HAKUNA PETE YA NDOA KIBIBLIA

SOMO:    HAKUNA PETE YA NDOA KIBIBLIA

Ni muhimu kufahamu kuwa neno pete limetajwa katika Biblia. Sasa kama neno hili limetajwa katika biblia. Je, tuvae pete kwa kuwa tu imetajwa au tuyachunguze maandiko kwanza kuona kama inakubalika kibiblia?.

Ni muhimu kufahamu kuwa hata madhehebu yanayoharalisha ushoga wanatumia andiko kimakosa ili kutetea kile wanachokifanya. Andiko wanalolitumia ni (MWANZO 2;18) “Bwana Mungu akasema, si vema  huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi  wa kufanana naye”. Wanasema kuwa, msaidizi wa Adamu hakuwa  mwanamke kutokana na neno “wa kufanana naye”.

Tunaona katika madhehebu mengi ya Kikristo, ndoa inapofungwa au inapobarikiwa huwa kuna tendo la kuvalishana pete. Pete hiyo huitwa pete ya ndoa. Pete ya ndoa hupewa heshima kubwa sana kiasi kwamba mtu aliyeoa au kuolewa akionekana hajaivaa haeleweki vizuri kwa waumini wa madhehebu mengi ya Kikristo na wale wasio wakristo.. Msingi wa imani hii ya uvaaji wa pete ya ndoa ni nini? Sisi wakristo tunaongozwa na Neno la Mungu tu, hatuongozwi na mapokeo. Kwa kila tendo lolote la kiimani tunalilifanya hatuna budi kuyachunguza maandiko kwanza kuona kama ni la kibiblia au ni maagizo tu ya wanadamu (mapokeo)..

Tunajifunza kwa Adamu na Hawa, wazazi wetu wa kwanza. Mungu aliyeunganisha ndoa yao hakuwavalisha pete ya aina yoyote. Kama hawakuvalishwa pete au kuvalishana wenyewe ndoa yao ilikuwa haijakamilika kwa kukosekana kwa pete ya ndoa? Wachungaji na walimu wote wa Biblia, wanapaswa kujua kuwa kazi yao ni kuwaombea wana ndoa kwa ajili ya Baraka tu. Mungu ndiye anayewaunganisha hao wawili waliopatana. Ni wakati gain basi Mungu anawaungani8sha? Wakati wazazi wa pande zote mbili (mume na mke) wanapokutana kwa ajili ya makubaliano ya mahali kutolewa au kutotolewa na kufikia muafaka na kutoa Baraka zao kwa watoto wao, hapo ndipo Mungu anawaunganisha hao wawili kama mke na mume kwa sababu ya  makubaliano ya wazazi (MATHAYO 1:18-21; MATHAYO 19:4-6). Kama Mungu mwenyewe hakutumia Pete hiyo inayoitwa ya ndoa wakati wa kuwaunganisha Adamu na Hawa, kwa nini sisi tufanye hivyo?   Tumezoea kuwaona wachungaji wakimuuliza kwanza bwana harusi kama anakitu chochote kwa ajili ya nadhiri mbele za Mungu kuwa hatamwacha mkewe. Mwanaume hutoa pete na kwa maelekezo ya mchungaji, humvalisha mkewe. Kwa mwanamke au bibi harusi hufanyika vivyo hivyo. Pete inatakiwa kuwa ya mzunguko bila maungio yaani mwanzo na mwisho wake. Je, unafahamu kwa nini pete haitakiwi kuonesha maungio yaani mwanzo na mwisho wake? Jibu ni kwamba wanadai maana yake “upendo  hauna mwanzo na mwisho”.. Hii siyo kweli. Mwanzo wa upendo ni pale walipokutana na kuanzauchumba na mwisho wa ndoa yao au upendo ni pale tu kifo kitakapowatenganisha .

HOJA YA WACHUNGAJI NA WATU WANAOVAA PETE YA NDOA.

Hoja kubwa wanayoitumia kutetea uvaaji wa Pete ni Isaka na Rebeka. Ni kweli tunaona katika Biblia Isaka akimvalisha  hazama na vikuku mchumba wake Rebeka. Kama nilivyotangulia kusema mwanzo kuwa, hata wale wanaoruhusu ushoga wanatumia vibaya maandiko ili kuhalarisha kile wanachokitaka. Andiko linalotumiwa na walimu wengi wa Neno la Mungu kuhalarisha uvaaji wa pete kwa wanandoa ni (MWANZO 24:29, 47).Kuna mambo muhimu ya kujifunza hapa katika andiko hili linalotumiwa na mamilioni ya watu Duniani kote, kutetea uvaaji wa pete ya ndoa. Nakuomba usome Biblia yako mwenyewe ili ujionee uongo wa Shetani. Biblia inasema (MWANZO 24:29, 47), “Na Rebeka alikuwa na kaka, jina laku Labani. Labani akatoka mbio kumwendea yule mtu kisimani. Kisha nikamwuliza nikasema, U  binti wa nani wewe?  Naye akasema, Mimi ni binti Bethueli, mwana wa Nahori, Milka aliyemzalia. Nami nikamtia hazama puani mwake na vikuku mikononi mwake”.Tuangalie maana ya maneno mawili hapo yaliyotumika, hazama na vikuku.

1. Tunaona kuwa Isaka alimvalisha Rebeka hazama puani.. Hazama maana yake ni pete ya puani..Maana hii inapatikana katika tafsiri ya maneno magumu katika Biblia, mwishoni mwa Biblia. Isaka alimvalisha heleni ya puani kwa namna inavyoitwa leo. Leo haitumiki heleni, tene haivalishwi puani bali kidoleni. Pia ni muhimu kufahamu kuwa siyo agizo la Mungu kwetu kufanya tendo hilo la Isaka na liko kinyume maandiko…

2. Isaka alimvalisha  vikuku (bangili) mikononi mwake. Mbona tendo hili la kuvalishana bangili linaachwa na hao wanaotetea uvaaji wa pete za ndoa?. Hata hivyo, uvaaji wa vikuku ni kinyume na Neno la Mungu.

3. Hio siyo agizo la Bwana na ndiyo maana tunaona Mungu mwenyewe akichukizwa na watu waliovaa pete, vikuku na mapambo mengineyo. Soma maandiko haya [ ISAYA 3:21, 16-24; HOSEA 2:13;  MWANZO 35:1-5; KUTOKA 33:4-6; YEREMIA 4:30; 1TIMOTHEO 2:9-10; 1PETRO 3:3-5]. Mapambo ni wavazi ya waabudu miungu, yanahusianishwa na ibada ya miungu (mashetani) [HOSEA 2;13; MWANZO 35:1-5].

Wanasema eti pete ni mfano wa upendo usio na mwanzo na mwisho. Hii si kweli, mwanzo wa upendo ni pale walipokutana na wakapendana na mwisho wa upendo ni pale mmoja  anapofariki na kumfanya mwenzake kuwa huru kuolewa au kuoa. Yesu alisema mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa. Hutapewa mke wako au mume wako uishi nae huko mbinguni.Yote hii ni janjajanja ya Shetani anayekuja kwa mfano wa malaika wa nuru ili kutufanya tuingize mapambo katika nyumba ya Mungu na kujenga ngome za mashetani kwa visingizio  kwamba mimi nimevaa pete sasa ni mke wa mtu au mume wa mtu. Mbona nyumba za wageni (guest houses) zimejaa watu wenye pete za ndoa? Kama pete hizo zingekuwa zinawafanya watu wasiwe makahaba, tusingekuwa na matatizo tuliyonayo leo.

Hazama aliyotumia Isaka ni pete ya puani (herein). Wanadamu wameenda mbali sana, siku hizi kuna pete za kitovuni, pete za mdomoni (kwenye lips), pete za  kwenye nyusi, pete za kwenye miguu, pete za masikioni n.k. Ushetani huo umetujia ili tumfanye Shetani atawale badala ya Yesu Kristo. Tumfanye Yesu ndiye atawale maishani mwetu kwa  kuhakikisha kila tunachovaa ni kwa utukufu wa Mungu. Tunatafuta kumpendeza Mungu na si wanadamu (ZABURI  73:25; WAGALATIA 1:10). Biblia inasema tumtukuze Mungu katika miili yetu.

Mtu aliyezaliwa mara ya pili (kwa roho) atakuwa na utayari kuyatendea kazi maneno haya na hayatamvuruga kabisa. Mtu aliyezaliwa mara ya pili wakati wote anatafuta kufanya mapenzi ya Mungu, akisikia kuwa hivi ndo mapenzi ya Mungu hahitaji hata mjadala wa kuyatendea kazi hayo. Si mapenzi ya Mungu kabisa sisi tuvae pete za aian yoyote. Mwanzo wa pete za ndoa ni wakati kanisa lilikuwa katika kipindi cha giza na upentekoste ulikuwa umekufa kabisa. Ndio kipindi ambacho ubatizo wa maji tele  ulikufa, kubatza watoto kukaanza, ibada za sanamu zinazoitwa za Yesu zilianza, na vitu vingine vvingi ambavyo vyote ni mapokeo, viko kinyume na Neno la Mungu.

Kama vile mchawi anavyochoma uchawi wake baada ya kuokoka na kama vile kahaba anavyopaswa kuiacha kazi yake baada ya kuokoka. Pia kama vile mwizi anavyoacha kazi yake ya kuiba baada ya kuokoka ndivyo kila mtu anapaswa kuyatendea kazi maneno ya Mungu. Lazima tufanye matendo yanayoambatana  na kutubu kwetu. Kahaba anapookolewa anapaswa afundishwe ili awe safi kwa kuondokana na tabia yake  ya mwanzo. Atakuwa mwanzo alikuwa na mavazi yasiyofaa, mavazi ya kikahaba (MITHALI 7:10) kwa hiyo pasipo mafundisho makahaba wataendelea kuvaa mavazi yao ya kikahaba hata kanisani. Hata katika madhehebu mengi siku hizi hakuna mafundisho ya kukemea dhambi. Kusisitiza juu ya maisha ya utakatifu ambayo pasipo hayo hakuna atakayemwona Mungu (WAEBRANIA 12:14). Siku hizi makanisa mengi yamekuwa makanisa vuguvugu, watu wana wokovu bandia. Watu wanaitwa ni wapendwa lakini uwezo wa kushinda dhambi ndani yao hakuna. Hawana uwezo wa kuushinda ulimwengu. Ndiyo maana hata ukiwafundisha kuwa kujipamba ni dhambi mbele za Mungu, watakupinga tu hata kama umetoa ushahidi wa maandiko mengi ya  kutosha. Paulo mtume alitabiri juu ya nyakati hizi za mwisho. Alisema utakuja wakati ambao watu watayakataa mafundisho yenye uzima (ya kweli) na kujiepusha wasisikie niliyo Kweli, kwa kuwa wana masikio ya utafiti, watajitafutia walimu makundi makundi 9wawatakao, wawapendao). [2 TIMOTHEO 4:3-5]. Hata wakati wa nabii Isaya walikuwepo watu wa namna hii. Wao walikuwa wakiwatafuta walimu wa kuwadanganya, wakitaka kufundishwa mafundisho laini yadanganyayo (ISAYA 30:9-10). Ole ni kwa waumini au washirika ambao  imani yao wameijenga kwa wachungaji au walimu wao wa Neno la Mungu. Hapa nawazungumzia wote wasiotaka kuongozwa na Neno la Mungu eti wakisubirii mpaka mchungaji au mwalimu wake afundishe hilo alilolisikia kwa mtumishi wa Mungu. Kuna watumishi wengi watakataliwa na Bwana Yesu siku ya mwisho kwa kutotimiza haki yote ya mafundisho. Ni muhimu kufahamu kuwa Neno la Mungu siyo la dhehebu Fulani, na si imani ya dhehebu Fulani tu bali madhehebu yote kwa majina yake tunapaswa kufanana kiimani kutokana na kiongozi mmoja NENO LA MUNGU. Kwa nini hatufanani basin a kiongozi ni mmoj (Neno la Mungu) ? Hapo ndipo tunapata kujua kuwa tumezungukwa na walimu wengi wa uongo, na  hukumu ya walimu wa uongo itakuwa kubwa sana (YAKOBO 3:1). Hatutakiwi kuamini kila kitu bila kuyachunguza kwanza maandiko. Watu wa Beroya wao waliyachunguza maandiko kuona kama  ndivyo yalivyo wakati Paulo na Sila wakifundisha (MATENDO 17:10-11). Paulo anasema “ nifuateni mimi kama ninavyomfuata Kristo “[1 wakoritho 11:1]. Mchungaji, mwalimu, mwinjilisti, mtume na nabii, tutawafuata na kuwa pamoja nao kama watakuwa wanatufundisha kulifuata Neno la Mingu. Yeye mwenyewe anatakiwa kuwa kielelezo cha yale anayofundisha. Yesu aliyatenda kwanza ndipo akayafundisha kwa watu wengine (MATENDO 1:1). Kwahiyo mtu anayesema usiangalie niyatendayo, fuata ninachokufundisha, huyo siyo kiongozi wa biblia, ni kiongozi kipofu. Neno la Mungu linawaagiza viongozi kuwa vielelezo kwao waaminio.

Baada ya kujifunza somo hili na kulielewa, ni vema kwako sasa kuwafundisha wengine ili nao wasiendelee kumpa shetani nafasi ya kuendelea kufanya  makao kwao. Tumejifunza kuwa mapambo yanahusianishwa na miungu (mashetani). Haitakuwa  vema  kwako kuendelea kuvaa pete kinyume na maandiko tuliyojifunza.; Kama hujaelewa vizuri, nenda kaulizie maandiko yanayohalarisha uvaaji wa pete inayoitwa ya ndoa, hutapata na hata kama utapewa ni hilo (MWANZO 24:29, 47) ambalo linataja pete ya puani na bangili tena vyote vikipingana na mapenzi ya Mungu. Mungu akupe neema ya kuyatendea kazi maneno yake. Pia akupe neema ya kuwafundisha wengine somo hili;

NINYI MWAIACHA AMRI YA MUNGU, NA KUYASHIKA MAPOKEO YA WANADAMU? 

                                       ( MARKO 7:8 )

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

                                    UBARIKIWE NA BWANA YESU!!!

Advertisements

10 comments on “HAKUNA PETE YA NDOA KIBIBLIA

 1. Aisey mie napatikana hapa mtaani Umoja,jijini Nairobi,Kenya.
  Mafunzo haya ni kama maini au kihalisia naomba niseme ni maini;Hayazeeki na hayatopungua thamani kamwe! Yapo kuwepo umilele na yanafaa kwa wote wanaohitaji kuujua na kisha kuufahamu ukweli huu.
  Mwenyewe nauishi ujumbe huu tangu kuamini maanake zamu nilipewa niitumie nami naazimia kuongozwa kwa maandiko matakatifu.

  Niseme tu! ahsante kwa ukweli huu.Nakuombeeni mibaraka na hekima pamoja nayo maarifa kutoka kwa BABA MUNGU MWENYEZI.

 2. Nadhani kuna shida ya kuelewa juu ya maana ya pete. Pete inabaki kama alama ya nje tu ya upendo na uhusiano uliopo baina ya mme na mke, kama ilivyo katika maji ya ubatizo. Lakini uhusiano wao umejengwa katika roho na kweli na si katika pete. Kuna vitu vingi vinavyofanyika ambavyo ni vyema hata kama havionekani moja kwa moja kuungwa na maandiko matakatifu. Hii haimaniishi kuwa Mungu anachukia kila kitu ambacho hakijaandikwa katika Biblia. Kwa hiyo si sawa kabisa kukejeli pete kwa wana ndoa.Ikiwa Isaka alimvisha pete Rebecca puani?, basi leo wanandoa wanavishana pete vidoleni, kuna ubaya gani hapo? Ndugu kama sisi ni watu wa Mungu si vema kuanza kukejeli mambo yanayofanyika katika madhehebu mengine.

 3. kibliblia sheria inapopitishwa hapa dunian pia mbingun inakubaliwa. je huon suala la watumish weng kitumia pete kwa wanandoa kuwa n sahihi?

  • Lini walipatana juu ya kutumia pete? Hata kama wangepatana, ni kwa andiko lipi linaloruhusu utumiaji wa pete? Ndoa siyo pete! Adamu na Hawa walikuwa wanandoa bila pete na Mungu mwenyewe ndiye aliyewaunganisha na kuibariki ndoa yao. Hatuwezi kupatana kutenda uovu halafu Mungu akapendezwa na hilo. Leo kuna watu wanahalalisha ushoga, je, mapatano hayo ni sawa mbele za Mungu?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s