote na Makristo wa uongo na  manabii wa uongo

( MATHAYO 24:23-27 ). Watakao faulu kufanya hivi na kuwa na ushuhuda

Wa Yesu  kuwa ndiye Kristo moyoni mwao hata wakifa katika Dhiki hiyo,

Watafufuliwa katika ufufuo huu  wakati huu.

2 . Ufufuo wa pili au ufufuo wa hukumu

Ufufuo huu pia unaitwa ufufuo wa aibu na kudharauliwa ( YOHANA 5:29; DANIELI 12:2 ). Huu ni ufufuo wa watenda mabaya au wenye dhambi wote, ambao watakuwa wanatoka Jehanum ya moto. Wote walioko Jehanum hivi sasa hadi wale watakaokwenda huko baada ya vita vya Gogu na Magogu itakayofanyika mwishoni mwa miaka elfu ya utawala wa Kristo duniani, ambayo itawamaliza wenye dhambi wote na kisha waende wote motoni; wote hawa watafufuliwa katika ufufuo huu `wa pili utakaofanyika muda mfupi baada ya miaka elfu ya Utawala wa Kristo miaka elfu duniani . Baada ya kufufuliwa watahudhuria wote mbele ya kiti cha enzi, kikubwa, cheupe cha hukumu. Walipokwenda motoni walikuwa hawajaelezwa waziwazi makosa yaliyowapeleka motoni, sasa hapa ndipo mahali ambapo Yesu Kristo mhukumu wa haki atakapo waonyesha waziwazi matendo yao kwa mfano wa video ( UFUNUO 20:5, 11-15 ). Itakuwa ni aibu mno na kudharauliwa maana siri zote za mtu zitakuwa waziwazi, yote aliyoyafanya ya uzinzi akiwa sirini yataonyeshwa waziwazi bele ya watu wote. Hapa ndipo watu watajitetea, “Bwana Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako na kwa jina lako kutoa pepo……….”, naye Yesu mhukumu wa haki atawaambia dhahiri, Si kuwajua ninyi kamwe! Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. Wote watatupwa kwenye ziwa la moto.

HERI YEYE ALIYE NA SEHEMU KATIKA UFUFUO WA KWANZA

                                            (  UFUNUO 20:6 )

Mpendwa msomaji, baada ya kusikia yote haya kutoka kwa nabii aliyetumwa kukuletea ujumbe huu, usifanye moyo wako kuwa mgumu.  Hii ni nafasi ya kipekee ya kuokoka.  Je, unajuaje kama utaamka kitandani baada ya kulala usiku wa leo?  Wakati uliokubalika wa wokovu ni sasa (2 WAKORINTHO 6:2).  Labda utaniuliza, ili uokoke, ufanyeje?  Jibu ni rahisi, kwa imani ukitubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, na kumwambia Yesu Kristo akusamehe, utasamehewa sasa hivi, na msamaha wa dhambi, huambatana na wokovu (LUKA 1:77).  Je, uko tayari kuokoka sasa hivi?  Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii kwa dhati toka moyoni, Mungu baba asante kwa kuniletea ujumbe huu.Natubu dhambi zangu zote, kwa kumaanisha kuziacha. Yesu Kristo nakuomba unisamehe dhambi zangu na kunipa uwezo wa kushinda dhambi na kuniokoa kutoka katika mateso ya moto wa milele. Asante, kwa kuniokoa katika Jina la Yesu.  Amen.  Tayari sasa umeokoka, na kwa hakika unakwenda mbinguni sasa, hata ukifa leo.  Ili uzidi kuukulia wokovu, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

.       Masomo ya matukio ya mwisho wa Dunia. Unaweza kuingia kwenye link ya kila somo.
1. KUNYAKULIWA KWA KANISA
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/01/02/kunyakuliwa-kwa-kanisa/
2. DHIKI KUBWA
https://davidcarol719.wordpress.com/dhiki-kubwa/
3. TAJI KWA WATAKATIFU NA HARUSI YA MWANAKONDOO
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/02/10/taji-kwa-watakatifu-na-harusi– ya-mwanakondoo/
4. KUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI NA VITA VYA HAR-MAGEDONI
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/02/10/kuja-kwa-yesu-kristo-mara-ya-pili-duniani-na-vita-ya-har-magedoni/
5. MIAKA 1,000 YA UTAWALA WA YESU KRISTO DUNIANI NA VITA VYA GOGU NA MAGOGU
https://davidcarol719.wordpress.com/miaka-1000-ya-utawala-wa-yesu-kristo-duniani-na-vita-vya-gogu-na-magogu/
6. UFUFU WA WAFU
https://davidcarol719.wordpress.com/187-2/
7. JEHANUM YA MOTO
https://davidcarol719.wordpress.com/jehanum-ya-moto/
8. KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE CHA HUKUMU
https://davidcarol719.wordpress.com/231-2/
9. MBINGU MPYA NA NCHI MPYA
https://davidcarol719.wordpress.com/mbingu-mpya-na-nchi-mpya/

                                                          . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .         

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

                                              UBARIKIWE NA BWANA YESU!!!

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s