KIUMBE ASIYE KUWA WA ASILI

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : http://www.youtube.com/user/bishopkak

SOMO:  KIUMBE ASIYE KUWA WA ASILI

Ni kawaida kabisa siku hizi  za sasa kuwakuta watu wanajiita  wameokoka wakiwa wavuta sigara, wachaza rapu n.k. Katika midoo yao  watakuwa wanasema hawa au wale ni mataifa lakini cha kushangaza  na wao wenyewe wanafanana nao. Hao wanaojiita wameokoka, utakuta wanachukuliwa na kila uovu na tama za kidunia. Kama vile Mapambo, kusuka nyele, kupaka rangi midomo na nyusi, wanja, kuvaa wigi n.k.

                          ( WARUMI 1:21-24 )

     “Kwa sababu , walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika; wkaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, nay a ndege, nay a wanyama, nay a vitambaavyo. Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tama za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao”

      Kama wangetokea wanafunzi wa Yesu wa kanisa la kwanza  wangewashangaa  sana kuwakuta katika hali hiyo. Tatizo kanisa limekuwa mbali na mafundisho ya msingi kwa mtu baada ya kuokoka.  Kama ilivyo kwa mtoto mchanga anapozaliwa hunyweshwa maziwa vivyo hivyo na kwa mtoto mchanga kiroho ( aliyezaliwa mara ya pili ) anapaswa kulishwa kufundishwa mafundisho ya kumfanya awe kielelezo na nuru ya ulimwengu.

      Mwanadamu anapozaliwa  kutoka katika tumbo la binadamu anaitwa “mwanadamu wa tabia ya asili au  kiumbe wa asili. Mwanadamu wa tabia ya asili hawezi kulipokea Neno la Mungu. Hawezi kuyapokea maneno ya roho au ya rohoni..

                          ( 1 WAKORINTHO 2:14-15 )

Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuuzi, wala hawezi kuyafahamu,  kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu  wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu”.

      Mtu wa tabia ya asili  akiambiwa usiibe yeye anasema bila  kuiba nitaishije ?  Neno  linakataza kunywa  mvinyo ( pombe ) lakini yeye atakataa kulipokea neno hilo  

                           ( MITHALI 23:20 ).

Usiwe  miongoni mwao wanywao mvinyo; ………………………”

      Mwanadamu wa tabia ya asili hawezi kulipokea neno la maungu.

Ukimfundisha mtu mwenye tabia ya asili kuhusiana na uvaaji wa mapambo na kumwambi ni kinyume na mapenzi ya Mungu. Yeye anasema nisipojipamba , nitawezaje kupendeza.        ( 1 PETRO 3:3-5; 1 TIMOTHEO 2:9-10 )

      Katika 1 PETRO 3:3-5  “Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi, bali kuwe utu wa moyoni usioonekana , katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu  mbele za Mungu. Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume wao”.

Neno mavazi linazungumzia mavazi ya mapambo ( subject matter ni mapambo )

      Katika 1 TIMOTHEO 2:9-10 ‘Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu”.

      Watachukuliwa na kila kiitwacho cha dunia  kwa sababu wao ni wa asili ya dunia

                                 (  YOHANA 3:31 )

“Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini,, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli”.

Mambo ya kidumia yapo hata makanisani.  Rapu nje ya kanisa na rapu hiyo hiyo tena ipo ndani ya kanisa, taarabu, ngwasuma, twangapepeta n.k, zote zieingizwa kanisani hivi karibuni. Kama wangekuja Mitume wa kanisa la kwanza wangelishangaa kanisa la leo linalotetea hayo yote na kusema hayana tatizo lolote kiroho.                                             Si kila mtu anayejiita  Mtume, Nabii, Mchungaji ambaye  ni wa kweli.

            ( 2 PETRO 2:1, UFUNUO 2:2 )

Watoto wa Mungu hawatendi dhambi ( 1YOHANA 3:4-10 ), atendaye dhambi ni wa Ibilisi. Kitu kilichokuwa kizuri  duniani  Paulo alikihesabu kama mavi  baada ya kuokolewa ( WAFILIPI 3:7-8 ). Wokovu wa sasa kwa waliowengi ni wokovu mamboleo ambao unakwenda na wakati. Unaweza kuona jinsi Makanisa ya Kipentekoste yalivyobadilika sana ukilinganisha na miaka ya 1970 na 1980. Wachungaji na walimu wa neno la Mungu wengi wameshauacha msingi wa neno la Mungu na wanafundisha mafundisho manyonge na laani ambayo hayawezi kuwabadilisha watu na kuwafanya wawe nuru ua ulimwengu. Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu ( YOHANA 8:47 ),”………… Hivyo ninyi  hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu”. Tunapaswa kujithibitisha  na siyo kujifariji kuwa tunaenda mbinguni na huku tukijua tunafanya yasiyotupasa kufanya ( 2 WAKORINTHO 13:5 )

Wana wa kuasi ( WAEFESO 5:6 ) Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana;  2:kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi”.( WAEFESO 2:1-3 ) “Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu  ambazo mliziendea zamani kwa kufuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi, ambao zamani,sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tama za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili nay a nia, tukawa kwa tabia yetu  watoto wa hasira kama na hao wengine”. Kawaida ya ulimwengu huu  ni pamoja na  kuvalia mawigi, suruali kwa wanawake, kuacha makwapa wazi,  kuvaa nguo za kuonesha matiti, nguo za kubana makalio, nguo fupi ju ya goti kwa wanawake n.k. Mtu aliyeokoka ni mwna wa kutii ( 1 PETRO 1:14 ). Mtoto wa Ibilisi tama za Ibilisi ndizo  apendazo kuzitenda. Mtoto wa Ibilisi anavaa mavazi ya Ibilisi ( MITHALI 7:10; YOHANA 8:44 ) Yeye ambaye ameokoka amri za Mungu kwake siyo ngumu ( 1 YOHANA 5:1-3 ). Hawezi kuvaa mawigi maana kuvaa mawigi ni kumkosoa Mungu..

 

YEYE ALIYEOKOKA NI KIUMBE ASIYE WA ASILI.

Mtu asiye kiumbe  wa asili anao uwezo wa kuushinda ulimwengu na mambo yake. Ligi za kidunia, anasa, starehe n.k. ( 1 YOHANA 5:4 ) Yesu aliwaambia wanafunzai wake kuwa  wao si wa ulimwengu huu ( YOHANA 17:16 ) Watoto wa Mungu si wa ulimwengu huu kama yeye aliyewaita asivyo wa ulimwengu. Kama unaona ndani yako kuwa haya huwezi kuyapokea ( kuyafanyia kazi ), ndio kipimo kuwa hujaokoka. Kila mtu kwa kuzaliwa, huzaliwa na asili ya dunia. Ndiyo maana kitoto kidogo kinasema uongo, kinaiba, kinagoma kunyonya, kucheza dansi, n.k bila kufundishwa na mtu.

 

          YESU KRISTO KIUMBE ASIYE WA ASILI

Yesu Kristo naye ni kiumbe asiye wa asili kwa sababu alizaliwa kwa Roho au kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ( MATHAYO 1:18-21 ). Yesu aliishi maisha ya ushindi bila kutenda dhambi kwa sababu ya kuzaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ( WAEBRANIA 4:14-15 ). Yesu si kiumbe wa asili kwa Sababu alizaliwa na Bikira bila mbegu yoyote ya kiume. Dhambi ya asili ya Adamu haikupata nafasi kwa kuzaliwa na bikira.

Kuzaliwa mara ya pili ni kukataa mambo yote na kutaka kufanya  mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo, mtu akitaka kuzaliwa mara ya pili sharti utubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha kabisa. Kuzaliwa mara ya pili ni kuumbwa upya katika roho na ndiyo maana unazaliwa kwa roho kama Yesu alivyozaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Mtu anapotubu dhambi zake kwa kumaanisha kuziacha anasamehewa dhambi na msamaha huo unaambatana na kupewa uwezo wa kushinda dhambi.                             ( 2 WAKORINTHO 5:17) . Mtu akiwa ndani ya Kristo Yesu ya kale yote yanapita, tazama yanakuwa mapya.. Mariamu alimuuliza Malaika, “ litawezekanaje jambo hili maana simjui mume ( LUKA 1:31,34-35 ). Unaweza kuuliza, inawezekanaje mtu kuishi akiwa mbali na uvaaji wa mawigi, mapambo,bila kusuka,  bila kushabikia ligi za michezo, bila kuangalia filamu na picha zote za maigizo n.k? Yote yanawezekana kuwa mbali na wewe ukihitaji uwezo wa Yesu aliyeushinda ulimwengu. Ni muhimu kufahamu kuwa hatutaingia mbinguni kwa majina yetu yaliyoandikwa katika Makanisa yetu au Madhehebu yetu bali ni kwa UTAKATIFU TU ( WAEBRANIA 12:14 ). Kuna tofauti ya kuokoka na kutakaswa, hata wanafunzi wa Yesu tunaona walikuwa hawajatakaswa ( YOHANA 17:17 )., Waitwao ni wengi ( wanaokoka ) lakini wateule ni wachache  ( Watakatifu ).. Kuwa mtakatifu ni kuwa na tabia ya Mungu ndani yako ( MATHAYO 5:48; 1PETRO 1:15-16 )..

Ili uweze kuingia mbinguni lazima uokoke.

Je, uko tayari kuokoka au kuzaliwa mara ya pili?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii kwa dhati. “Mungu wangu, hakika mimi ni mwenye dhambi, kwa kuzaliwa na kwa kutenda.  Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Mungu wangu, nisamehe dhambi zangu zote, na kuniumba upya katika Kristo Yesu, ili nizaliwe mara ya pili sasa, nikiwa na asili mpya inayoniwezesha kushinda dhambi.  Kwa imani, napokea  msamaha na kuamini kwamba nimezaliwa mara ya pili sasa katika Jina la Yesu.  Amen”.  Mpendwa, tayari sasa umeokoka. Ili uzidi kuwa na ushindi dhidi ya dhambi, inakupasa kuhudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu (ZABURI 119:11       )

                             . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook, Twitter n.k,  kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe).  MUNGU AKUBARIKI

Advertisements
By neno la uzima

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s