TAJI KWA WATAKATIFU NA HARUSI YA MWANAKONDOO

ZACHARY KAKOBE

Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

 

SOMO: TAJI KWA WATAKATIFU NA HARUSI YA WANAKONDOO

Tuliona katika somo la kunyakuliwa kwa kanisa jinsi ambavyo watakatifu watakavyo nyakuliwa wote kwa pamoja-wale walioko mbinguni ambao watarudi katika miili yao kwa ufufuo na sisi tuliopo sasa baada ya kubadilishwa miili tena kufumba na kufumbua , tutaanza kwenda mawinguni kwa kupaa na kwenda kumlaki Bwana Yesu mawinguni. Somo letu la leo tutaangalia yale yatakayofuata tangu kipindi hicho cha kuanza kupaa. Tutaligawa somo letu katika vipengele sita ( 6 ) vifuatavyo:

 1. KUONDOKA KWA SHANGWE KWA WATAKATIFU.
 2. KITI CHA DHAWABU AU TAJI.
 3. KUJARIBIWA KWA KAZI YA KILA MTU.
 4. AINA ZA TAJI ZITAKAZOTOLEWA KWA WATAKATIFU.
 5. HARUSI YA MWANAKONDOO
 6. JINSI YA KUJIWEKA TAYARI KUYASHIRIKI HAYA YOTE.
 1. KUONDOKA KWA SHANGWE KWA WATAKATIFU

Wakati wa kuondoka, kwa muda mfupi sana tutafundishwa nyimbo mbili na Mungu mwenyewe. Wimbo mmoja unaitwa wimbo wa Musa na mwingine unaitwa wimbo wa MwanaKondoo ( UFUNUO 15:3-4 ).Mungu alimfundisha wimbo Musa na kumwambia awafundishe wana wa Israeli ili waukumbuke wakati Mungu atakapo waka hasira juu yao na kuwaacha ( KUMBUKUMBU 31:17-19 ; KUMBUKUMBU 32 Yote ). Hiki kilikuwa kivuli cha mambo yajayo wakati tutakapoimba wimbo wa Musa na kuondoka, huku nyuma yetu hasira Mungu ikidhihirika kwa wenye dhambi waliobaki wakati wa dhiki kuu. Vilevile, Musa na wana wa Israeli baada ya kuwaona Wamisri wamekufa baharini, na kutenganishwa nao kabisa, waliimba wimbo wa Musa wakiwa wanaanza kwenda Kanaani ( KUTOKA 15:1-20 ). Sisi nasi itakuwa vivyo hivyo. Tutaimba wimbo wa Musa tutakapoanza kwenda Kanaani.Siyo hilo tu. Yesu Kristo alikuwa akiimba na wanafunzi wake. Alikuwa mwimbaji ( MARKO 14:26-27 ). Baada ya kumshinda Shetani pale msalabani, Yesu alishangilia kwa wimbo ( WAKOLOSAI 2:14-15 ). Wimbo huu ndio wimbo wa MwanaKondoo. Tutauimba tukiwa tunapaa juu mawinguni baada ya kumshinda shetani na majaribu yake yote. Halleluya.

 1. KITI CHA DHAWABU AU TAJI.

Biblia inataja mara kwa mara kwamba kutenda kazi kwetu katika wokovu kutazawadiwa. Tutapewa taji au dhawabu ( RUTHU 2:12; ZABURI 58:11; MITHALI 13:13;23:18; 24:20; ISAYA 40:10; 49:3-4; YEREMIA 31:16; MATHAYO 5:12; 10:41; 1WAKORINTHO 3:8; 9:25; 15:58; WAEBRANIA 10:35; 2YOHANA 1:18 ). Dhawabu hizi au Taji hizi atakuja nazo Yesu mawinguni na kila mmoja atalipwa kulingana na utumishi aliomfanyia Mungu katika kipindi chake cha wokovu; na zitatolewa mawinguni mara tu ya kumlaki Yesu ( UFUNUO 22:12; 2TIMOTHEO 4:8; LUKA 14:12-13 ). Yesu atakalia kiti kinachoitwa KITI CHA HUKUMU CHA KRISTO wakati wa kutoa Taji ( 2WAKORINTHO 5:10 ).Kiti hiki kwa Kiyunani kinaitwa BEMA. Ni kiti atakachokalia Yesu na kutoa hukumu kwamba nani apewe dhawabu ipi na taji ipi. Tungeweza kukiita kiti cha dhawabu au taji.

 1. KUJARIBIWA KWA KAZI YA KILA MTU.

Wakati wa BEMA kazi ya kila mtu aliyeokoka aliyoifanya katika kumtumikia Mungu itajaribiwa kwa moto ili ipate kufahamika dhawabu ipi atakayopata ( 1WAKORINTHO 3:12-15 ). Moto huu ni Mungu mwenyewe, Yesu Kristo ( KUTOKA 24:17; ISAYA33:14; WAEBRANIA 12:29 ). Kazi ya kila mtu itajaribiwa kwa kulinganisha na jinsi ambavyo Yesu Kristo mwenyewe angeifanya kazi hiyo kwa karama hizohizo alizopewa mtu yule.

 1. AINA ZA TAJI ZITAKAZOTOLEWA KWA WATAKATIFU.

Haitapendeza kabisa kumuona mtu ambaye hakupewa taji yoyote wakati alikuwa na muda wa kumfanyia kazi Mungu tofauti na yule mhalifu msalabani. Ni wajibu wetu kuwa na lengo la kupata taji zozote zifuatazo kwa gharama yoyote katika maisha ya wokovu.

 1. TAJI ISIYOHARIBIKA ( INCORRUPTIBLE CROWN ).

               1WAKORINTHO 9:23-25; 2TIMOTHEO 2:4-6 ,

Taji hii watapewa watakatifu ambao walifanya mambo yote kwa ajili ya injili ili kuishiriki pamoja na wengine. Walijizuia yote katika utoaji wao kwa ajili ya injili, walijizuia katika maombi yao pia walitumia vyote walivyonavyo, muda, ujuzi, vipawa, cheo chao, uwezo wao wote n.k; ili kuishiriki injili pamoja na wengine.

 1. TAJI YA KUJIONEA FAHARI ( CROWN OF REJOICING ).

1WATHESALONIKE 2:19; DANIELI 12:3,

Taji hii inaitwa taji ya kujionea fahari kwa sababu watakaoipata taji hii watang’ara kama nyota tofauti na wengine watakavyong’ara. Fahari yao itakuwa kubwa kuliko ya wengine. Mng’ao wao wa utukufu utakuwa mkubwa kuliko wengine. Taji hii watapewa wale waliowaleta WATU WENGI kwa Kristo kutokana na kushuhudia kwao au kuhubiri injili. Washuhudiaji wale waliozaa watoto wengi katika injili yao ya mtu kwa mtu au vinginevyo na wakawaongoza mahali ambapo watakuzwa kwa mafundisho na kuwa watenda haki.

 1. TAJI YA UZIMA ( CROWN OF LIFE )   YAKOBO 1:12.

Taji hii ni kwa wale waliopita katika mateso au mitihani mikubwa ya maudhi na kuchukiwa kwa ajili ya Kristo wakashinda. Hawakupenda maisha yao hata kufa               ( UFUNUO 12:11; MATHAYO 5:11-12; WAEBRANIA 11:24-26; ZABURI 129:2 ).

 1. TAJI YA HAKI ( CROWN OF RIGHTEOUSNESS ).2 TIMOTHEO 4:6-8

( a ). Taji hii ni kwa wale waliopenda kufunuliwa kwake Yesu Kristo. Wakati wote moyoni walisema “amina; na uje Bwana Yesu”. Walikuwa katika utakatifu wakati wote. Kila neno walilojifunza walilitendea kazi. Kwao hakukuwa na kurudirudi nyuma na kwenda duniani kwanza, halafu wakaendelea na wokovu kidogo, hivyo hivyo mpaka alipokuja Yesu akawakuta katika hali ya kutubu.

( b ). Taji hii pia ni kwa wale wote waliowatendea mema ADUI ZAO ( LUKA 6:34-36 )

 1. TAJI YA UTUKUFU ILE ISIYOKAUKA ( CROWN OF GLORY ).

             1 PETRO 5:2-4; MATAHYO 10:41-42.

( a ). Taji hii watapewa wachungaji, walimu, au watumishi wa Mungu wanaojitaabisha kuwafundisha wengine na kuwalea kwa njia zozote-Kuwafundisha kanisani na kuwapa huduma za kichungaji, kuandika vitabu au tracts au mandishi yoyote yanayowasaidia watu wengine kiroho.

( b ). Taji hii watapewa wale ambao wanachukua muda wao kuwafundisha watoto wachanga wengi wa kiroho mpaka wanakua. Namna yoyote ya kumsaidia mtu kujifunza, itapata dhawabu hii-Kumwazima au kumpa vitabu au kaseti ( kanda ) za mafundisho mwenzio, kumpa nauli aende kwenye mafundisho, kazi ya kuhudumia kanisani- Kubeba watoto au kufanya lolote ili watu wawe na raha ya kujifunza n.k.

( c ). Taji hii watapewa wale ambao wanawahudumia mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na walimu ili wapate urahisi wa kuzifanya kazi zao.

     5: HARUSI YA MWANAKONDOO.

Watu waliookoka wanaishi katika utakatifu, wanaitwa BIKIRA SAFI WA KRISTO ( 2 WAKORINTHO 11:2 ) na pia BIBI ARUSI WA KRISTO ( YOHANA 3:29 ). Baada ya kupewa taji, Yesu atatufanyaia karamu kubwa ya kutupongeza. Hii ndiyo karamu ya  Arusi ya MwanaKondoo ( UFUNUO 19:7-9 ). Hii itafanyika katika kipindi hichohicho cha miaka saba wakati huku duniani wako katika Dhiki Kuu.

     6  JINSI YA KUJIWEKA TAYARI KUYASHIRIKI HAYA YOTE.

( a ). Kuwa miongoni mwa watakatifu ( WAEBRANIA 12:14 ).

( b ). Kuifanya kazi ya Mungu kwa bidii na nguvu zote ( MHUBIRI 9:10; YOHANA     4:34-36; WARUMI 12:11; YOHANA 9:4; 1WAKORINTHO 7:29-35; 9:17 ).

         Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

         Masomo ya matukio ya mwisho wa Dunia. Unaweza kuingia kwenye link ya kila somo.
1. KUNYAKULIWA KWA KANISA
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/01/02/kunyakuliwa-kwa-kanisa/
2. DHIKI KUBWA
https://davidcarol719.wordpress.com/dhiki-kubwa/
3. TAJI KWA WATAKATIFU NA HARUSI YA MWANAKONDOO
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/02/10/taji-kwa-watakatifu-na-harusi– ya-mwanakondoo/
4. KUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI NA VITA VYA HAR-MAGEDONI
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/02/10/kuja-kwa-yesu-kristo-mara-ya-pili-duniani-na-vita-ya-har-magedoni/
5. MIAKA 1,000 YA UTAWALA WA YESU KRISTO DUNIANI NA VITA VYA GOGU NA MAGOGU
https://davidcarol719.wordpress.com/miaka-1000-ya-utawala-wa-yesu-kristo-duniani-na-vita-vya-gogu-na-magogu/
6. UFUFU WA WAFU
https://davidcarol719.wordpress.com/187-2/
7. JEHANUM YA MOTO
https://davidcarol719.wordpress.com/jehanum-ya-moto/
8. KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE CHA HUKUMU
https://davidcarol719.wordpress.com/229-2/
9. MBINGU MPYA NA NCHI MPYA
https://davidcarol719.wordpress.com/mbingu-mpya-na-nchi-mpya/

                                                          . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .         

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook ,Twitter n.k kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

                                                         UBARIKIWE NA BWANA YESU!!!

Advertisements
By neno la uzima

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s