KUANDAMANA NA MKUTANO KUTENDA UOVU

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SOMO LA 4 :  KUANDAMANA NA MKUTANO KUTENDA UOVU

 

NENO LA MSINGI:

KUTOKA 23:2

“USIANDAMANE NA MKUTANO KUTENDA UOVU; wala usitie ushahidi wako katika neno lolote kwa kugeukia kando na KUANDAMANA NA MKUTANO ili kupotoa hukumu.”

<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><>< 

N

eno “mkutano” au “makutano” linapotumika katika Biblia, maana yake “watu wengi” [ANGALIA MARKO3:7-9, 20, 32; MARKO 4:1]  Njia ya kwenda mbinguni ni nyembamba, na wapitao katika njia hiyo ni WACHACHE maana hata kuiona tu ni neema ya ajabu!  Biblia inasema wazi, kwamba njia ya kwenda upotevuni ni pana, na waendao katika njia hiyo ni watu wengi [SOMA MATHAYO 7:13-14].  Sisi tunaokwenda mbinguni ni wachache mno, na tumezungukwa na watu wengi au MKUTANO, kila upande.  Hapa ndipo inapotupasa kuwa waangalifu!  Mambo ya watu wengi huwa yana mvuto mkubwa, na ni mepesi sana kukubalika kwetu; na tukajaribiwa KUGEUKIA KANDO na kuyafuata.  Tukumbuke kila mara kwamba, sisi sio wenyeji wa nchi hii, wenyeji uko mbinguni [SOMA WAEFESO 2:19].  Sasa basi hapa duniani tunapokaa katika miji na vijiji, tunapokuwa majumbani au katika maofisi na viwanda; au popote, tujue kwamba tumezungukwa na mkutano au watu wengi ambao ni wenyeji wa nchi hii.  Wenyeji wa nchi hii ni watu ambao maisha yao hayafuatani na Neno la Mungu.  Wanaweza wakajiita wakristo kumbe wanajidanganya nafsi zao, maana mkristo ni yule anayeenenda VILEVILE kama Kristo alivyoenenda alipokuwa duniani, na kuzishika amri zake katika kuwaza, kusema na kutenda [SOMA 1 YOHANA 2:3-6].  Mungu katika hekima yake kubwa, anatuagiza kwamba tusifanye kamwe agano na wenyeji hawa wa nchi hii, walio mkutano mkubwa; maana agano hilo litakuwa ni mtego kwetu [SOMA KUTOKA 34:12].  “Kufanya agano” maana yake kukubaliana na kupatana katika kutenda jambo fulani.  Kufanya agano na wenyeji wa nchi hii, maana yake kuwafuata watu wengi waliotuzunguka na kukubaliana, na kupatana nao; katika mavazi, usemi, jinsi ya kufanya biashara, jinsi ya kuoa au kuolewa na jinsi yote ya maisha ya kila siku.  Kufanya agano na mkutano, ni kuufuata mkutano katika kutenda mambo yanayokubalika kwa watu wengi, ingawa yako kinyume na Neno la Mungu. Huu ni mtego mkubwa ambao utamnasa mtu aliyeokoka na kumfanya ashindwe kuendelea kwenda katika njia nyembamba.  Hatupaswi kuwafuata watu wengi au mkutano katika namna yao ya kuvaa, huu ni mtego.  Hatupaswi kuufuata mkutano katika namna yao ya starehe.  Muziki wa dansi redioni au kwa kaseti, ni furaha ya wenyeji wa nchi hii.  Hatupaswi kuandamana na mkutano na sisi tukafungulia redio zetu na kuyaruhusu masikio yetu kusikia vipindi vya “Mchana Mwema”, “Jioni Njema”, “Kijaluba”, “Michezo”, “Mchezo wa Kuigiza wa Chibuku ni pombe bora”, n.k.  Huu ni mtego, kufanya hivyo ni kuandamana na mkutano kutenda uovu.  Michezo ya Karata, darts, bao, “snakes & ladder”, draft n.k.  haya yote ni starehe za wenyeji wa nchi hii.  Hatupaswi kufanya agano nao katika mambo haya.  Kufanya hivyo ni kunaswa katika mtego.  Hatupaswi kuandamana na wanawake wenyeji wa nchi hii, katika mazungumzo yao ya kimataifa wanapokuwa wakiosha vyombo, kusukana au katika mabaraza ya kusengenyana.  Huu ni mtego.  Hatupaswi kuandamana na wenyeji wa nchi hii katika ubishi wa mpira na kwamba nani atashinda ligi ya mwaka huu.  Hizi ni starehe za wenyeji wa nchi hii, na ni mtego kwetu [MITHALI 1:15-16].  Wenyeji wanaotuzunguka, wanatumia hirizi, na watatushawishi kuwafunga hirizi watoto wetu.  Hatupaswi kuandamana na mashauri yao.  Tunapougua, watatushawishi kuwaona waganga wa kienyeji wanaotumia bao na ramli, hatupaswi kuandamana na mkutano kutenda uovu [SOMA MITHALI 1:10].  Tunatofautiana mno na wenyeji wa nchi hii katika namna zao za kufanya harusi, kufanya matanga au shughuli za misiba.  Ni lazima kujihadhari na njia zao za kufanya mambo haya ili tusiwe mtegoni.  Hatupaswi kushiriki sherehe za “Kipaimara”, au “Ubatizo wa watoto wadogo”, kwa kuwa hizi ni sherehe za wenyeji wa nchi hii, na hazifuatani na Neno la Mungu [SOMA ZABURI 50: 17-18].  Miongoni mwa wenyeji wa nchi hii, ambao ni watu wengi, wapo wengine wanaojiita wameokoka na wanasema “Bwana Asifiwe”, lakini wanafanya mambo yasiyolingana na Neno la Mungu [SOMA LUKA 6:46; MATHAYO 7:21-23].  Baadhi ya watu wanaosema “Bwana Asifiwe”, hufanya mambo yaliyo kinyume na Neno la Mungu na wakisema jinsi Neno linavyoyakataza, wao wanasema “Dhehebu letu halitukatazi”.  Tukumbuke kwamba dhehebu siyo Njia na Kweli  na Uzima.  Tuliona katika masomo ya wiki zilizopita katika Kanisa la Nyumbani kwamba Yesu ambaye ni Neno la Mungu, Yeye ndiye Njia.  Watu wanaotushawishi kutenda mambo yaliyo kinyume na Neno la Mungu na kutuvuta katika “madhehebu yao yanayoruhusu mambo hayo”, hatupaswi kufanya agano nao na kufuata ushauri wao.  Wengine wanaosema “Bwana Asifiwe”, wanaondoa mpaka uliowekwa katika Neno la Mungu na kusema kwamba miaka hii, wokovu lazima uende kwa njia ya kisasa ya karne ya 20!  Hawa wote, ni wenyeji wa nchi hii.  Hatupaswi kuandamana na ushauri wao ingawa wanajiita wameokoka.  Kufanya hivyo ni kugeukia kando na kuandamana na mkutano.  Biblia inatuonya kwamba tusiondoe alama ya mpaka wa zamani uliowekwa na baba zetu katika Biblia, kwa kusingizia nyakati za kisasa.  Kufanya hivyo ni kutafuta ghadhabu ya Mungu [SOMA MITHALI 22:28; AYUBU 24:1-2; HOSEA 5:10].  Tukitaka kuendelea katika njia nyembamba iendayo uzimani ambayo ndiyo Njia Kuu ya Mungu, Biblia inatuagiza kuuliza MAPITO YA ZAMANI na tunaelekezwa kuyafuata hayo, na siyo mapito ya kisasa.  Biblia inasema tusipotaka kuyafuata mapito ya zamani, hatutajipatia raha nafsini mwetu [SOMA YEREMIA 6:16].

 

Tunayo furaha kubwa mno tunapowaona watu waliookoka ambao wako katika madhehebu mengine, maana wasio kinyume chetu, wako upande wetu [SOMA MARKO 9:38-40].  Hivyo tunapaswa kuwapenda na kushirikiana nao kama watoto wa Baba mmoja [YOHANA 1:12].  Hata hivyo, uhusiano wetu na wao, lazima ubaki katika alama za mpaka wa Neno la Mungu na mapito ya zamani ya Kanisa la Kwanza.

M J A D A L A:

Kwa mjadala, kila mmoja katika Kanisa la Nyumbani, aeleze jinsi ambavyo mkutano au watu wengi wanaotuzunguka wanavyoweza kutushawishi kuwaandama, na kutenda  uovu.  Taja maeneo ambayo hayakuguswa hapa.

 

M  A  S  W  A  L  I

(1)       Wenyeji wa nchi hii ni watu gani?

—————————————————————————————————————-

(2)       Watu waliookoka ni wenyeji wa wapi?  Hapa tunafanya nini? [WAEFESO 2:19].

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

(3)       Kufanya Agano na wenyeji wa nchi hii, kutatuletea nini? [KUTOKA 34:12].

—————————————————————————————————————-

(4)       Kufanya agano na wenyeji wa nchi hii ni kufanya nini?

—————————————————————————————————————-

(5)       Je, kuna wokovu wa karne ya 20 au Wokovu wa Kisasa?  Kama jibu lako SIYO, kwa kutumia maandiko, eleza na kufafanua jibu lako na eleza hasara ya kuleta maisha ya wokovu yanayolingana na nyakati hizi za kisasa.

—————————————————————————————————————-

Usikose faida zilizomo katika somo lililotangulia “KUHURUMIANA NA KUPENDANA KAMA NDUGU”, ingia hapa ujifunze Neno la Mungu https://davidcarol719.wordpress.com/wp-admin/post.php?post=310&action=edit

<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><>< 

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

                                                         UBARIKIWE NA BWANA YESU!!!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s