JE, KUCHEZA AU KUSHABIKIA MPIRA NI DHAMBI?

JE, KUCHEZA AU KUSHABIKIA MPIRA NI DHAMBI?

MECHI

   

        

            Je, wewe ni mchezaji wa mpira au ni mshabiki tu? Kama jibu ni ndiyo somo hili ni muhimu sana kwako. Hata kama wewe siyo mchezaji au mshabiki wa mpira, somo hili ni muhimu kwako kwani limejaa maarifa mengi ya kukujenga kiroho.

           Wako watu wengne ambao kwa kutokuelewa wanataka kila neno ambalo ni dhambi walione limeandikwa hivyo hivyo kama linavyotamkwa katika biblia zetu kwa mfano sigara au hii habari ya mipira ya ligi.biblia imeandikwa ili ipate kueleweka kwa vizazi vyote tangu kipindi cha uumbaji au kipindi chote hiki cha miaka elfu elfu ilyopita.mfano redio, tv, magari ndege tulizonazo leo hayakuwepo nyakati zao za nyuma.lakin neno moja tu linatolewa kuwa MAARIFA YATAONGEZEKA [DAN 12:4]. Linatoa picha kutakuwa na mambo gani yatakayotokea leo ,lazima tuelewe biblia haijaandika neno moja, kuna maneno kadha wa kadha ambayo hayajaandikwa kwa sababu hayakuwepo katika vizazi vingine vilivyotangulia, na hivyo watu wa vizazi hivyo wasingeweza kuyaelewa kwa namna tunavyoweza kuyaelewa leo. ndiyo mana MUNGU katika kuleta neno lake, alilileta ili lipate kuwa ni neno linaloweza kuvifaa vizazi vyote kwa wakat wowote.

             kwa sababu hiyo tunaweza tukawa tunataka kufahamu ni nini mapenzi ya MUNGU katika jambo fulani na tukilitafuta kama lilivyo katika biblia, tutapata shinda kuliona,mengi hatutaweza kuyaona kwa sababu hayakuwepo kama yalivyo nyakati nyingine za biblia. mfano jambo la mchezo wa mpira wa miguu au soka ambao unaendesha mamilion ya watu leo.sasa mtu atajiuliza tukiwa tumeokolewa tunaweza tukawa mashabiki wa mipira au kucheza mipira hiyo.Na mtu anaweza kujiona salama kwa kusema hakuna mahali tulipokatazwa ktk biblia.

             Hik tunachokiita mchezo wa mpira si kitu cha zamani kama wengine wanavyofikiria.ebu tuangalie historia fupi ya mchezo huu ndipo nitakueleza kwa nini mpira ni dhambi. Huko zamani kile walichokuwa wanakiita mpira hakikuwa hvyo kwa sheria tulizo nazo kwa namna ya sasa.kitu hichi kinachoitwa mpira kilianza mwaka 1863 mwezi 10,walikuwepo watu kadhaa waliotoka katika shule kadhaa uingereza na club chache zilizokuwapo hapo,wakawa wamewakilisha vikundi11 na ndio wakakusanyika mwezi 10,1863 na kuanza kutunga sheria za kupatana za mchezo

               Hawa ndio waliosababisha kiundwe chama cha mpira ambacho kinaitwa FA (FOOTBALL ASSOCIATION) cha England mwaka huu 1863 ambao ni mwaka wa karibun sana (miaka 149 iliyopita).lakini mwaka 1869 ndipo katika sheria hizo walizounda wakazidi kuziboresha kuwa katika mpira huo hautakiwi kushika mpira kwa mkono na kuubeba, itakuwa faulo.ndio wakatenganisha mchezo huu wa ragbi na football mwaka 1871 ndipo mashindano ya kwanza ya mpira yalipoanzishwa ya kombe la FA CUP.mwak 1888 ndipo mashindano ya kwanza ya ligi ya mpira yalipoanzishwa30-12-1872 ndipo mech ya kwanza ya mpira ya kimataifa ilipochezwa kati ya england na scotland. Chama cha mpira cha dunia(FIFA) kilianzishwa mwak 1904,waanzilish zilikuw nchi saba ufaransa,ubelgiji,dernmark,netheland,spain,sweeden na swizland. mwaka 1930 ndipo kwa mara kwanza kombe la dunia lilipoanzishwa.

Kwa hiyo mpira huu ni kitu cha majuzi sana kuliko wengi tunavyofahamu.kama ingeandikwa habari za mipira ya ligi, soccer miaka hiyo ya nyuma watu wasingeelewa kwa namna ambavyo sisi tunavyoelewa.

           Sasa tunajuaje je wakristo au watu tuliookoka, je tunaweza kushiriki mipira kama hii na club kam hizi.ili kuweza kujua vitu kama hivi, tunatakiwa tuangalie kanuni.MUNGU ameweka kanuni ambazo zinatuongoza kupata ufahamu mapenzi ya MUNGU kwa kila jambo.

            Pale ambapo jambo halijatajwa moja kwa moja, kanuni hizi zinaweza zikatuongoza.sasa tutakwenda kuangalia kanuni kadha wa kadha ambazo zitakuwa zinahusisha mambo mengi sana ambayo yanaweza kujitokeza katika nyakati mbalimbali katika vizazi tofauti. Sasa tunajuaje je wakristo au watu tuliookoka, je tunaweza kushiriki mipira kama hii na club kama hizi. ili kuweza kujua vitu kama hivi, tunatakiwa tuangalie kanuni. MUNGU ameweka kanuni ambazo zinatuongoza kupata ufahamu mapenzi ya MUNGU kwa kila jambo. pale ambapo jambo halijatajwa moja kwa moja, kanuni hizi zinaweza zikatuongoza. sasa tutakwenda kuangalia kanuni kadha wa kadha ambazo zitakuwa zinahusisha mambo mengi sana ambayo yanaweza kujitokeza katika nyakati mbalimbali katika vizazi tofauti.

Yako maandiko kadha wa kadha ambayo yanaweza kutuongoza katika kujua mapenzi ya MUNGU katika mipira hii.

       1) (WAKOLOSAI 3:17) “KILA MFANYALO KWA NENO AU KWA TENDO, FANYENI LOTE KWA JINA LA BWANA YESU NA KUMSHUKURU MUNGU BABANi muhimu kuelewa ndani yetu tuliokoka kuna mafuta au tuna dhamiri ambayo inatufundisha kujua mema na mabaya (1PET2:26-27).Hata kama jambo hatujajifunza kwa undani juu ya jambo fulani,ndani yetu kutakuwepo roho mtakatifu akitufundisha kuwa hapa siyo na hapa ndiyo.

Sasa kila tunalolifanya kwa neno au kwa tendo, anasema tulifanye hayo yote kwa kufungua kwa maombi.sasa kutokan na mafuta ndani yetu JE TUNAWEZA KUFUNGUA MECHI YA MPIRA KWA KUSHUKURU BABA KWA MAOMBI? Utaona ndani yetu inakataa.

        2.) (YOHANA 5:19) “MWANA HAWEZI KUTENDA NENO MWENYEWE ISIPOKUWA AMEMUONA BABA ANALITENDA”. (YOH 14:6-9) Hivyo hatuna budi kujiuliza kutokana na maisha ya YESU, JE INAWEZEKANA YESU AKAWA ANACHEZA MPIRA? YESU KASHIKA MPIRA, MARA BEKi FULANI KAMKATA MTAMA AU TIMU YA YESU IMEPIGWA MAGOLI 6-0? kama dhamiri inakataa kuwa YESU hawezi kufanya hvyo na sisi hatuwezi kufanya hvyo.Tunatenda neno ambalo YESU anaweza kulitenda.

        3) Mashabiki wengi wa jambo hilo,vinara wa jambo hilo ,JE NI MATAIFA?Kama wanaongoza ni mataifa,basi nyuma ya jambo hilo kuna mashetani (UFUNUO 18:2-3,23). Mataifa yote yanapokuwa wanachukuliwa hivyo katika jambo hilo, ndio vinara, mashabiki, kwa namna hiyo hiyo uchawi unavyotajwa lazima tujue kuna roho za mashetani.ukiona vinara au viongozi ndio waasherati au walevi,wavuta bangi.

Hawa wanaotajwa washauri wa mambo ya kifundi katika timu hizo ndio wachawi wa timu.

       4) Sitatiwa chini ya uwezo wa kitu chochote (1WAKORINTHO 6:12).Shetan anaitwa mfalme wa uwezo wa anga (EFESO 2:1-2). Chochote kile ambacho nyuma yake kuna mashetani kinamuweka mtu au watu chini ya uwezo fulani na hawezi kujikwamua pale, atakuwa anakitumikia kile kitu na hawezi kujinasua.unaweza kuona mtu anaweza kuwa na uchungu wa kuona timu yake imefungwa hata kushindwa kula lakini hana uchungu kufunga ili kuona watu wanaokoka, mtu anaweza kukaa masaa mengi kuangalia na kusiliza hizo mechi zake lakini mtu huyu huyu ni shida kuchukua masaa mengi kusoma biblia, hata kwenye ibada akiona mchungaji anahubiri muda mrefu, anatamani akatishe au anasinzia ibadani.saa nyingine anaweza kugairi kuja kwenye ibada kama ikiwa ratiba hiyo imeingiliana na mechi yake.kwa ujumla mtu halifurahii neno kama anavyoushabikia mpira.ndio mana ni rahisi kujiua kwa ajil ya mpira kuliko kwa ajili ya YESU.MTU ATAKITAMANi KUACHA INAKUWA SHIDA, UJUE AMETIWA CHINI YA UWEZO WA MPIRA NA SHETANi.

Miongoni mwa mambo ambayo shetani amefanikiwa kuchukua watu wengi ni katika mipira, hata walokole nao wanatetea kwa nguvu zote. Ndio unasikia kanisa fulani ina timu ya mpira inaitwa haleluya football club.ndio maana makanisa ya leo yameishiwa ngvu za MUNGU si kama kanisa la kwanza,watumishi wa leo wanalazimisha kuangusha watu chini na kukumbatia wake za watu kwa kigezo ndo wanaachilia upako.shame upon them.ni kwa sababu lnachanganya mambo ya kdunia na kuyaingiza kanisani.

‎            Sasa nimependa kuanza hivyo ili tupate kujua kuwa sisi tuliookolewa hatuna chetu / hatuna sehemu katika kushiriki michezo ya dunia hii. kushindana kwetu ni juu ya kuishindania imani tuliyokabidhiwa mara moja tu. watakatifu wa kanisa la kwanza walilijua vema jambo hili na kutokana na jinsi walivyokuwa wakamilifu hawakushiriki katika michezo na walichukiwa na jamii iliyowazunguka kwasababu walionekana “washamba” haya ni maelezo kuhusu watakatifu wa kanisa la kwanza” The Christians were charged with being unsocial and came to be hated and counted as enemies of societies, they were simple and modest in dress, strictly moral in their conduct and would not go to the games and feast “maneno haya yanapatikana katika biblia iitwayo THOMPSON CHAIN REFERENCE BIBLE(NIV)” ambayo mwisho kwenye kurasa za mwisho inatoa dondoo(notes) ya baadhi ya matukio ya kanisa la kwanza na kabla yake. sasa ikwa sisi tutanana nao wanaoshabikia mipira na michezo mingineyo tofauti yetu na wao ni ipi? tujifunze kwa ndugu zetu walio tutangulia, tuige imani yao maana ikiwa tufanana na watu wa ulimwengu na sisi tukaanza kuenenda kama ulimwengu unavyoenenda tukaishi kana kwamba sisi ni wenyeji hapa duniani basi tunaitwa wazinzi kwa kuwa tutakuwa na mabwana wawili mungu wa dunia hii, shetani (2WAKORINTHO 4:3-4) na MUNGU muumba wa mbingu na nchi; (YAKOBO 4:4) Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu” BAADHI YA MASOMO YAPO CHINI BOFYA SOMO UINGIE UJIFUNZE;

SOMO; “KANISA LA FILEDELFIA” SOMOAMIUJIZA YA WATU KUANGUKA CHINI”   SOMO AMANI YA KRISTO IAMUE MIOYONI MWENU SOMO” MAVAZI YA KIKAHABA”  ZACHARY KAKOBE  “BISHOP ZACHARY KAKOBE INTERNATIONAL MINISTRIES”

OMBI LANGU KWAKO.

           Share ujumbe huu na  marafiki zako wa “facebook” na “twitter” kwa kubonyeza kitufe chenye neno “share” hapa chini ya maneno haya. Ukifanya hivyo, utakuwa mmoja kati ya maelfu ya watu wengine watakaopokea baraka za Mungu kwa kusambaza somo hili kwa maelfu ya watu katika mitandao mbalimbali ya internet.

MUNGU AKUBARIKI SANA!!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s