UTHIBITISHO KUWA YESU NI MUNGU

ZACHARY KAKOBE

Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SOMO: UTHIBITISHO KUWA YESU NI MUNGU

Ni muhimu kufahamu kuwa Yesu Kristo ni Mungu.Ikiwa sisi ni wanafunzi wa Biblia tusiwe kama wengine wanaosema kuwa Yesu si Mungu.Kama huna moyo wa jiwe  kama  wengine waliotiwa upofu kiroho na kushindwa kuyaelewa maandiko,Je,unaamini kuwa Yesu ni Mungu?  Yesu ni Mungu na ushahidi mwingi wa maandiko upo.

Somo hili lipo katika vipengere vinne vifuatavyo:-

 1. KUTAJWA KWA YESU KRISTO NI MUNGU KATIKA BIBLIA.
 2. SABABU SABA ZA KUTHIBITISHA KUWA NI MUNGU.
 3. YESU ALIPOKUWA DUNIANI ALIKUWA EMANUELI MUNGU PAMOJA NASI.
 4. YESU MWANA WA MUNGU.

Kipengere cha kwanza,

1.KUTAJWA KWA YESU KRISTO NI MUNGU KATIKA MAANDIKO.

Hapa tunaona maandiko yakimtaja Yesu KriNasto waziwazi kuwa ni Mungu. Katika  ( 1YOHANA. 5:20 ) “Nasi twajua kuwa Mwana wa Mungu amekwisha kuja,naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli,nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli.,yaani ndani ya Mwana wake Yesu Kristo.Huyu ndiye MUNGU WA KWELI NAUZIMA WA MILELE”.. Pia katika ( YOHANA 20:26-29 ) “basi,baada ya siku nane,wanafunzi wake walikuwamo ndani tena,na Tomaso pamoja nao.Akaja Yesu na milango ilikuwa imefungwa,akasimama katikati,akasema,Amani iwe kwenu.Kisha akamwambia Tomasolete hapa kidole chako;uitazame mikono yangu;ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu;wala usiwe asiyeamini;bali aaminiye.Tomaso akajibu akamwambia,BWANA WANGU NA MUNGU WANGU..Yesu akamwambia,wewe kwa kuwa umeniona umesadiki;wa heri wale wasioona wakasadiki”.YESU KRISTO MUNGU MKUU, ( 1TITO 2:13  )  “Tukilitazamia tumaini lenye mafunuo ya KRISTO YESU MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU”.. YESU NI MUNGU aliyejifunua katika mwili ( WARUMI 9:5 )  “Na katika hao alitoka KRISTO KWA NJIA YA MWILI,NDIYE ALIYE JUU YA MAMBO YOTE,MUNGU,MWENYE KUHIMIDIWA MILELE.AMINA..Mhalifu msalabani alimwita YESU Mungu na kumuomba YESU atakapokuwa katika ufalme wake amkumbuke mharifu huyo”. ( LUKA 23:39-43 ).Yesu hakukataa kuwa SI MUNGU bali alisema,Amini nakuambia leo hivi,utakuwa pamoja nami peponi.YESU NI MUNGU ALIYEKUJA DUNIANI .( WAFILIPI 2:5-6  )  “Ambaye yeye mwanzo alikuwan yuna namna ya Mungu,naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho,bali alijifanya kuwa hana utukufu,akatwaa namna ya mtumwa,akawa ana mfano wa wanadamu”.YESU alijita-mbulisha kwao kuwa ni MUNGU lakini hawakuelewa ( YOHANA 10:30-33 )  “Yesu akawajibu,kazi njema nyingi niwewaonyesha zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe? Wayahudi wakamjibu,kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe;bali kwa kukufuru,na kwasababu wewe uliye.mwanadamu wajifanya kuwa Mungu. Wayahudi walisema anakufuru kwa kusema kuwa yeye ni Mungu.Kimsingi Yesu ndiye Baba mwenyewe ndio maana anasema huwezi kumtenganisha na Baba; ukimwona yeye umemuona Baba. ( YOHANA 14:7-9 )

Katika mstari 8 na 9  Filipo akamwambia,Bwana,utuonyeshe Baba yatutosha. Yesu akamwambia,Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote,wewe usinijue,Filipo?

    Ikiwa tu wanafunzi wa Yesu hatupaswi kubabaishwa na watu ambao hawana Roho wa Mungu.Mtu ambaye hana Roho wa Mungu hawezi kusema Yesu ni Mungu..Kwasababu hiyo,wanatumia akili tu.Hawa ni watu wa tabia ya asili ambao hawawezi kuyaelewa  mambo ya kiroho ( 1WAKORITHO 2:14 ) “Basi,mwanadamu wa tabia ya asili hawezi kuyapokea mambo ya Roho wa Mungu;maana kwake ni upuuzi;wala hawezi kuyafahamu;kwa kuwa yanatambulikana kwa jinsi ya rohoni”

2.SABABU SABA ZA KUTHIBITISHA KUWA YESU NI MUNGU.

1.YESU NI MUUMBAJI.

Sifa ya kuumba niya Mungu peke yake ( YOHANA 1:3,14 )  “vyote vilifanyika kwa huyo;wala pasipo yeye hakukufanyika chochote kilichofanyika.Naye Neno alifanyika mwili;nasi tukauona utukufu wake kama utukufu wa Mwana pekee atokaye kwa Baba,amejaa neema na kweli”.Yesu aitwa Neno la Mungu (UFUNUO 19:13) “Kwahiyo Neno ni Mungu “(YOHANA 1:1)..  na huyo ndiye aliyevifanya kuwako vitu vyote.Aliyeshuka kutoka juu na kufanyika mwili ni Yesu pekee aliyezaliwa na bikira Mariamu bila mbegu ya kiume kama inavyotokea kwa wanadamu wengine..Katika yeye vtu vyote viliumbwa (WAKOLOSAI 1:13-16) vinavyoonekana na visivyoonekana;vya mbinguni na vya duniani.Maandiko yako wazi kabisa kwa mtu mwenye Roho wa Mungu anaelewa kwa urahisi.

2.YESU ALIKUWEPO KABLA YA VITU VYOTE KUWEPO DUNIANI.

( WAKOLOSAI 1:17 ) “Naye amekuwako kabla ya vitu vyote;na vitu vyote hushikamana katika yeye”.( MIKA 5:2 ) Basi,wewe Bethlehemu,Efrata,uliyemdogo kuwa miongoni mwa maelfu za Yuda;kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli;ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale;tangu milele“.

Yesu Kristo alikuwako kabla ya Nabii Ibrahimu kuwako(YOHANA 8:52-58). Watu walioambiwa maneno hayo n a Yesu mwenyewe wliokota mawe ili kumpiga Yesu wakisema kuwa anakufuru.Hawa ni watu wa tabia ya mwilini wanaotumia akili kupambanua mambo ya Mungu (mambo ya kiroho huwezi kuyatambua kwa akili maana Mungu ni Roho,( YOHANA 4:24)..YOHANA 17:5,24.WAEBRANIA 7:3 ). Imasema  “hana baba,hana nana,hana wazazi,hana mwanzo wa siku zake,wala mwisho wa uhai wake,bali amefananishwa na Mwana wa Mungu;huyo adumu kuhani milele”.YESU ni alfa na omega ,wakwanza nawa mwisho kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu yeye alikuwako (UFUNUO 22:13).Bali kwa damu ya thamani,kama ya mwana-kondoo asiye na ila,asiye na waa,yaani ya Kristo.Naye amejulikana kweli tangu zamani,kabla haijawekwa misingi ya  dunia,lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yetu ( 1PETRO 1:19-20 ).

3.YESU NI MTAWALA JUU YA YOTE.  HII NI SIFA YA MUNGU PEKEE.

  (YOHANA 330 ) “Yeye ajaye kutoka juu,huyo yu juu ya vyote.Yeye aliye wa dunia asili yake ni ya dunia,naye anena mambo ya duniani,yeye ajaye kutoka mbinguni yuu juu  ya yote” . ( YOHANA 13:13 ) “Ninyi mwaniita ,Mwalimu, na Bwana;nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo“. ( WARUMI 14:9 ) “Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii,awamiliki waliokufa na walio hai pia”. Neno kumiliki ni kutawala sifa ya kutawala ni sifa ya Mungu pekee.


4,YESU KRISTO NI ZAIDI YA MTU YEYOTE AU NABI AU MTUME YEYOTE YULE..

( WAEBRANIA 3:1-7 ) Mustari 3 unasema,Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahiliutukufu zaidi kuliko Musa,kama vile yeye atengenezayenyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba”..Anayezungumziwa hapa ni Yesu Kristo Mungu muumbaji. YESU ,ameketi mkono wa kuume wa ukuu huko mbinguni (WAEBRANIA 1;3-4).

5,YESU NDIYE ATAKAYE HUKUMU WALIMWENGU (WATU) WOTE.

( ZABURI 58:11 ), ‘Hakika yuko Mungu anayetawala katika dunia“. (UFUNUO 18;8 ) “Kwasababu hiyo,mapigo yake yatakuja katika siku moja,mauti na huzuni na njaanaye atateketeza kabisa kwa moto.Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu“.Tene ndiye atakaye ihukumu Dunia yote  “Tena Baba hamhukumu mtu ye yote,bali amempa Mwana (YESU) hukumu yote“.( MATHAYO 25:31-32 ) “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu (YESU) katika utukufu wake,na malaika watakatifu wote pamoja naye,ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake.Na mataifa yote yatakusanyika mbele zake,naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi” .( MATENDO 10:42 ) “Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudiaya kuwa huyu ndiye (Yesu) aliyeamriwa na Mungu awe mhukumu wa wahai na wafu” ( WARUMI 2:16 )  “Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu,sawasawa na injili yangu,kwa Kristo Yesu.( 2TIMOTHEO 4:1 ) “Nakuagiza mmbele za Mungu,na mbele za Kristo Yesu,atakayewahukumu waliohai na waliokufa;kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake’.

6.YESU HABADILIKI TENE HANA KIGEUGEU.                                     {WAEBRANIA 13:8} “Yesu Kristo ni yeye yule jana na leohata milele“. ( WAEBRANIA 1:10-12 ) “Wewe ,Bwana,hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi.Na mbingu ni kazi ya mikono yako;Hizo zitaharibika,lakini wewe unadumu;Nazo zote zinachakaa kama nguo,Na kama mavazi,utazizinga,nazo zitabadilika;Lakini wewe u yeye yule,na miaka yako haitakoma“. ( MALAKI 3:6 ) Kwa kuwa mimi,Bwana,sina kigeugeu” ( ZABURI 102:26-27 ) “Hizi zitaharibika,bali wewe utadumu;Naam,hizi zitachakaa kama nguo;na kama mavazi utazibadirisha,nazo zitabadilika.Lakini wewe U yeye yule;na miaka yako haitakoma“. ( YAKOBO 1:17 ) “Kwake hakuna kubadilika,wala kivulu cha kugeukageuka”.

 1. YESU YUPO KILA MAHALI ,KOTEKOTE DUNIANI.

( MATHAYO 18:20 ) “Kwa kuwa walipo wawili watatu,wamekusanyika kwa jina langu,mimi nipo papo hapo katikati yao”. Mwenye uwezo wa kukaa mahali pote ni Mungu.

 1. YESU ALIPOKUWA DUNIANI ALIKUWA EMANUELI(MUNGU PAMOJA NA WANADAMU).

( MATHAYO 1:23-25 ) Tazama; bikra atachukua mimba; naye atazaa mwana;nao watamwita jina lake Emanueli; yaani ,Mungu pamoja nasi”.Tabia ya Yesu inaonyesha kuwa kama mwanadamu,kuzaliwa kwake kwa uwezo wa Roho mtakatifu.Hapa tunaona jinsi alivyo na uwezo wa tofauti na wanadamu akiwa anafahamu mambo yote kabla akiwa duniani..Yeye pia ajua yote yaliyomo ndani ya moyo wa mwanadamu (YOHANA 6:64,YOHANA 13:1,YOHANA 13:11,YOHANA 18:4,YOHANA 19:28).Tena Yesu alitabiri kabla jambo kutokea,pia alijitabiria mwenyewe yatakayomtokea mbele (MARKO 8:31,LUKA 9:22,LUKA 12:50,LUKA 22:37,LIKA 24:7-26,YOHANA 3:14,YOHANA 10:17-18,YOHANA 7:33,YOHANA 13:33,YOHANA 14:28,YOHANA 17:11,YOHANA 16:5,10,16,18 ).

Yesu aliabudiwa na kusujudiwa akiwa hapa duniani,Sifa ya kuabudiwa na kusujudiwa ni ya Mungu pekee hivyo Yesu ni Mungu.(MATHAYO 4:10).

 • Hata malaika wote wanamsujudia Yesu (UFUNUO 22:8-9,WAEBRANIA 1;6).
 • Ndiyo maana Yesu alisujudiwa akiwa mtoto mchanga alipozaliwa (MATHAYO 2:11,MATHAYO 14:33<LUKA 24;52).
 • Hata pepo wachafu walimsujudia Yesu (MARKO 5:2,6).

YESU ALIKUWA MWANADAMU ALIPOKUWA DUNIANI

A: Alizaliwa na bikira Mariamu(mwanadamu) ( LUKA 2:3-7 ).

B: Aliongezeka kimo  ( LUKA 2:40-42-52)

C: Aliona njaa  kama watu wengine ( LUKA 4:2)

D: Alilala usingizi kama binadamu wengine( LUKA 8:23)

E: Alikuwa na viungo kama binadamu( LUKA 24:36-40)

F: Alikula chakula ( LUKA 24:41-43)

G: Alichoka kama mwanadamu ( LUKA 4:6; WAEBRANIA 4:15 : 2:16-18

 •  Msalabani alikufa kama mwanadamu hakufa kama Mungu ila alitupatanisha 1TIMOTHEO 2:5
 • Tunaona mama yake mariamu asema  mimi ni mjakazi wa BWANA YESU ( LUKA  1:38-46-47)
 • Tunaona pia hapa wakati wamekusanyika kwa ajili ya maombi akiwemo na Mariamu waliomba kwa jina la BWANA wala si kwa jina la mariamu(MATENDO 1:13-15,1 YOHANA 4:1-2.         

    4:YESU MWANA WA MUNGU

Tunaona hapa biblia inatuambia YESU KRISTO ni mwana wa Mungu (YOHANA 20:30-31) hapa Yesu mwenyewe anasema yeye ni mwana wa Mungu ( MATHAYO 26:59-64; 16:13-17 ) , neno mwana linamzungumzia Yesu mwana siyo kuwa Mungu anazaa la hasha

Yesu anaitwa mwana wa Mungu kwa sababu alizaliwa kwa uweza wa R oho Mtakatifu. Hata sisi tumezaliwa kwa mara ya pili kwa roho tunapo mwamini Yesu Kristo hivyo tunahesabika kuwa ni wana wa Mungu.(WAFILIPI 2:14-15,YOHANA 1:12).Kwahiyo Yesu anapoitwa Mwana wa Mungu maana yake ni chapa ya  Mungu (HUIOS) WAEBRANIA 1:1-3.Ndiyo maana hapa Yesu anawaambia wanafunzi wake,mumeniona mimi ;mumemuona Mungu,maana yake ndiyo hiyo (HUIOS) yaani chapa ya Mungu (YOHANA 14:7-9)

 1. Tunaona hapa Yesu alisema Yeye ni Mwana wa Mungu  (YOHANA 9:35-37)
 2. Shetani naye anajua kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu (MARKO 3:11,LUKA 4:41).
 3. Malaika nao wanasema kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu (LUKA 1:30-35)
 4. Mungu mwenyewe anasema kuwa Yesu ni Mwanangu mpendwa (MATHAYO 3:17,MATHAYO 17:5   )
 5.       KUMKIRI YESU KRISTO KUWA NI BWAMNA                             

Matatizo yote yanayompinga Yesu Kristo kuwa si Mwana wa Mungu,inatokana mtu yeyote anakuwa hana roho wa Mungu (1yohana 4:15) na Mungu hayuko ndani ya mioyo yao (1YOHANA 2:23,LUKA 10:16)ndiyo maana maandiko matakatifu ya Mungu yanasema asiyemwamini Mwana hana uzima wz milele,hiyo adhabu ya milele inamkalia (YOHANA 5:23,YOHANA 3:36,YOHANA 5:11-13) Kwahiyo wanaomkataa Yesu Mwana wa Mungu hawawezi kushinda dhambi.Huwezi kushinda dhambi kama huamini kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu (1YOHANA 5:4-5,YOHANA 1:12).Ndiyo maana mtu mwenye dini tu hawezi kushinda dhambi kwasababu hajampokea Yesu Mwana wa Mungu (YOHANA 1:12) Wote wanaompokea wanapewa uwezo wa kushinda dhambi.Ni rahisi kuthibitisha ukweli wa maneno haya; wewe muangalie mtu yeyeyote wa dini tu bila Yesu,hana uwezo wa kushinda dhambi.Ni watukanaji,wazinzi,wenye tama n.k ingawa sala zao ni nyingi na ndefu lakini haziwezi kuwasaidia kushinda dhambi.Ni muhimu kufahamu kuwa ni Yesu peke yake aliyeishi duniani bila kutenda dhambi (WAEBRANIA 4:15).Hakuna wokovu katika mwingine (MATENDO  4:12).Hakuna uwezekano kwa mtu ambae hajamkiri Yesu Kristo kuingia mbinguni (YOHANA 14:6).Yesu ni njia na kweli n a nuzima………………………………………………………………………..

………………………………………………………………………………………………………..

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

.

                                     . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

                                                          . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .         

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook ,Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

                                                         UBARIKIWE NA BWANA YESU!!!

 

Advertisements

3 comments on “UTHIBITISHO KUWA YESU NI MUNGU

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s