HAKIKA YA KUJIBIWA MAOMBI

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SIKU YA KUICHAMBUA BIBLIA

SOMO:    HAKIKA YA KUJIBIWA MAOMBI

L

eo, tunamaliza kutafakari SURA YA 14 ya Kitabu cha YOHANA katika Biblia zetu.  Tunachukua muda wa Siku ya leo ya Kuichambua Biblia, kujifunza YOHANA 14:13-31.  Katika mistari hii, pamoja na mambo mengine, tutajifunza kuhusu, “HAKIKA YA KUJIBIWA MAOMBI“.  Tutayagawa mafundisho yote tunayoyapta katika mistari hii, katika vipengele tisa:

(1)  KUOMBA KWA JINA LA YESU (MST. 13-14);

(2)  HAKIKA YA KUJIBIWA MAOMBI (MST. 13-14);

(3)  ALAMA YA KUMPENDA YESU (MST. 15, 21, 23-24);

(4)  MSAIDIZI MWINGINE (MST. 16-27, 25-26);

(5)  SITAWAACHA NINYI YATIMA (MST. 18-20);

(6)  FAIDA ZA KUZISHIKA AMRI ZA YESU (MST. 21-23);

(7)  MSIWE NA WOGA (MST. 27-29);

(8)  MKUU WA ULIMWENGU HANA KITU KWA YESU (MST. 30);

(9)  JINSI YA KUUJULISHA ULIMWENGU YA KUWA TUNAMPENDA BABA

        (MST.34).

 

(1)                          KUOMBA KWA JINA LA YESU (MST. 13-14)

Yesu Kristo aliye Bwana na Mwalimu wetu, hapa anatufundisha jinsi ya kuomba, ili maombi yetu yawe na uwezo wa kipkee wa kuleta majibu kutoka kwa Mungu.  Anatuelekeza kumwomba Mungu baba, kwa JINA LA YESU, na anarudia maelekezo haya tena na tena (YOHANA 16:23-24).  Shetani, adui yetu, hataki kuona maombi yetu yakiwa na uwezo, hivyo mbinu yake kubwa, ni kutufanya tuombe kinyume na maelekezo ya Yesu.  Atatufanya tuwaombe watakatifu Petro, Yohana, Yakoba, n.k.  watuombee.  Yote haya, ni kinyume na maelekezo haya ya Yesu.  Maelekezo ya Yesu kwetu ni “Nanyi Mkiomba“, kutufundisha wajibu weetu wa kuomba wenyewe.  Wanaotajwa kutuombea katika Biblia, ni WAWILI TU, Roho Mtakatifu na Yesu mwenyewe; na hawa hufanya hivyo kwetu, bila kuwaomba watuombee (WARUMI 8:26; 1 YOHANA 2:1).  Bikira Mariamu, anjitaja yeye mwenyewe kwkamba ni MJAKAZI WA BWANA, au mtumwa wa kike wa Mungu, na kamwe hajitaji kuwa Mama wa Mungu (LUKA 1;38).  Yesu kama Mungu hana mama (WAEBRANIA 7:3).  Bikira Mariamu, ni mama yake Yesu katika ubinadamu wake tu.  Bikira Mariamu, pamoja wanafunzi wengine wa Yesu, wote walimwomba Baba kwa Jina la Yesu (MATENDO 1:13-15).  Ktumia sanamu za watakatifu fulani katika maombi yetu, vivyo hivyo ni kinyume na maelekezo haya.  Mungu ni roho, inatupasa kumwabudu KATIKA ROHO NA KWELI, na kuikimbia ibada ya sanamu, maana sanamu hizi ni dhambi (ISAYA 31:7; ZABURI 135:15-18; 1 WAKORINTHO 10:14).

(2)                          HAKIKA YA KUJIBIWA MAOMBI (MST. 13-14)

Yesu Kristo hapa anatuelezea juu ya hakika ya kujibiwa maombi.  Anasema, tukiomba kama alivyotuelekeza kwa Jina la Yesu, hilo tunaloliomba, atalifanya.  Hata hivyo, hatuna budi kuviondoa vikwazo vingine vya kujibiwa maombi, vinavyotajwa katika maandiko, ili hakika ya kujibiwa maombi itende kazi kwetu.  Hatuna budi kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu au Neno lake (1 YOHANA 5:14-15; MATHAYO 20:20-23).  Hatuna budi pasipo kutaka kuvitumia kwa tamaa zetu (YAKOBO 4:3).  Hatuna budi kuomba pia kuwa mbali na dhambi au uasi wa sheria za Mungu (MITHALI 28:9; 15:29; YAKOBO 4:2), na pia hatuna budi kuomba kwa imani, pasipo shaka yoyote (YAKOBO 1:6-7).  Tukiondoa vikwazo hivi, hatuna budi kuwa na hakika ya kujibiwa maombi kwa wakati wa Mungu uliokubalika.

 

(3)                            ALAMA YA KUMPENDA YESU (MST. 15, 21, 23-24)

Wako watu wengi ambao wanassema wanampenda Yesu, hata hivyo, wengi kati yao wanapenda kwa neno tu, siyo kwa tendo na kweli (1 YOHANA 3:18).  Yesu anatufundisha alama itakayoonyesha kwa tendo na kweli kwamba tunampenda Yesu.  Alama hii, ni kuzishika amri zake zote, kulishika neno lake na kulitendea kazi kama lilivyo, bila kulijadili.  Yeyote anayesema anampenda Yesu huku hayashiki maneno yake, huyu ni mwongo.

 

(4)                          MSAIDIZI MWINGINE (MST. 16-17, 25-26)

Yesu Kristo alipokuwa duniani, alikuwa Msaidizi wa kipekee kwa wanafunzi wake.  Hata sasa anatusaidia sisi (2 WAKORINTHO 6:2; WAEBRANIA 2:18; 13:6).  Kabla ya kuondoka, anatutambulisha kwa Msaidizi mwingine.  Msaidi huyu, siyo Mtume Mohamed, kama wengine wanavyodai.  Msiaidizi huyu, ni ROHO WA KWELI, siyo mtu.  Ulimwengu hauwezi kumpokea, wala kumwona kwa macho, wala kumtambua; naye atakuwa NDANI ya wanafunzi wa Yesu, naye anakaa nao MILELE (MST. 16-17).  Sifa hizi zote, haziko kwa mtume yeyote mwanadamu.  Wengine wote hawakuwa ndani ya watu na pia hawakukaa milele!  Msaidizi huyu wingine ni ROHO MTAKATIFU (MST. 25-26).  Huyu hutusaidia udhaifu wetu wa kuomba (WARUMI 8:26), na kutufundisha na kutukumbusha yote, na kutuongoza atutie kwenye kweli yote.  Msaidizi huyu, ni wa muhimu mno kwetu ikiwa tunataka kuwa mashahidi wa Yesu (MATENDO 1:8).  Pasipo Msaidizi huyu, hatuwezi kuwaleta watu kwa Yesu kwa mfanikio makubwa (YOHANA 16:7-8).

(5)                          SITAWAACHA NINYI YATIMA (MST. 18-20)

Yesu hakutuacha yatima.  Siyo tu ametuachia Msaidizi mwingine, lakini tukiwa wawili watatu tumekusanyika kwa jina lake, yupo kati yetu katika roho (MATHAYO 18:20).  Kwa sasa tunamwona katika roho, hata hivyo atakuja kwetu wakati wa kunyakuliwa kwa kansia na tutamwona katika utukufu wake akiwa ndani ya Baba.

(6)                          FAIDA ZA KUZISHIKA AMRI ZA YESU (MST. 21-23)

Tukizishika amri za yesu, Baba na Mwana wote hutupenda.  Yesu akitupenda hivi, anajidhihirisha kwetu; kutuonyesha upendo wake katika kututendea mengi, katika roho na mwili.  Tukizishika amri za Yesu, Baba na Mwana, hufanya makao kwetu.  Wakifanya makao kwetu, hatutapungukiwa kitu, wala hatuna haja tena ya kuogopa lolote.

(7)                          MSIWE NA WOGA (MST. 27-29)

Woga, ni kinyume na imani (MARKO 4:40).  Woga hautokani na Mungu, bali Shetani (2 TIMOTHEO 1:7).  Tukiruhusu woga au hofu kututawala, tunampa Ibilisi nafasi ya kutupa adhabu (WAEFESO 4:27; 1 YOHANA 4:18).  Ikiwa baba, Mwana, wamefanya makao kwetu, na roho Mtakatifu pia yuko ndani yetu, na ni Msaidizi wetu, kwa nini tuogope kama kwamba tuko wenyewe?  Yesu kwa kutupa maelezo haya, anazidi kusema “Amani yangu nawapa“, Amani nawaachieni“.  Amani yake Yesu aliyotupa, itafuta kila namna ya hofu ndani yetu.  Kama tuna hofu, tupokee amani hii ndani mwetu, kwa imani.

(8)                          MKUU WA ULIMWENGU HUU HANA KITU KWA YESU (MST. 30)

Mkuu wa Ulimwengu huu yaani watu wa ulimwengu huu wenye dhambi, ni Ibilisi au Shetani (1 YOHANA 5:19; WAEFESO 2:1-2; WAKOLOSAI 1:13).  Yesu hapa, anatuhakikishia kwamba Shetani hana kitu chochote kwake.  Tunapoomba na kuliitia Jina la Yesu, hatuna haja ya kuogopa, Shetani hana kitu kwa Bwana wetu Yesu!  Majini yote hayana kitu kwake.  Hatuna haja ya kuogopa vitisho vya mapepo tukiwa na Yesu!

 

(9)                          JINSI YA KUUJULISHA ULIMWENGU YA KUWA TUNAMPENDA BABA (MST.

        31)

Hapa, Yesu anatuonyesha jinsi ya kuujulisha ulimwengu ya kuwa tunampenda Baba.  “Kama Baba  alivyomwamuru, ndivyo afanyavyo“, ni kielelezo cha Yesu kwetu.  Je, kama baba anavyotuamuru katika neno lake, ndivyo tufanyavyo?  Kama sivyo, hatumpendi Baba!

 

…………………………………………………………………………………………………………………………………..

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “somo” hili, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa pamoja nawe.

Advertisements

One comment on “HAKIKA YA KUJIBIWA MAOMBI

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s