KUGEUKA SURA MLIMANI

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe

Tovuti : http://www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : http://www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube : http://www.youtube.com/user/bishopkakobe
SIKU YA KUICHAMBUA BIBLIA

SOMO:        KUGEUKA SURA MLIMANI

(MATHAYO 17:1-13)
Katika MATHAYO 16:28; Yesu alisema kwamba, miongoni mwa wanafunzi wake hawataonja mauti kabisa hata watakapomwona Yesu akija katika ufalme wake. Maneno haya yanatimia katika MATHAYO 17, ambapo Petro, Yakobo na Yohana wanapochukuliwa juu ya mlima mrefu faraghani na hapo Yesu anageuka sura yake mbele yao na kuwa katika ufalme wake. Kuna mengi ya kujifunza katika MATHAYO 17:1-13. Tutajifunza somo letu la leo katika mistari hii, kwa kuligawa katika vipengele vitano:-

(1) KUTWALIWA KWA PETRO, NA YAKOBO NA YOHANA (Mst. 1);
(2) KUUONA UTUKUFU WA MUNGU MLIMANI (Mst. 1-2);
(3) SABABU ZA KUTOKEWA NA MUSA NA ELIYA (Mst. 3-8);
(4) SIRI KATIKA HUDUMA (Mst. 9);
(5) ELIYA AJAYE KABLA YA SIKU YA BWANA (Mst. 10-13).

(1) KUTWALIWA KWA PETRO, NA YAKOBO NA YOHANA (Mst. 1)
         Katika kuichambua Biblia katika Injili ya Mathayo, Marko, Luka na Yohana , tunaona mara kwa mara Yesu akiwatenga Petro, Yakobo na Yohana na kuwashughulikia tofauti na wanafunzi wengine (MATHAYO 26:36-38; MARKO 5:35-37). Kwa kufanya hivi, Yesu alikuwa anawatayarisha ili wawe na huduma kubwa zaidi. Katika WAGALATIA 2:9, wanaitwa “wenye sifa kuwa ni NGUZO“. Tukiona Mungu anatutenga kwa kupitia kwa Watumishi wake na kushughulikiwa tofauti na wanafunzi wengine, tujue kwamba tunatayarishwa tofauti kwa ajili ya huduma iliyo kubwa zaidi. Hatupaswi kunung’unika moyoni na kuona kwamba mbona wengine hawashughulikiwa namna hiyo hiyo. Tukizidi kutii na kutamani kutengwa na kuwa tayari kukabiliana na gharama zote, huduma zetu zitakuwa maalum kuliko wengine.

(2) KUUONA UTUKUFU WA MUNGU MLIMANI (Mst. 1-2)
          Hatuwezi kuuona utukufu wa Mungu mahali tambarare, nyikani, bondeni au penye watu wote. Ni lazima tukubali kupanda MLIMA MREFU. Kupanda mlima mrefu ni kazi ngumu mno na isiyokubalika mwilini, lakini hiyo ndiyo siri ya kuuona utukufu wa Mungu. Kuomba, kufunga, kufuatilia na kufundisha watoto wachanga kiroho, kulisoma Neno la Mungu n.k; ni kama kupanda mlima mrefu, ni kazi ngumu, hata hivyo, ndiyo njia pekee ya kuuona utukufu wa Mungu. Musa aliambiwa apande Mlima Sinai ili akachukue sheria ya Mungu (KUTOKA 24:12). Eliya pia ilimbidi apande mlima Horebu ili aisikie sauti ndogo ya utulivu ya Mungu, baada ya safari kubwa mno ya siku 40; mchana na usiku (1 WAFALME 19:7-8, 11-13). Hatuwezi kupata mafunuo makubwa katika Neno la Mungu na kuona nguvu ya Mungu ikitenda kazi pamoja nasi, ikiwa hatuko tayari kupanda mlima mrefu kwa kukwepa gharama.

(3) SABABU ZA KUTOKEWA NA MUSA NA ELIYA (Mst. 3-8)
          Katika MST. 3-8 tunaona Petro, Yakobo na Yohana wakitokewa na Musa na Eliya. Kulikuwa na sababu kadha za kutokewa na Musa na Eliya, ndipo waisikie sauti ya Mungu:
1. Mungu aliwaambia wamsikie Yesu na siyo Musa, kuthibitisha mwisho wa sheria ya Musa na kuanza kwa sheria ya Kristo (LUKA 16:16; WAGALATIA 3:23-25; YOHANA 1:17; WAGALATIA 6:2);
2. Mahali hapa, Mungu alituthibitishia juu ya maisha baada ya kufa. Musa alikuwa amekufa yapata miaka 1,700 na Eliya alikuwa ametoweka yapata miaka 1,000, lakini hapa wanaonekana wakiwa hai. Ni hakika kuna maisha baada ya kufa (LUKA 16:19-31; UFUNUO 6:9-11; WAFILIPI 1:21-23);
3. Tunathibitishiwa kuja kwa Yesu Kristo katika utukufu wake na kutoa malipo kwa wenye haki na wasio na haki (MATHAYO 16:27; 25: 31-34);
4. Tunajifunza kwamba mwili unakufa na kuoza kaburini, lakini NAFSI YA MTU HAIFI bali inaishi milele (ZABURI 16:10; LUKA 20:37-38);
5. Petro hakutamani kurudi tambarare tena. Kukaa na Yesu katika utukufu wake mbinguni ni jambo la kupendeza mno. Heri ashindaye na kuketi pamoja na Yesu katika utukufu wake (UFUNUO 3:21).

(4) SIRI KATIKA HUDUMA (MST. 9)
         Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo (MITHALI 25:2). Yako mambo mengi katika huduma zetu na maisha yetu ya Ukristo ambayo Mungu hapendi tuyaseme kwa wengine. Ni siri. Ikiwa tunahitaji Mungu atutumie sana, ni lazima tujifunze kuficha siri za wale wanaotaka ushauri kwetu au maombezi na tena lolote tunaloambiwa na Mtumishi wa Mungu kwamba ni siri linapaswa kutunzwa hivyohivyo. Tena haifai yote tunayoyaona katika maono na ndoto kuyatangaza kwa wengine, hasa yale yanayohusiana na matukio ya watu tunaowajua. Ni muhimu sana pia kuomba hekima ya kujua ni lipi linafaa kutajwa kwa wakati fulani. Mambo mengine ni siri mpaka wakati wake mzuri wa kuyataja (MATHAYO 16:20; MITHALI 25:11).

(5) ELIYA AJAYE KABLA YA SIKU YA BWANA (MST. 10-13)
         Katika MALAKI 4:5-6; TUNAONA UTABIRI WA KUJA KWA Eliya kabla haijaja siku ile ya BWANA. Eliya huyu siyo WILLIAM BRANHAM kama wengine wanavyodai, bali ni Yohana Mbatizaji kama Yesu alivyofafanua waziwazi katika MATHAYO 17:10-13; MATHAYO 11:11-15. Yohana Mbatizaji anatajwa kutangulia mbele za Yesu katika roho ya Eliya na nguvu zake ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatia waasi akili (LUKA 1:13-17).
Yohana Mbatizaji anafananishwa na Eliya kwa jinsi ambavyo mavazi yao yalivyofanana (MARKO 1:6; linganisha na 2 WAFALME 1:8 na jinsi ambavyo huduma zao wote zinavyoanza kwa kuwaambia watubu kwa maonyo makali 2 WAFALME 1:5-8; linganisha na MATHAYO 3:6-10); na tena Eliya na Yohana Mbati5zaji wote walikuwa wanakaa nyikani mara kwa mara.
…………………………………………………………………………….
       Mpendwa msomaji, unaona sasa! Hakuna haja ya kusema, “Hivi kweli nitaweza kushinda dhambi duniani? Hivi kweli maisha ya wokovu nitayaweza?” Ni Neema juu ya Neema. Unalotakiwa kufanya ni kutubu dhambi zako tu kwa kumaanisha kuziacha; kwa imani tu, na mengine yanayofuata mwachie Yesu; na leo hii utashangaa kuona maisha yako yamebadilika ghafla na kwa urahisi utaona unaweza kufanya mapenzi ya Mungu, bila jitihada za kibinadamu. Je, uko tayari kutubu dhambi zako? Najua uko tayari. Basi sema hivi, Mungu wangu, natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha kuanzia leo. Asante kwa neema yako ambayo kwa hiyo tunaokolewa kutokana na kazi aliyoifanya Yesu. Niokoe sasa na kunipa neema ya kufanya mapenzi yako kuanzia sasa na wakati wote ujao. Asante kwa kuniokoa katika Jina la Yesu. Amen”. Ili uzidi kuukulia wokovu ulioupokea leo, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook, Twitter, n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “somo hili” kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s