KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE CHA HUKUMU

ZACHARY KAKOBE  Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

  SOMO:   KITI  CHA  ENZI  KIKUBWA  CHEUPE   CHA  HUKUMU 

                                                                       (  UFUNUO 20:11-15  )

Baada tu ya vita vya Gogu na Magogu vitakavyofanyika mwishoni mwa miaka elfu moja ya Utawala wa Yesu Kristo duniani, kutafuata ufufuo wa pili unaoitwa pia ufufuo wa Hukumu ( YOHANA 5:28-29  ) . Huu ni ufufuo wa wale waliotenda mabaya, yaani wote wenye dhambi waliokufa pasipo utakatifu, tangu nyakati za mwanzo kabisa za vizazi vya Adamu hadi wale wote watakaoliwa na moto kwenye Vita vya Gogu na Magogu (UFUNUO 20:7-9 ) . Hawa wote baada ya kufa kwao wamekuwa katika kipindi chote hicho kwenye mateso makali Jehanum ya moto . Hawa, watafufuliwa na kuirudia miili yao ya asili na kusimama mbele ya Kiti cha Enzi Kikubwa Cheupe cha Hukumu . Ili tuelewe yale yatakayofanyika hapa, tutaligawa somo letu katika vipengele saba.

( 1 )   HAKIMU ATAKAYEKALIA KITI CHA ENZI KIKUBWA

CHEUPE CHA HUKUMU

( 2 )   MAKUSUDI YA HUKUMU YA KITI CHA ENZI KIKUBWA

CHEUPE

( 3 )  WINGI WA WATU WATAKAOHUKUMIWA

( 4 )  WADOGO PIA KUHUKUMIWA

( 5 )   KIPIMO KITAKACHOTUMIWA KATIKA HUKUMU

( 6 )   KUFUNULUWA KWA SIRI ZOTE MBELE YA MASHAHIDI

WA MUNGU

( 7 )   HUKUMU YA MWISHO

( 1 )  HAKIMU ATAKAYEKALIA KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE CHA

         HUKUMU

Hakimu atakayekikalia kiti hiki ni Yesu Kristo . Yeyote leo anayemkana Yesu Kristo kuwa siyo mwana wa Mungu , atafahamu hapa kwamba hukumu yote iko chini yake ( YOHANA 5:22 ; MATENDO 10:38-41; 17:31; WARUMI 2:16; 2TIMOTHEO 4:1 ). Ni heri kufahamu mapema hivi leo kwamba Yesu ndiye hakimu na kuomba msamaha kwake, yeye yuko tayari kulehemu na kusamehe kabisa ( ISAYA 55:6-7 ). Yesu atakapokikalia kiti cha enzi kikubwa cheupe atakuwa mwenye hasira, huruma itakuwa mbali naye kabisa (  EZEKIELI 7:4; 8:18; WARUMI 2:4-5 ).

 

( 2 ). MAKUSUDI YA HUKUMU YA KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE.

Hukumu hii, haitakuwa na makusudi ya kuwaweka huru wenye dhambi fulani fulani. Ilivyo ni kwamba yeyote yule asiyemwamini Yesu Kristo hadi kufa kwake, ghadhabu ya Mungu inamkalia ( YOHANA 3:36 ). Mtu yeyote mwenye dhambi anapokufa, huenda motoni moja kwa moja. Mtu huyu huenda motoni bila kuelezwa ni kwa nini anapelekwa kwenye mateso hayo.   Makusudi ya hukumu hii itakuwa ni kumfahamisha kila mmoja aliye katika mateso ya Jehanamu uhalali way eye kupewa adhabu hiyo ya milele. Itadhihirishwa kwa kila mmoja mmoja kwamba adhabu ya moto wa milele ni malipo halisi aliyopata kadri ya matendo yake ( WARUMI 2:6 ). Yesu hapa atasimama kama mhukumu wa haki ( MATENDO 17:31 ).

( 3 ). WINGI WA WATU WATAKAOHUKUMIWA

Watu wanaokwenda Jehanum ni wengi sana kuliko wengi wanavyofikilia ( MATHAYO  7:13-14 ). Mbinguni kuna vitabu vya aina mbili, kitabu cha uzima ambamo huandikwa majina ya wale waliookoka ambao hudumu kutenda mapenzi ya Mungu ( LUKA 10:20; WAFILIPI 4:3 ). Wale waliookoka wasiodumu kutenda mapenzi ya Mungu, hufutwa majina yao na kuondolewa katika kitabu mbali na wokovu, majina yao yamo katika vitabu vya kumbukumbu, vitabu vya hukumu. Kwa kuwa watu hawa ni wengi sana, majina yao yako katika VITABU VINGI, lakini wale wa mbinguni wako katika KITABU KIMOJA CHA UZIMA ( UFUNUO 20:12 ). Hatupaswi kudanganyika kutokana na watu wengi wanaosema wameokoka huku maisha yao hayako nuruni na kufikiria kwamba wote hawa wataingia mbinguni. Gharika iliwaangamiza watu wote duniani na  kubakia WANANE TU walioingia safinani. Viwango vya Mungu vya utakatifu havibadiliki ( MATHAYO 5:48; 1PETRO 1:15-17; WAEBRANIA 12:14 ).

( 4 ). WADOGO PIA KUHUKUMIWA.

Wakubwa kwa wadogo, watakuwepo kwenye hukumu hii ( UFUNUO 20:12 ). Ni muhimu kuwashuhudia injili watoto wetu wadogo walio na akili ya kujua mema na mabaya, na kuwapa nafasi ya kutubu, na kuokolewa; au sivyo, tutahuzunika kuwaona wakiwa kwenye hukumu hii, wakiwa wametoka kwenye mateso ya moto. Mtoto mdogo mwenye uwezo wa kufahamu hesabu ya 59 + 68 ana upeo mkubwa wa kufahamu mema na mabaya. Katika injili yetu kwa watoto wa jinsi hii, tunatakiwa kutaja dhambi wanazoweza kuzielewa. Wizi wa kalamu, uongo, kutokuwatii na kuwaheshimu wazazi  n.k, baada ya mtoto kumwamini Yesu, huongozwa sara ya Toba. Baada ya hapo, fahamu kuwa ameokoka na endelea kumfundisha bila kubabaishwa na mambo ya kitoto anayofanya siku kwa siku. Ni muhimu kukumbuka kwamba ni watoto wadogo kabisa wasioifahamu sheria ambao ufalme wa mbinguni ni wao. Wengi wao huwa bado wana umri wa kukumbatiwa ( MARKO 10:13-16; WARUMI 4:15; 5:13 ).

( 5 ). KIPIMO KITAKACHOTUMIWA KATIKA HUKUMU.

Watu wengi wanafanya makosa makubwa pale wanapofikiria kwamba, watakwenda mbinguni kutokana na kufanya mambo yaliyo sana na mafundisho ya madhehebu yao au mchungaji wao.Hiki siyo kipimo kitakachotumiwa na Yesu katika hukumu. Wengi wanaojifariji kwa kutenda yaliyo halali kwa wachungaji wao au madhehebu yao, ingawa yako tofauti na maagizo ya Neno la Mungu; watakwenda katika mateso ya moto wa milele. Kipimo atakachotumia Yesu katika hukumu ni NENO LA MUNGU au INJILI ( WARUMI 2:16 ). Ni muhimu kuyalinganisha yale tunayoyafanya  na Neno la Mungu  na siyo mafundisho  ya madhehebu yetu  au Wachungaji na Maaskofu  wanaotuambia kufanya hili na lile  siyo lazima ( ZABURI 119:6, 9 ). Siyo hilo tu, kipimo cha Yesu katika hukumu kitakuwa  Neno la Mungu. Wale ambao hawakuwa  na Biblia kijijini kwao, wale ambao walikuwa mahali pasipokuwa na mafundisho, wale ambao walikatazwa na wazazi wao kuwa Wakristo, wote hawa watapotea  pasipo kuifahamu sheria.. Kukosa kufahamu yaliyo halali siyo udhuru utakaokubalika. Wale wanaoyafahamu mafundisho lakini hawayatendi waon pia wataangamia pamoja na kuyajua hayo ( MAMBO YA  WALAWI 5:17; WARUMI 2:11-14 ). Mungu anamtarajia kila mwanadamu kuyatafuta mafundisho ya kweli hata iwe mbali kiasi gani kama alivyo tayari kufuata elimu Ulaya au biashara nchi za nje ( MATHAYO 12:42 ).

( 6 ). KUFUNULIWA KWA SIRI ZOTE MBELE YA MASHAHIDI WA MUNGU.

Mmojammoja atasimama mbele ya kiti hicho cha Enzi kikubwa cheupe. Mahali hapo itakuwa ni aibu na kudharauliwa ( DANIELI 12:2 ). Kila mmoja ataonyeshwa matendo yake, maneno yake, mawazo yake na nia yake kwa mfano wa VIDEO iliyotuzwa kumbukumbu zake. Siri zote za wanadamu zitakuwa wazi hapo ( AYUBU 20:27; METHELI 26:26; MHUBIRI 22:14; LUKA 12:2; 1WAKORINTHO 4:5; WARUMI 2:16 ). Mahali hapo utawaona wahubiri wazinzi. Kila kitu kitaonyeshwa WAZIWAZI. Hatua zote za mtu kumshawishi mwanamke wa mtu hadi kuingia naye nyumba ya kulala wageni na kufanya uchafu wote, vyote vitaonyeshwa hapo mbele ya wote. Maneno yote ya mtu anayoyatamka, yatawekwa wazi hapo, na kwa kila neno mtu atahukumiwa ( MATHAYO 12:36-37 ). Mtu aliyekuwa anahudhuria mikutano ya injili bila kukata shauri kuokolewa, atajiona picha yake akiwa katika mikutano hiyo na wakati akirudi nyumbani atajiona anasema “siwezi kuokoka”. Wala walioshindwa kufanya hili na lile kwa visingizio kuwa ni wanajeshi, ni vijana wadogo n.k watawaona mashahidi wa Mungu walioyafanya waliyoyakataa wakiwa na hali zao. Watakatifu watakuwepo kuona kila mtu na kuwa mashahidi wa Mungu ( WAEBRANIA 12:1; MATHAYO 12:42; MALAKI 3:18; 4:1-2 ).

( 7 ). HUKUMU YA MWISHO.

Watu watajitetea kwa kilio hapo na kisema “mimi nilifanya miujiza kwa jina lako”, “mimi nilitoa pepo kwa jina lako”, mimi nilishuhudia na kufuatilia n.k, na Yesu atasema sikuwajua ninyi; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu ( MATHAYO 7:22-23 ). Kila mtu atatolewa hapo na kukamatwa kwa nguvu kisha atatupwa kwenye ZIWA LA MOTO. Ziwa la moto ni tofauti na kuzimu au Jehanum. Ziwa la moto kwa sasa halina mtu ndani yake. Wa kwanza kutupwa humo watakuwa Mnyama au mpinga Kristo na nabiii wa uongo ( UFUNUO 19:20 ). Kisha atafuata Shetani ( UFUNUO 20:10 ). Mateso ya ziwa la moto ni mazito zaidi kuliko Jehanum. Mauti au kifo ni Jehenum ya sasa, vyote pia vitatupwa katika ziwa la moto pamoja na wenye dhambi wote ( UFUNUO 20:14-15, 21:8 ). Hapo itakuwa “kwaheri ya kutokuonana tena” kwa wenye dhambi na watakatifu.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Mpendwa msomaji, baada ya kusikia yote haya kutoka kwa nabii aliyetumwa kukuletea ujumbe huu, usifanye moyo wako kuwa mgumu.  Hii ni nafasi ya kipekee ya kuokoka.  Je, unajuaje kama utaamka kitandani baada ya kulala usiku wa leo?  Wakati uliokubalika wa wokovu ni sasa (2 WAKORINTHO 6:2).  Labda utaniuliza, ili uokoke, ufanyeje?  Jibu ni rahisi, kwa imani ukitubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, na kumwambia Yesu Kristo akusamehe, utasamehewa sasa hivi, na msamaha wa dhambi, huambatana na wokovu (LUKA 1:77).  Je, uko tayari kuokoka sasa hivi?  Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii kwa dhati toka moyoni, Mungu baba asante kwa kuniletea ujumbe huu.Natubu dhambi zangu zote, kwa kumaanisha kuziacha. Yesu Kristo nakuomba unisamehe dhambi zangu na kunipa uwezo wa kushinda dhambi na kuniokoa kutoka katika mateso ya moto wa milele. Asante, kwa kuniokoa katika Jina la Yesu.  Amen.  Tayari sasa umeokoka, na kwa hakika unakwenda mbinguni sasa, hata ukifa leo.  Ili uzidi kuukulia wokovu, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

Masomo ya matukio ya mwisho wa Dunia. Unaweza kuingia kwenye link ya kila somo.
1. KUNYAKULIWA KWA KANISA
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/01/02/kunyakuliwa-kwa-kanisa/
2. DHIKI KUBWA
https://davidcarol719.wordpress.com/dhiki-kubwa/
3. TAJI KWA WATAKATIFU NA HARUSI YA MWANAKONDOO
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/02/10/taji-kwa-watakatifu-na-harusi– ya-mwanakondoo/
4. KUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI NA VITA VYA HAR-MAGEDONI
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/02/10/kuja-kwa-yesu-kristo-mara-ya-pili-duniani-na-vita-ya-har-magedoni/
5. MIAKA 1,000 YA UTAWALA WA YESU KRISTO DUNIANI NA VITA VYA GOGU NA MAGOGU
https://davidcarol719.wordpress.com/miaka-1000-ya-utawala-wa-yesu-kristo-duniani-na-vita-vya-gogu-na-magogu/
6. UFUFU WA WAFU
https://davidcarol719.wordpress.com/187-2/
7. JEHANUM YA MOTO
https://davidcarol719.wordpress.com/jehanum-ya-moto/
8. KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE CHA HUKUMU
https://davidcarol719.wordpress.com/?s=KITI+CHA+ENZI+KIKUBWA+CHEUPE+CHA+HUKUMU
9. MBINGU MPYA NA NCHI MPYA
https://davidcarol719.wordpress.com/mbingu-mpya-na-nchi-mpya/

               . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook, Twitter n.k  kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

UBARIKIWE SANA KWA KAZI YAKO NJEMA

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s