KIFO CHA YOHANA MBATIZAJI

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

Kuchambua Biblia.

SOMO:       KIFO CHA YOHANA MBATIZAJI

(MATHAYO 14:1-14)

Kuna mambo mengi ya kujifunza katika mistari 14 ya kwanza ya Sura ya 14 ya kitabu cha MATHAYO.  Tutayagawa mafundisho tunayoyapata katika mistari hii, katika vipengele vinane:-

  1. UMUHIMU WA KUMFAHAMU YESU NI NANI (Mst. 1-2);
  2. WAJIBU WA KUISEMA KWELI (Mst. 3-4);
  3. KUUDHIWA KWA AJILI YA KWELI (Mst. 3-5);
  4. KUWAPENDEZA WANADAMU NA SHETANI (Mst. 6-7);
  5. TAHADHARI YA KUPOKEA MASHAURI YA WAZAZI (Mst. 8);
  6. KUFA KWA AJILI YA KWELI (Mst. 9-11);
  7. USHIRIKIANO WA WAKRISTO KATIKA MAZISHI (Mst. 12);
  8. SIRI YA HUDUMA YENYE UWEZO (Mst. 13-14).

(1)      UMUHIMU WA KUMFAHAMU YESU NI NANI (MST. 1-2; MATHAYO 16:13-16)

Ni muhimu sana kumfahamu Yesu ni nani.  Majibu yetu ya maombi au uwezo wetu wa kupokea kutoka kwa Mungu, kunategemeana sana na ufahamu tulio nao kuhusu Yesu ni nani.  Je, Yesu ni nani kwetu?  Jibu sahihi la swali hili, ndilo ufunguo wa kupokea lolote kutoka kwa Mungu.  Je tunamfahamu Yesu kama mmojawapo wa manabii, kama Eliya, Yeremia au Yohana Mbatizaji?  Tunamfahamu Yesu kama mtu mwenye kipimo cha uwezo kama Eliya?  Tunamfahamu Yesu kama mwana tu wa Yusufu? (YOHANA 6:41-42).

Yesu Kristo ni:-

a)     MKUU KULIKO HEKALU (MATHAYO 12:6);

b)     MKUU KULIKO YONA (MATHAYO 12:41);

c)      MKUU KULIKO SULEMANI (MATHAYO 12:42);

d)     MKUU KUPITA MALAIKA, MUUMBAJI (WAEBRANIA 1:1-4,6);

e)     MWANA WA MUNGU ALIYE HAI (MATHAYO 16:6).

Yesu, Mwana wa Mungu, maana yake kwamba Yesu ni sawa na Mungu Baba.  Yeye ni Mungu (YOHANA 10:30-36).

(2)      WAJIBU WA KUISEMA KWELI (MST. 3-4; 2 WAKORINTHO 13:8)

Wajibu wa kila mtu aliyeokoka ni kuwa shahidi wa Mungu wa kweli.  Sisi ni mashahidi wa Mungu (ISAYA 43:10).  Tunajionyesha kwamba ni mashahidi wa Mungu kwa jinsi ambavyo tunaishuhudia kweli wakati wote (YOHANA 18:37).  Kweli ni nini? (YOHANA 18:38).  NENO LA Mungu ndiyo kweli (YOHANA 17:17).  Yesu Kristo aliifundisha kweli bila kujali cheo cha mtu (LUKA 20:21).  Mtume Paulo pia aliifundisha kweli bila kujali cheo cha mtu (WAGALATIA 2:5-6).  Hatuwezi kudai kwamba tunamtumikia Mungu ikiwa kweli tunaionea aibu, na tunachagua watu wa kuwaambia kweli.

(3)      KUUDHIWA KWA AJILI YA KWELI (MST. 3-5)

Kila mtu anayeisema kweli na kuishindania kweli, lazima ataudhiwa na kuwa na maadui wengi.  Mtume Paulo alikuwa na maadui wengi kwa sababu alisema kweli na kuishindania (WAGALATIA 4:16).  Wengi sana walimpinga Paulo, hawakusimama upande wake (2 TIMOTHEO 4:14-16).  Yeremia alipoisema kweli, walimkamata ili wapate kumwua kama Yohana Mbatizaji.  Yeremia alikamatwa na viongozi wa dini.  Watu wa dini hawaipendi kweli (YEREMIA 26:7-9).  Hatupaswi kuogopa maudhi na mateso na kuacha kuisema kweli.  Watakatifu wote, lazima waudhiwe kwa ajili ya kweli (2 TIMOTHEO 3:12).

(4)      KUWAPENDEZA WANADAMU NA SHETANI   (MST. 6-7)

Katika jambo lolote tunalolifanya katika wokovu ni lazima tujiulize kwamba tunafanya jambo hilo kwa lengo la kuwapendeza wanadamu na Shetani au Mungu?  Ni Mungu au wanadamu (WAGALATIA 1:10).  Ikiwa tunafanya jambo ili kutafuta kuwapendeza wanadamu basi hatuwi tena watumwa wa Kristo, bali wa Shetani.  Wakati wote, katika mambo yote tulenge kumpendeza Mungu tu (ZABURI 73:25).  Ikiwa kutokana na sisi kumpendeza Mungu, wanadamu nao watapendezwa basi vema, lakini ikiwa watachukizwa, hatuna jinsi nyingine ya kufanya.  Wanadamu na Shetani wanaweza kutuahidi zawadi kubwa hata kwa viapo tukiwapendeza, lakini hatimaye; hayo yatatufanya twende Jehanum milele.  Tujifunze kwa Yesu jinsi alivyopuuza ahadi za zawadi za Shetani na hakufanya yanayompendeza Shetani.  Tukifanya hivyo, malaika watatutumikia (MATHAYO 4:8-11).

(5)      TAHADHARI YA KUPOKEA MASHAURI YA WAZAZI   (MST. 8; MARKO 6:22-24)

Biblia inatueleza kwamba tuwaheshimu na kuwatii wazazi.  Hata hivyo, hatupaswi kukubali mashauri yao pale ambapo mashauri hayo yanakwenda kinyume na Neno la Mungu.  Kufanya hivyo ni kuwafanya wawe zaidi ya Baba yetu aliye mbinguni.  Utii wetu kwa wazazi lazima uwe katika Bwana na tena kwa yale yaliyo mema tu (WAEFESO 6:1-2; TITO 3:1).  Binti Herodia aliponzwa na ushauri wa mama yake.  Ni wajibu wa kila mzazi kutoa ushauri ulio sawa na maonyo ya Bwana wetu Yesu Kristo (WAEFESO 6:4).  Hatupaswi kuzifuata amri za wazazi wetu ambazo zitatutia unajisi (EZEKIELI 20:1-8).

(6)      KUFA KWA AJILI YA KWELI   (MST. 9-11)

Yohana Mbatizaji anakuwa miongoni mwa mashahidi wengi ambao hawakukubali ukombozi wowote ule, bali wakawa tayari kufa kwa ajili ya kweli (YEREMIA 26:23; MATHAYO 23:37; MATENDO 7:59; MATENDO 12:1-2; WAEBRANIA 11:35-38).  Tunapaswa kuwa waaminifu hata kufa kwa ajili ya kweli, ikiwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi wengi namna hii (UFUNUO 2:10; WAEBRANIA 12:1-2).  Tunapaswa kuidharau aibu ya kupigwa na mume, kufukuzwa kazi, kulazwa nje ya nyumba, kutukanwa na lolote lile linalotupata kwa ajili ya kweli.

(7)      USHIRIKIANO WA WAKRISTO KATIKA MAZISHI   (MST. 12)

Wanafunzi wote walishiriki katika mazishi ya mwanafunzi mwenzao Yohana Mbatizaji.  Hapa tunajifunza waziwazi kwamba kila mmoja wetu, ni lazima awe na ushirikiano na wenzie katika masuala ya mazishi ya wenzetu katika Bwana, na hata ndugu zao.  Kila tunapotangaziwa juu ya misiba iliyotokea katika Makanisa yetu ya Nyumbani au Zoni zetu kila mwanafunzi wa Yesu anapaswa kutoa muda wake, nguvu zake, mali zake na lolote lile akilipa jambo hilo uzito unaostahili.  Katika LUKA 9:60, Yesu alimwambia mtu yule awaache watu wawazike wafu wao, kwa sababu alikuwa mwongo.  Kama kweli Baba yake angekuwa amekufa, asingekuwa anamfuata Yesu wakati huo na kungoja ruhusa ya Yesu kwenda kumzika Baba.  Hatupaswi kutumia msitari huu kwa kutokujua kweli na kuuacha upendo wa Kikristo.

(8)      SIRI YA HUDUMA YENYE UWEZO  (MST. 13-14)

Siri ya huduma yenye uwezo wa Yesu Kristo, ilikuwa ni kujitenga na watu na kwenda mahali pasipo watu na kuomba faraghani (MST. 13; LUKA 9:18).  Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kufanya hivyo (MARKO 8:31-32).  Hatupaswi kuchukuliwa na Utumishi wa Kristo kiasi ya kusahau kujitenga na watu na kwenda faraghani.  Namna hiyo, tutakuwa tunazungumza bila amri wala uwezo, na maneno yetu yatakuwa hayana nguvu ya kubadilisha.  Mamlaka yetu pia itakuwa hafifu, licha ya miili yetu kuchoka na kuchakaa upesi.

HERI, WEWE UKIWA SHAHIDI WA KWELI KAMA YOHANA MBATIZAJI.

 Usikose faida zilizomo katika Biblia, jifunze somo hili “https://davidcarol719.wordpress.com/ndugu-zake-yesu/

…………………………………………………………………………………………………………………………………..

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe..

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s