JINSI ISIVYOWEZEKANA MTU KUOKOKA BILA MAOMBI

ZACHARY KAKOBE

Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SOMO: JINSI ISIVYOWEZEKANA MTU KUOKOKA BILA MAOMBI

Jumapili 20. 2. 2000 itakuwa ni siku ya uzinduzi wa Operesheni Maliza Kazi (YOHANA 4:34; 17:4 ). Siku ya kunyakuliwa kwa Kanisa inazidi kukaribia. Bado kitambo kidogo sana, Yesu ajaye, anakuja wala hatakawia, (WAEBRANIA 10:37), hivyo huu ni wakati wa kumaliza kazi tuliyopewa ya kuwaleta watu kwa Yesu; kwa kishindo zaidi kuliko tulivyoanza. Siku hiyo ya jumapili 20.2. 2000, tunatazamia kuwaona watu wageni maelfu-elfu ambao hawawezi  kutosha katika mfumo wa ibada wa sasa, na hivyo kuanzia siku hiyo tutaongeza ibada nyingine. Sasa basi, ni makusudi ya somo letu la leo, kujifunza yatupasayo kufahamu ili tupate kuona maelfu-elfu wakija na kuokoka siku hiyo. Tunajifunza somo hili kwa kulitafakari katika vipengele vinne vifuatavyo:-

( 1 ). JINSI MTU ASIYEOKOKA ALIVYO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO

( 2 ). JINSI ISIVYOWEZEKANA MTU KUOKOKA BILA MAOMBI

( 3 ). JINSI YA KUFANYA MAOMBI KIVITENDO

( 4 ). MAMBO YA KUZINGATIA

( 1 ). JINSI MTU ASIYEOKOKA ALIVYO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO

Watu wote tuliokolewa, tuko katika ufalme wa Mungu. Bwana Yesu ndiye Mtawala wetu. Upande wa pili, kwa jinsi hiyohiyo, watu wote ambao hawajaokoka, wako katika ufalme wa Ibilisi. Shetani ndiye mtawala wao.katika ufalme wa Shetani, watu hawa ni watumwa wa Ibilisi, ni mali yake Ibilisi, ni watoto wa Ibilisi ( 1 YOHANA 3:8-10; YOHANA 8:34 ). Watu hawa walioko katika ufalme wa Shetani, pia ni wafungwa katika gereza la Shetani, na Shetani hataki kuwaachia. Ni mpaka apatikane mwenye nguvu zaidi, wa kuwafungua ( LUKA 4:18 ) Wafungwa hawa wanalindwa vikali na Shetani ili kuhakikisha hawatoki katika nyumba yake, na anawaita VITU  VYAKE, na mateka wake ( LUKA 11:21-22 ).Siyo hilo tu. Akili zao zimetiwa giza, wamepofushwa fikra zao na kujazwa kila namna ya ujinga ili isiwazukie nuru ya Injili ya wokovu ( WAEFESO 4:17-19;2WAKORINTHO 4:3-4 ).Wamedanganywa na Ibilisi baba wa uongo. Kwa kila namna ya uongo, na kufanya wachukie kweli ya wokovu, na kuona kwamba hakuna kuokoka duniani, dini zao zinatosha  n.k. ( UFUNUO 12:9; YOHANA 8:43-45 ). Kujaribu kuwaarika watu wa jinsi hii kuja kusikia Injili au kujaribu kuwashuhudia katika hali hii, ni kupoteza muda wetu. Kwanza kabisa Shetani hawezi kuwaachia watoke katika ufalme wake na pia kwa jinsi walivyodanganywa na kupofushwa fikra zao. Hakuna lolote la wokovu linaloweza kueleweka kwao.

( 2 ). JINSI ISIVYOWEZEKANA MTU KUOKOKA BILA MAOMBI

Kama tulivyotangulia kuona, Shetani hawezi kutuachia tuvichukue VITU VYAKE kiulaini, na kuviweka katika ufalme wa Mungu ni mpaka tupambane naye, tupigane naye vita na kumshinda, kisha kumnyang’anya mateka wake bila yeye kupenda kwa sababu tu amezidiwa nguvu. Kwa namna ile ile ambayo Farao hakuweza kuwaachia Waisraeli kiulaini, mpaka pale aliposhindwa. Vivyo hivyo hawezi kuviachia “vitu vyake” mpaka tupambane naye kwanza na kumshinda, na kumlazimisha kumuachia. Vita hii inaitwa VITA YA KIROHO (spiritual warfare)=       ( WAEFESO 6:11-12; 2WAKORINTHO 10:3-4 ).Siraha kubwa ya kivita tunayopaswa kutumia ni MAOMBI. Katika WAEFESO 6:11-20, tunaona siraha zote za vita hizi zikitajwa. Hapa tunaona siraha saba zinazotumika katika vita vya kiroho, zikitajwa. Hata hivyo, siraha ya mwisho, siraha ya saba , maombi, inapewa uzito mkubwa kuliko zote zilizotangulia. Siraha sita za mwanzo zinatajwa zote katika mistari mine ( MST 14-17 ), lakini mistari yote mitatu (MST 18-20 ), inazungumzia  silaha moja ya maombi, kuonyesha uzito wake ikilinganishwa na zile nyingine. Maombi, ndiyo ufunguo wa kumshinda Shetani na kumnyanganya vitu vyake. Kwa maombi, kwa jina la Yesu, tunamfunga Shetani na majeshi yake, na kuhakikisha hawafurukuti na kumnyang’anya silaha zake anazozitegemea, kisha tunawachukua mateka wake na kuwaongoza katika ufalme wa Mungu ( MATHAYO 16:18-19; LUKA 11:21-22 ). Tunapokwenda kumshuhudia mtu juu ya wokovu au kumwalika aje kusikia Injili, bila kwanza kumtoa kifungoni, baada ya kumzidi nguvu Mfalme wake Ibilisi, kufanya hivyo ni kazi bure. Ni vigumu sana kupata matokeo yanayotarajiwa. Kwa ufupi, kabla ya kufanya maombi tusijaribu kwenda kushuhudia  au kuwaalika watu kusikia Injili. Matokeo yake yatakuwa hafifu. Hata kama wataisikia Injili, wataisikia wakiwa katika hali ya uzezeta, na hawawezi kuokoka.

( 3 ). JINSI YA KUFANYA MAOMBI KIVITENDO

  1. 1.      Sehemu kubwa ya maombi yetu, iwe ni maombi ya vita dhidi ya Shetani. Kuharibu ufalme wa Shetani juu ya mtu anayehusika, kukatilia mbali vifungo vyake juu ya mtu husika, kama vifungo vya kidini n.k, kusambaratisha uongo wake, ujinga wake, ganzi na kila namna ya upofu wa fikra au uzezeta  aliouweka Shetani ndani ya mtu huyo. Kuharibu kila kamba za utumwa wa dhambi, iwe ni ulevi, uasherati, uzinzi na kila aina ya dhambi hizo. Kuamuru mtu huyo husika kutoka katika gereza la Ibilisi na kuwekwa huru kwa jina la Yesu Kristo ( YOHANA 8:36 )Maombi haya ya mapambano au vita yachukue theluthi mbili ya muda wetu wa jumla wa maombi. Kama muda wetu wa maombi ni saa moja basi  muda wa maombi ya vita uwe dakika 40. Kama muda wetu wa jumla wa maombi ni saa tatu basi saa mbili  iwe ni maombi ya kupambana na Ibilisi.
  2. 2.      Theluthi moja ya muda uliosalia wa maombi, tumwombe Mungu sasa amvute mtu huyo aliyewekwa huru kutoka katika ufalme wa Shetani na kumwingiza katika ufalme wa Mungu. Abadilishe maisha yake kwa Neno na kumfanya akue katika neno lake bila kurejezwa tena katika dhambi ( YOHANA 8:44; 10;28-29; 1PETRO 1:23 ).Kama muda wote wa maombi ni saa moja, dakika 20 zitumike kwa maombi hayo. Kama muda wote wa maombi ni saa tatu, saa moja itumike kwa maombi haya. Wakati wote maombi haya yatanguliwe na maombi ya mapambano.
  3. 3.      Kutajwa kwa majina ya watu tunaotaka wawekwe huru na waokolewe ni muhimu sana. Maombi specific au maalum kwa mtu maalum, yanakuwa na nguvu ya ziada. Yeyote atakayeuambia mlima huu ng’oka ( MARKO 11:23 ). Akauambia mti (mtini) mtu asile matunda kwako ( MARKO 11:12-14, 20-21). Hauna budi kumwombea mtu maalum kwa kutaja jina lake maalum ili baadaye tujue matokeo ya maombi yetu, kwa jinsi ile ile ambavyo wanafunzi wa Yesu walivyoufuatilia ule mtini uliolaaniwa na kujua matokeo ya maombi yale. “Simon, Simon………nimekuombea wewe” ( LUKA 22:31-32 ). Katika wanafunzi kumi na wawili, Yesu alichagua mmoja maalum wa kumwombea kwa jina, ili kuongeza nguvu ya maombi. “Lazaro, njoohuku nje” ( YOHANA 11:43 ), ni fundisho jingine kwetu. Tutaje majina ya wale tunaotaka watoke nje ya gereza la Shetani.

( 4 ). MAMBO YA KUZINGATIA.

Imani ni silaha mojawapo pia ya vita vyetu. Tusiangalie ugumu wa wale ambao hawajaokoka. Tusiangalie nguvu na uwezo wa Shetani, basi tuangalie nguvu na uwezo wa Yesu aliyemwokoa Sauli na kumfanya Mtume Paulo. Shetani anaitwa “Mtu mwenye nguvu” bali Yesu anaitwa “Mtu mwenye nguvu kuliko yeye” ( LUKA 11:21-22 ). Vile vile tuwaombee wale tunaofahamu wanakokaa ili mwishoni mwa maombi  haya tuwaalike kuja siku ya jumapili tarehe 20.2.2000. Kwa sasa tusiwaalike kamwe. Maombi kwanza, kualika baaadaye.

  Kama wewe ni mtendakazi shambani mwa Bwana, naamini umeberikiwa sana kwa somo hili zuri kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe. Muombe Mungu akusaidie ili usiwe msikiaji wa Neno tu bila kulitendea kazi ( YAKOBO 1:22 )

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook,Twitter n.k,  kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

                                                         UBARIKIWE NA BWANA YESU!!!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s