UBATIZO WA MAJI MENGI WA KIBIBLIA

ZACHARY KAKOBE

Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SOMO:   UBATIZO WA MAJI MENGI WA  KIBIBLIA

                  Ni muhimu kufahamu kuwa Yohana mbatizaji alimbatiza Yesu katika maji tele (MATHAYO 3:13-17). Yesu Kristo alibatizwa katika mto Yordani kwasababu huko kulikuwa na maji tele. Yohana mbatizaji alikuwa akibatiza sehemu zenye maji tele ili watu waweze kuzamishwa katika maji kama tutakavyoona maana ya ubatizo na kwa nini kuzamisha katika maji tele. Yohana mbatizaji hakubatiza Yordani tu, alibatiza Ainoni karibu na Salimu kwa sababu huko kulikuwa na maji tele. YOHANA 3:23 “Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwasababu huko kulikuwa na maji tele, watu wakamwendea wakabatizwa”. Ubatizo lazima ufanye kwenye maji tele ya kumtosha mtu kuzamishwa.

                   MAANA YA NENO KUBATIZWA AU UBATIZO

       Lugha za asili za biblia kabla ya tafsiri mbalambali ni kiebrania na kiyunani. Agano la kala iliandikwa kwa lugha ya kiebrania na again jipya iliandikwa kwa kiyunani. Katika kuifasiri biblia kwa lugha zetu kuna baadhi ya maneno machache ambayo misamiati yake ilipoteza maana halisi iliyopo katika biblia. Kwasababu lugha zingine zunakuwa na mapungufu.

       Katika biblia ya lugha ya kiebrania  kuna neno “BAPTIZO” lenye maana ya UBATIZO kwa Kiswahili na kwa kiingereza BAPTIZM,

       Katika biblia ya lugha ya kiyunani kuna neno   “BAPTO” lenye maana ‘kuzamisha au kuchovya”.

        Mifano katika biblia kuhusiana na neno” BAPTO’  kuzamisha au kuchovya.

 ( 1 ). Tonge la ugali linavyotowelewa katika ugali kasha linazamishwa lote. Tendo hilo la kuziswa ni kubapto “bapto” katika kiyunani (YOHANA 13:26).

 ( 2 ). Kuchovya ncha ya kidole. Neno kuchovya hapo (LUKA 16:24) lina katika lugha ya kiyunani ni ‘BAPTO” bapto likiwa na maana kuchovya au kuzamisha.

 ( 3 )  Tendo la kuchovya vazi katika damu lina maana ya kubapto “ BAPTO”  katika biblia ya ya lugha ya asili kwa kiyunani.

      Kwahiyo biblia inapozungumzia juu ya ubatizo inazungumzia ubatizo wa maji tele.Yohana aliwabatiza watu wa Ainoni kwasababu huko nako kulikuwa na maji tele (YOHANA 3:23). Pia tunamuona mtumishi wa Mungu Filipo na owashi wakitelemka majini ili abatizwe katika maji tele (MATENDO 8:34-39). Walitelemka majini akambatiza kasha wakapanda kutoka majini (MATENDO 8:36-39).

WATU WANAOFUNDISHA JUU YA UBATIZO WA KUNYUNYIZIA MAJI  KICHWANI AU USONI NAO PIA WANA MAANDIKO.

(EZEKIELI 36:25)Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafuwenu wote, na vinyago vyenu vyote”. (HESABU 8:5-7) “Kisha Bwana akanena na Musa. Na kumwambia, watwae walawi na kuwaondoa kati ya wana wa Israeli, kasha uwatakase. Nawe utawafanyia mambo haya ili kuwatakasa, nyunyiza juu yao maji yatakasayo dhambi, nao wajinyoe kwa wembe mwili wote, kasha wazifue nguo zao na kujitakasa”.    Upotofu ni rahisi kuingia kama tutayatafsiri maandiko kama tupendavyo. (2 PETRO 1:20; 2TIMOTHEO 2;15).

Maana ya maandiko hayo yanayotumiwa kimakosa kuharalisha ubatizo wa kunyunyiza maji kichwani au usoni. HESABU 19:13 “Mtuawaye yote agusaye maiti ya mtualiyekufa, asijitakase, yuatia unajisi maskani ya Bwana; na mtu huyo atakatiliwa mbali na Israeli; maana, hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake, atakuwa najisi, unajisi wake ungali juu yake bado”. Kwahiyo tunaona kuwa wakati wa agano la kale mtu aliyekuwa akiigusa maiti ya mtu aliyekufa, alihesabika kuwa amenajisika kwa kuigusa tu. Alihesabika kuwa ni mwenye dhambi (unajisi) na angeweza kulinajisi hekalu la Bwana (maskani ya Mungu). Mtu aliyenajisika alihesabika kuwa safi baada ya kunyunyiziwa kichani maji ya utakaso yaitwayo FARAKANO. (WAEBRANIA 9:10 )“kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya”.Hayo maandiko wakati wake ulishapita maana sisi tunaongozwa na agano jipya, again la rohoni, aganin la kale lilikuwa na mapungufu (WAEBRANIA 8:7-9). Dhambi au uchafu unaondolewa na damu ya Yesu kwa njia ya imani (1PETRO 1:2). Hatunyuziwi maji kichwani bali damu ya Yesu ndiyo inayonyunyizwa juu yetu na kuondoa dhambi. Tendo la kunyunyiziwa damu ya Yesu ndilo linaitwa kuzaliwa kwa roho au kuzaliwa mara ya pili (YOHANA 3:3-10).  Mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu (YOHANA 3:5;  1:12). Maji yanayotajwa katika YOHANA 3:3-10 ni neno la Mungu siyo ubatizo wa maji kama walimu wengi wanavyopotosha. Neno la Mungu linamsafisha mtu kama vile maji yasafishavyo (1PETRO 1:23)

KABLA YA KUBATIZWA SHARTI MTU HUYO ATUBU DHAMBI ZAKE ZOTE KWA KUMWAMINI YESU KRISTO BAADA YA KUHUBIRIWA AU KUFUNDISHWA .                                                                                                              

Ili  mtu awe na sifa ya kubatizwa kibiblia lazima atubu dhambi zake kwanza kwa kumwamini mwanawa Mungu Yesu Kristo . (MATENDO 2:37-38) “ Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha roho mtakatifu”.        MARKO 16:16 “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.Mtu anabatizwa baada ya kuamini na kutubu dhambi zake zote. Kuamini maana yake ni kuacha njia zako zote za awali na kugeuka au kufanya matendo ya wokovu. MATENDO 2:41 “Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu”. MATENDO 8:12-13 “ Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njeme za ufalme wa Mungu na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake. Na yeye Simon mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; Akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka”. Pia katika MATENDO 8:35-38 Towashi aliamini kwanza kabla ya kubatizwa na Filipo. Mtu baada ya kujifunza Neno la Mungu na kuliamini kwa moyo wake wote na kusafishwa kwa damu ya Yesu kwa njia ya imani aweza kubatizwa (MATENDO 16:31-33;  MATENDO 18;8)

 UBATIZO HAUFANYWI KWA WATOTO WADOGO.

Kwa kawaida  watoto wadogo wanapobatizwa huwa anakuwepo mtu mzima amempakata na kujibu maswali badala ya mtomto huyo, hii siyo sahihi kibiblia   EZEKIELI 18:20 “Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa babaye, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe; haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake”. Kwa msingi huo, mtu hawezi kutubu dhambi  kwa niaba ya mtu mwingine. Ni muhimu kufahamu kuwa watoto wadogo ufalme wa mbinguni ni wao hata  bila kutubu dhambi (MARKO 10:13-14). Sisi sote tunazaliwa tukiwa na dhambi ya asili. Tnazaliwa kwa mfano wa Adamu na si kwa mfano wa Mungu (ZABURI 51:5; ZABURI 58:3). Pasipo sheria hakuna dhambi, dhambi inahesabiwa kwa sheria (WARUMI 4:15; WARUMI 5:12-13). Mtoto anaweza kutenda dhambi kama vila kusema uongo, kutukana, uchoyo, ugomvi, kucheza dansi (mzikiwa kidunia), kuzira n.k .Lakini sasa watoto hawahesabiwi dhambi kwa kuwa hawajui mema na mabaya. Watoto hawana uwezo wa kupambanua au kutofautisha mema na mabaya. Wanafanya bila kujua kuwa ni dhambi, ndiyo maana Yesu alisema ufalme wa mbinguni ni wao.Kabla motto kuzaliwa duniani dhambi ilikuwa imekwisha kuwako. Adanu na Eva walitenda dhambi kabla ya kuwazaa watoto wao (WAEBRANIA 5:13-14). Mwenye uwezo wa kupambanua mema na mabaya ni mtu mzima, motto mdogo akifa anaenda mbinguni moja kwa moja bila kizuizi chochote.                                                        

                  YESU ALIWABARIKI WATOTO HAKUWABATIZA.

 Yesu mwenyewe aliwabariki watoto hakuwabatiza. Watoto wadogo wanabarikiwa tu haturuhusiwi kuwabatiza watoto wadogo. Ubatizo unafanya kwa mtu baada ya kulisikia Neno la Mungu na kutubu dhambi zake zote. Lazima mtu asafishwe dhambizake kwanza kwa damu ya Yesu kwa njia ya imani. Yesu mwenyewe alibarikiwa akiwa motto mdogo na kubatizwa akiwa mtu mzima (LUKA 2:27,34;  LUKA 3:21-23).

YESU KRISTO ALIBARIKIWA AKIWA MTOTO NA KUBATIZWA AKIWA MTU      MZIMA.

    Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni kielelezo au mfano wa jinsi tunavyotakiwa kuishi na kutenda , alibarikiwa akiwa motto mdogo (LUKA 2:27,34). Yesu Kristo akaonesha mfano kwa kubatizwa akiwa mtu mzima na akasema ndivyo inavyotupasa kuitimiza haki yote (LUKA 3:21-23;   MATHAYO 3:13-17). Tunaona Yesu alibarikiwa na mtumishi wa Mungu Simion akiwa motto mdogo, na kubatizwa akiwa na umri unaokaribia miaka thelathini. Tunapaswa kujifunza kwa Kristo (1 PETRO 2:21; 1WAKORITHO 11;1, MATENDO 2:37-41). Watu waliobatizwa wakati wa kanisa la kwanza walikuwa wengi sana hivyo walikuwa na umri wa miaka tofauti.Kigezo kinachotumika ni utu uzima, yaani uwe na uwezo wa kupambanua mema na mabaya (WAEBRANIA 5;13-14).

.UWEZEKANO WA KUBATIZWA MARA MBILI AU ZAIDI.

Wapo watu wengine watasema mimi nilishabatizwa tangu mwanzo toka utotoni, sasa itakuwaje baada ya kugundua kuwa nilibatizwa kimakosa?. Wapo watu ambao walibatizwa mara mbili katika biblia ingawa mwanzo walibatizwa katika maji tele (MATENDO 19:3-5). Ikiwa mwanzo tulibatizwa kwa ubatizo usio wa kibiblia, tunapaswa kubatizwa ubatizo wa kibiblia kama Yesu alivyosema tujifunze kwake (MATHAYO 11:29). Huhitaji kuomba ushauri kwa mtu yeyote, ni kulitii Neno la Mungu tu bila kulijadili kwanza. Ubatizo wa kibiblia unafanywa kwa mtu mara moja tu. Mtu anayetakiwa kubatiza sharti awe ni mwanafunzi wa Yesu. (YOHANA 4:2). Kama ulibatizwa bila kutubu dhambi kwanza huo sio ubatizo wa kibiblia ni sawa na mtu aliyeoga majini tu. Kama ulibatizwa utotoni unahitaji kutubu dhambi zako mwenyewe na ndipo utaweza kubatizwa kibibli. Kama ulinyunyiziwa maji kichwani au usoni hujabatizwa kibiblia. Lazima uzamishwe katika maji na ndipo unakuwa umeshiriki mauti ya Kristo (WAKOLOSAI 2:12,  WARUMI 6:4-5).

       TUNABATIZWA KATIKA MAJI MENGI ILI TUWE WA KRISTO.

       Hatuna budi kufahamu kuwa safari Yetu ya kuelekea mbinguni inafananishwa na safari ya wana wa Israeli kuelekea Kanani (1WAKORINTHO 10;11). Mungu alimtumia Musa kuwaokoa waisraeli mikononi mwa Farao ili wamtumikie na leo hii kamtuma Mwanae wa pekee Yesu Kristo ili kutuokoa kutoka utumwani mwa Shetanui  ili tumtumikie Mungu.

        Ni muhimu kufahamu kuwa ubatizo ulikuwepo  tangu zamani za agano la kale. Waisraeli walibatizwa ili wawe wa Musa (1WAKORINTHO 1O:1-2). Tunabatizwa sawasawa na agizo la Yesu ili nasi tuwe wa Kristo. Ni muhimu kufahamu kuwa kuzamisha katika maji tele kibiblia ni sawa na kuzikwa ndiyo maana ubatizo ni mara moja tu. Tunazikwa na kufufuka na Kristo kwa njia ya ubatizo. Hapa ndipo tunashiriki mauti ya Kristo (WAKOLOSAI 2:12). Utii wa kwanza kwa mtu baada ya kuokoka ni kukubalikuzikwa na kufufuka pamoja na Kristo (WARUMI 6:4-5). Kwahiyo kubatizwa katika maji mengi kunatufanya kushiriki mauti ya Kristo yaani kuzikwa na kufufuka kwake. Maji yanakuwa kama kaburi tu ambayo mtu anazamishwa ndani yake ili kushiriki mauti ya Yesu kibiblia (WAKILOSAI 2:12, WARUMI 6:4-5).

        KUWA TAYARI KUTIMIZA HAKI YOTE.

                          (MATHAYO 3:13-15)

 Yesu Kristo alisema “ndivyo inavyotupasa kutimiza haki yote”.Kutimiza haki yote maana yake nini? Tunaona maana ya haki yote katika (ZABURI 119:172) . Haki yote ni maagizo yote (ZABURI 119:6). Tunapaswa kutimiza haki yote (maagizo yote ) ya Yesu. Yesu Kristo alitimiza haki yote ingawa alikuwa hana dhambi na ndiyo maana Yohana mbatizaji  alishangaa na hakutaka kumbatiza akisema kuwa yeye hastahili kabisa kumbatiza. Tunatakiwa kuwa tayari kutimiza haki yote kama Yesu alivyofanya. Wana wa Israeli walibatizwa mara tu walipotoka katika utumwa wa Farao na sisi tunapaswa kubatizwa mara tu tunapotoka katika utumwa wa dhambi au utumwa wa Shetani.    

 • Je, wanafunzi wa yesu walibatizwa?

     Ni muhimu kufahamu kuwa  kuna mambo mengi sana aliyoyafanya Yesu  lakini hayakuandikwa, ndiyo maana habari zingine hatuzikuti katika maandiko. Lakini haya yaliyoandikwa yanatosha kutuongoza katika njia ya Bwana. Kwa mfano, neno Television halipo katika biblia lakini kuna andiko linalotukataza kuweka matendo maovu mbele za macho yetu (ZABURI 101:3). Yesu Kristo alifundisha yale aliyoyatendea kazi mwenyewe  (MATENDO 1:1). Yesu alibatizwa kwanza ndipo aliposema aaminiye na kubatizwa ataokoka. Pia aliowasimamia wanafunzi wake walipokuwa wakiwabatiza watu wengine (YOHANA 4:2). Kama wangelikuwa hawajabatizwa Yesu kristo asingeliwapa rkibali cha kuwabatiza wengine. Yesu aliwakabidhi kazi ya kubatizwa kwa kuwa hawakuwa wanafiki kama mafarisayo (MATHAYO 23:3-4)                                  

 • Je, paulo mtume alibatizwa katika maji tele?

   Katka kitabu cha ( MATENDO 9:18 )  biblia zetu za Kiswahili zinasema alibatizwa lakini hazielezi vizuri. Tafsiri nzuri tunaipata latika biblia ya kingreza tafsiri ya king James Vision,                              ACTS 9:18

18

And straightway there fell from his eyes as it were scales, and he received his sight; and he arose and was baptized;

Paulo mtume katka mafundisho yake alifundisha kwamba watu wamfuate yeye kama anavyomfuata Kristo (1 WAKORINTHO 11:1). Yesu ndiye aliyeagiza kuwabatiza watu mara wanapotubu dhambi zao. Tunamuona Paulo akibatiza (MATENDO 19:3-5). Kama yeye angekuwa hajabatizwa katika maji mengi asingewabatiza wengine katika maji mengi..

 • Je. Askari wa gereza na watu wa nyumbani mwake  walibatizwa katika maji tele?  

(MATENDO 16:30-34).

     Agizo la Yesu kwa wanafunzi wake kwa kila aaminiye kuwa ni sharti abatizwe, wanafunzi wake hawa walilitendea kazi. Tunaoan kuwa walibatizwa lakini kuna watu ambao siku hizi ambao hutafuta andiko la kupindisha  ukweli ili kuharalisha uovu wao

Bila shaka watumishi hawa waliwapeleka mahali penye maji mengi na kuwabatiza kwa kuwazamisha ili washiriki mauti ya Yesu kuzikwa na kufufuka kwake (WAKOLOSAI 2:12; WARUMI 6:4-5).

 • Kama mtu yupo mahali ambapo hapana maji mengi kama jangwani atabatizwa wapi?     

 (LUKA 14:28-32; MATHAYO 12:42)

Kwa Mungu hakuna udhuru wowote, yeye akiagiza haunabudi kulitendea kazi agizo hilo. Kwa gharama yoyote tunapaswa kuhakikisha tunatimiza haki yote kwa kubatizwa katika maji tele., Hatuna budi kusafiri kuyafuata maji yaliko kwa gharama yoyote. Kama Malkia wa Kushi aliweza kusafiri umbali mkubwa kwenda kuitazama hekina ya  Sulemani Yesu anasema huyo atawahukumu watu wenye udhuru wa umbali. Wanadamu wanatafuta visingizio ili wasibatizwe katika maji tele kibiblia.

 • Je, ikiwa nilibatizwa kwa kufuata mkumbo nifanye nini?

         Kama ulibatizwa kabla ya kutubu dhambizako na kuzaliwa marapili unatakiwa kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha na ndipo ubatizwe katika maji tele. Hii Ni pamoja na watu wote waliobatizwa utotoni kinyume na Neno la Mungu. Tumeona kuwa watoto wadogo hawabatizwi bali wanabarikiwa tu. Hata Yesu hakubatizwa akiwa motto, alibarikiwa akiwa motto na kubatizwa alipokuwa mtu mzima.. Lazima mtu ahubiriwe injili ya Yesu na aiamini na kutubu dhambi zake zote hapo anakuwa ametimiza sifa ya kubatizwa (MATENDO 2:37-41).

 • Je, ikiwa nilibatizwa na mtu ambaye hakubatizwa katika maji tele nifanye nini?

 Ikiwa tulibatizwa na mtu ambaye yeye mwenyewe hajabatizwa kibiblia tunapaswa kubatizwa mara ya pili. Mtu anayetakiwa kubatiza lazima awe ni mwanafunzi wa Yesu kwele kweli anayemfuata Yesu kwa kila jambo. Paulo alisema tumfuate yeye kama anavyomfuata Yesu Kristo (1WAKORINTHO  11:1).

 • Je, ikiwa  nilibatizwa na mtu ambaye haamini ubatizo wa maji tele nifanye nini?

Kama tulivyoona mwanzo, kazi ya kubatiza niya wanafunzi wa Yesu tu. Wanafunzi wa Yesu ni watu wote ambao wameokolewa kwa kutubu dhambi zao na kuwa tayari kuishi sawasawa na Neno la Kristo. Watu wote ambao wanatuimiza haki yote ikiwa ni pamoja na kubatizwa katika maji tele. Yeye mwenyewe anatakiwa awe amekwisha kubatizwa katika maji tele. Ikiwa ulibatizwa na mtu ambaye yeye mwenyewe hajaamini unatakiwa kubatizwa tena.

 • Je, kama mtu alibatizwa kibiblia hatimaye akarudi nyuma kiroho, akitubu atabatizwa tena?

Ubatizo wa kibiblia unafanyika mara moja tu kama vile Yesu alivyozikwa mara moja na kufufuka mara moja tu (WAKOLOSAI 2:12; WARUMI 6:4-5). Mtu akirudi nyuma kiroho, akitubu tene hatakiwi kubatizwa tena.

 • Je, tunabatiza kwa jina la nani?

(MATHAYO 3:13-16;  MATENDO 8:36-39; MATHAYO 28:19).

Ubatizo wa kibiblia unafanya kwa mtu mara moja tu. Tena tunabatiza kwa jina la Baba,na Mwana, na Roho mtakatifu. Tunachovya au kuzamisha mara moja tu na si mara tatu kama majina yalivyo. Tunazamisha mara moja kama Yesu alivyozikwa mara moja.

 • Je, mbona mitume wa yesu walibatiza kwa jina la yesu?

(MATENDO 19:3-5; MATENDO 10:48; MATENDO 8:14-17; MATENDO 2:38).

Kielelezo chetu siyo mitume bali ni Kristo. Paulo anasema tumfuate yeye kama anavyomfuata Kristo (1 WAKORINTHO 11:1). Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake, wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka (YOHANA 13;16). “Kwa jina la” ina maana “kwa ajizo la”. (ESTA 8:7-10). Hii ilikuwa inatumika hivyo wakati wa bablia lakini siku hizi ni tofauti na hapo zamani. (ESTA 13:16). Kwa jina la mfalme yaani kwa agizo la mfalme.  (ESTA 13:10). Walitaka kutofautisha ubatizo uliofanyika kwa jina la (agizo la ) Yohana na ubatizo wa jina la (agizo la ) Yesu. ( MATHAYO  3:4-6; 3:1-3). Kutokana na kwamba watu wengi walikuwa wameshabatizwa ubatizo wa Yohana, ndiyo maana mitume wakawabatiza tena kwa jina la (agizo la) Yesu. Yesu ni mkuu kuliko Yohana. Mitume walibatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu., kama lilivyo agizo lake Bwana wetu Yesu Kristo..Mungu akikuagiza jambo la kufanya, usipunguze wala usiongeze lolote au kusahihisha  (KUMBUKUMBU 12:32). Kwahiyo, tumeagizwa kubatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu (MATHAYO 28:19).

 • Je, kama mtu amebatizwa kwa roho, anaweza kubatizwa kwa maji tena?         (MATENDO 10:44-46).

Ubatizo wa maji mengi wa kibiblia ni kwa watu wote. Yesu alisema ndivyo inavyotupasa kutimiza haki yote. Yesu Kristo alionesha kielelezo kwa kutimiza haki yote. Kubatizwa kibiblia ni kushiriki mauti ya Yessu kwa kuzamishwa ambako ni sawa na kuzikwa, maji ni kaburi (WAKOLOSAI 2:12;;  WARUMI 6:4-5).

 • Je ubatizo wa nyumba yote unapotajwa katika biblia si pamoja na watoto wadogo?

(  MATENDO 18:8; 16:31-33 )

     Katika tamaduni za wakati wa biblia, watoto hawakuruhusiwa kuwepo eneo lenye watu wazima ndiyo maana wanafunzi wake Yesu walitaka kuwafukuza ( KUMBUKUMBU LA TORATI 3:5-6 ). Hata katika hesabu za watu watoto hawakuhusishwa katika hesabu ( 1 SAMWELI 22:19; EZRA 10:1; YEREMIA 40:7 ). Watoto hawakubatizwa katika familia zao ( 1 WAKORINTHO 1:10-11; MATENDO 10:1-2 ). Mtoto mdogo hawezi kumcha Mungu, hivyo biblia inaposema nyumba nzima ikabatizwa ina maanisha watu wazima.

 • Kubatizwa na kutokubatizwa ni sawa yaani hakuna umuhimu wowote wa kutahiriwa.

 ( WAGALATIA 6:12-15 ). Kutahiriwa maana yake ni nyingine na kubatizwa maana yake ni nyingine. ( MATENDO 15:1-2 ), Kutahiriwa ilikuwa desturi ya Musa, agizo la Toratui kwa Waisraeli ( WARUMI 2:28-29; WAKOLOSAI 2:11 ).

 

 • Mbona maandiko yanasema tusiweke msingi tena wa mabatizo.

( WAGALATIA 6:1-2 Jibu lake WAEBRANIA 5:11-14 ). Tusifundishe ubatizo wowote bali tufundishe neno la kuukulia wokovu kwanza ndio msingi wa kwanza

 • Je mtu anapobatizwa ni lazima kubadilisha jina?

 Si lazima isipokuwa pale majina yetu yanapokuwa na ushuhuda mbaya kwa jamii inayotuzunguka nay awe na ushuhuda wa Kristo. ( 2 WAKORINTHO 3:2-3 ) Sauli baada ya kuokoka alibadili jina lake akawa Paulo. Unabadili jina lako na siyo jina la baba yako kwani wewe ndio umeamini yeye bado.

 • Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanywaje?

( 1 WAKORINTHO 15:29 ). Kwa kutokujua watu walikuwa wanabatizwa kwa ajili ya wafu. Ubatizo wa Yohana ulijulikana kila mahali na watu bila kujua wakawa wanabatizwa na kubatiza kwa ajili ya wafu. Huo ni ubatizo wa kipagani. Waliokuwa wakifanya hivyo ni Wasadukayo ambao pia hawakuamini juu ya kiyama cha wafu            ( MATENDO 23:7-8 ).

 • Je mtu asipobatizwa kwa maji mengi hawezi kuingia mbinguni? Kama ndiyo mbona yule mnyanganyi aliingia?

( LUKA 23:33, 39-43 ). Yule mwizi alikiri kuwa ni mwenye dhambi na Yesu aliangalia moyo wake akaona ni moyo wa toba. Yesu alijua huyu angepata muda wa kutosha angeweza kufuata maagizo yote hata kubatizwa katika maji tele.. Mungu anaangalia moyo ndiyo maana alisema “ amwangaliaye mwanamke kwa kumtamani tayari kasha zini naye “.Huyu aliamini kuwa Yesu ni Mungu, pia ufalme wake ni wa Mbinguni.

 • Nikiamua kubatizwa kinyume na mafundisho au maagizo ya wazazi wangi si watanilaani.

                     ( EZEKIELI 20:18-19 )

Mungu anataka tuzishike amri zake, tusizishike amri za wazazi pale zinapokuwa kinyume na Mungu. (  HESABU 23;8; MITHALI 26:2 ).

 

 • Je kama katika dhehebu letu tunafundishwa kuwa ubatizo tunaobatizwa umepitishwa katika vikao vyao kama Mungu alivyosema ‘ lolote mtakalolifunga duniani na mbinguni litafungwa na litakalofunguliwa duniani pia mbinguni litafunguliwa”.

( ZABURI 119:6,9 ).  Tunapaswa kuangalia maagizo ya Mungu yote  siyo maagizo ya wanadamu. Utii uliochelewa pia unaitwa uasi ( ZABURI 119:60; WAGALATIA 1;15-17 ). Tunapojua kweli au kufahamu juu ya ubatizo wa kibiblia, huna haja  ya kumuuliza mtu yeyote wala mkuu wako wa dini. ( KUTOKA 23;2 ) Mtu hatakiwi kujisifu au kutegemea watu wengine.

         TUBUNI MKABATIZE SAWASAWA NA AGIZO LA YESU

                                   MATENDO YA MITUME 2:38

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!

Advertisements
By neno la uzima

8 comments on “UBATIZO WA MAJI MENGI WA KIBIBLIA

 1. Ndg davidcarol719,

  Shalom!

  Maelezo uliyoyatoa ni mazuri saana, ila yangependeza zaidi iwapo yoote katika ujumla wake yangesimama na Maandiko, hiyo Biblia; bali naona umeleta mchanganyiko wa Neno la Mungu na Mafundisho ya kidhehebu, kwa hiyo utenzi woote uliouleta, kimsingi ni mauti!!

  Haya maelezo uliyoyaleta:
  “”Je, tunabatiza kwa jina la nani?
  (MATHAYO 3:13-16; MATENDO 8:36-39; MATHAYO 28:19).
  Tena tunabatiza kwa jina la Baba,na Mwana, na Roho mtakatifu.””
  Pia:
  ““Je, mbona mitume wa yesu walibatiza kwa jina la yesu?
  (MATENDO 19:3-5; MATENDO 10:48; MATENDO 8:14-17; MATENDO 2:38).
  Kielelezo chetu siyo mitume bali ni Kristo. Paulo anasema tumfuate yeye kama anavyomfuata Kristo (1 WAKORINTHO 11:1). Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake, wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka (YOHANA 13;16).
  Mitume walibatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu., kama lilivyo agizo lake Bwana wetu Yesu Kristo..Mungu akikuagiza jambo la kufanya, usipunguze wala usiongeze lolote au kusahihisha (KUMBUKUMBU 12:32). Kwahiyo, tumeagizwa kubatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu (MATHAYO 28:19).””

  Maelezo haya yote ni tungo za kidhehebu tu! Huyo Yesu unayedai kumfuata, wewe umemjulia wapi kama si kupitia mitume? Unaposema kielelezo chako ni Yesu na si mitume, ni jambo la ajabu sana, kama Yesu aliwatuma hao wakuletee wewe habari zake, kauli kama hiyo uliyoitoa ni dharau kwa huyo aliyewatuma, sasa sijui unategemea huyo Yesu akupokee wewe uliyewadharau hao aliowatuma??

  Jambo la dhahiri ni kuwa roho aliye juu yako si yule aliyekuwa ndani ya mitume. Hata kauli yako kuwa mitume walibatiza kwa “jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu” ni jambo la uongo linalodhihirisha utofauti wa roho atendaye kazi, maana sijawahi kuona Andiko lolote kuhusu hilo! Basi iwapo una ujasiri wa jinsi hii, hilo pekee lakuhitaji ujitazame mara mbili ujikague katika kipimo cha Neno, maana hakuna mkristo yeyote yule katika Biblia aliyebatizwa kama ulivyobatizwa wewe!!

  Rudi tena katika Maandiko, jinyenyekeze kwa hayo, na kisha utubu haya unayoyafundisha, ndipo ubatizwe kama Biblia inavyoagiza katika Mdo 2:38 ili upate ONDOLEO la DHAMBI, hizo ulizojiingiza ; maana Biblia inasema katika Gal.1:8 “Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.” Basi iwapo mitume walihubiri Ubatizo katika Jina la Bwana Yesu Kristo, wewe kuhubiri jambo la kuwabatiza watu katika titles ukizigeuza hizo kuwa jina na hivyo kuwakosesha ONDOLEO la DHAMBI, hilo si jambo la mzaha, na sioni utaikwepaje hiyo LAANA!

  Basi hebu tupe mfano wa jambo hilo unalolifundisha kwa ushahidi wa kutimizwa kwake katika Biblia, tuoneshe hata mtu mmoja tu aliyewahi kubatizwa kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, maana Maandiko yote uliyoyanukuu, hakuna hata Andiko moja linaloshuhudia jambo hilo!

  • @Lwembe

   Je, mbona mitume wa Yesu walibatiza kwa jina la Yesu?

   (MATENDO 19:3-5; MATENDO 10:48; MATENDO 8:14-17; MATENDO 2:38).
   Kielelezo chetu siyo mitume bali ni Kristo. Paulo anasema tumfuate yeye kama anavyomfuata Kristo (1 WAKORINTHO 11:1). Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake, wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka (YOHANA 13;16). “Kwa jina la” ina maana “kwa ajizo la”. (ESTA 8:7-10). Hii ilikuwa inatumika hivyo wakati wa bablia lakini siku hizi ni tofauti na hapo zamani. (ESTA 13:16). Kwa jina la mfalme yaani kwa agizo la mfalme. (ESTA 13:10). Walitaka kutofautisha ubatizo uliofanyika kwa jina la (agizo la ) Yohana na ubatizo wa jina la (agizo la ) Yesu. ( MATHAYO 3:4-6; 3:1-3). Kutokana na kwamba watu wengi walikuwa wameshabatizwa ubatizo wa Yohana, ndiyo maana mitume wakawabatiza tena kwa jina la (agizo la) Yesu. Yesu ni mkuu kuliko Yohana. Mitume walibatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu., kama lilivyo agizo lake Bwana wetu Yesu Kristo..Mungu akikuagiza jambo la kufanya, usipunguze wala usiongeze lolote au kusahihisha (KUMBUKUMBU 12:32). Kwahiyo, tumeagizwa kubatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho mtakatifu (MATHAYO 28:19).Tunajifunza kwa Yesu ( MATHAYO 11:29, 1 WAKORINTHO 11:1 ). Watu wote tunapaswa kuwa na ubatizo mmoja ( WAEFESO 4:5 ). Mungu akubariki sana.

 2. @ davidcarol719
  Hivi, Baba ni jina?
  Au, Mwana ni jina?
  Au, Roho Mtakatifu ni jina?
  Na kama hayo ni majina, kwa nini agizo liseme “Jina” na si majina?
  Je, kama Mwana ni jina, Yesu itakuwa nini?
  Pia, unaweza kutupatia Andiko lolote linalomuonesha yeyote yule aliyewahi kubatizwa kwa jina la Baba na la mwana na la Roho Mtakatifu?

  Ubarikiwe

  • @ Lwembe
   Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni majina. Nilichogundua ni kwamba wewe huamini juu ya utatu mtakatifu wa Mungu.Nitakuandalia somo hivi karibuni ya uthibitisho wa utatu kibiblia.
   kuhusiana na ubatizo tunamfuata Yesu na maagizo yake.(MATHAYO 28:19)

 3. Ndg davidcarol719
  Bwana Yesu asifiwe!
  Ninakushukuru kwa kuniandalia hilo somo lihusulo UTATU MTAKATIFU. Hilo ni jambo jema na lenye kutia moyo. Napenda kukuhakikishia kuwa nitalipitia kwa utulivu ili nami nipate kujifunza kuhusu jambo hilo kutoka katika hazina uliyonayo ya Neno la Mungu.

  Kuhusu Ubatizo, umenukuu hapo kuhusu kumfuata Paulo, “Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo”, naona kama umechanganya mambo, maana unaelezea tena ukuu wa bwana kwa mtumwa wake, na hapo hapo huyo mtumwa anatuambia tumfuate yeye, sijaelewa unakuwaje umemfuata mtumwa ilhali umeikataa tafsiri ya maagizo ya Bwana wake aliyokabidhiwa akuletee! Na pia hayo unayosema ya huyo Bwana wake, yeye huyo mtumwa ndiye aliyekuletea, mimi nadhani kwa kukataa kimoja basi umevikataa vyote!!

  Neno linasema hivi: “Basi wakamwambia, Tufanyeje ili tupate kuzitenda kazi za Mungu? Yesu akajibu, akawaambia, Hii ndiyo kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa na yeye.” (YN. 6:28-29 SUV)

  Huyo Yesu unayedai kumfuata, ndiye ALIYEWATUMA mitume kuja kutuhubiria sisi Injili, “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” (MT. 28:19-20 SUV)

  Sasa mtu anayemfuata Yesu na si mitume, anafanya kazi ya nani? Maana mwenye kufanya kazi ya Mungu, kazi yenyewe ndiyo hiyo kama mwenye kazi anavyoiainisha!

  Na pia unaniambia kuwa Mwana ni jina, basi hapo Yesu anaposema, kwa jina langu mtatoa pepo, kwanini hatukemei pepo kwa jina la Mwana? Pia tunaagizwa, “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu.” Basi Ubatizo si tendo? Au mitume hawaelewi wanachokifanya? Au Roho Mtakatifu aliwaacha? Na kama aliwaacha, kwanini ayaruhusu makosa yawe sehemu ya Neno lake?

 4. ni vigumu kumfungua macho mtu asiyeona huku anadai anaona, ni neema ya mungu pekee ndiyo itamfungua mtu kama huyo. utatu mtakatifu ni upagani wa wazi wazi sana ila mpaka unyenyekee na uwe tayari kusikia, kuelimishwa, kukubali na kisha kutubu kwa mungu mmoja yesu kristo kwa kuabudu miungu watatu kwa muda mrefu. fikiria, eti baba si mwana wala si roho,mwana si baba wala si roho na roho si baba wala si mwana. alafu mtu anasema ni mungu mmoja. fundisho hili la utatu haukwepo katika kanisa la kwanza, limeingizwa na kanisa katoliki na kuendelezwa na mabinti zake( madhehebu yoye likiwemo sabato,ingawa wao wanadai ndilo dhehebu lililosahihi) ndugu zangu karibia asilimia 95(kadirio) ya mafundisho ya kanisa katoliki yanapingana na biblia. kwa hiyo ukiona fundisho flani la kanisa katoliki kimbia usilikubali hilo

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s