KUHURUMIANA NA KUPENDANA KAMA NDUGU

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

 

SOMO LA 2  :  KUHURUMIANA NA KUPENDANA KAMA NDUGU

 

NENO LA MSINGI:

1 PETRO 3:8

Neno la mwisho ni hili, muwe na nia moja, WENYE KUHURUMIANA, WENYE KUPENDANA KAMA NDUGU, wasikitikivu, wanyenyekevu, watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka”.

<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><>< 

K

atika wokovu, moja ya mambo tuliyoitiwa ili kuirithi baraka, ni kuhurumiana na kupendana kama ndugu.  Biblia inatuamuru kudumisha upendo kati yetu [WAEBRANIA 13:1].  Yesu Kristo alisema kwamba, mataifa au watu ambao hawajaokoka, watakapotuona jinsi ambavyo tunapendana, ndipo watakapotutambua kuwa ni wanafunzi wa Yesu.  [SOMA YOHANA 13:35] Watu wote tuliookoka, ingawa tuko wengi; katika Roho moja, sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, na kunyweshwa Roho mmoja; bila kujali kabila, elimu, rangi, umri, utajiri n.k.  [SOMA 1 WAKORINTHO 12:12-13].  Kila mmoja wetu ni kiungo kimoja katika mwili, na viungo vyote katika mwili vina kazi muhimu.  Masikio, macho, pua, miguu, mikono, vidole n.k.; vyote vina kazi muhimu katika mwili; na tena kile kiungo cha mwili, kinachodhaniwa kuwa ni kinyonge zaidi; chahitajiwa zaidi [SOMA 1 WAKORINTHO 12:14-24].  Ilivyo ni kwamba, hakuna faraka au matengano katika viungo vya mwili.  Kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia.  Kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.  Ndivyo inavyotupasa kuwa, watu wote tuliookoka kama mwili wa Kristo [SOMA 1 WAKORINTHO 12:25-27].  Kidole kikikatwa na kisu, viungo vyote huumia na kuchukua hatua.  Moyo ukifurahi viungo vyote huonyesha furaha hiyo na kuishiriki n.k.  Kwa jinsi hiyo hiyo, watu tuliookoka, tu viungo vya mwili na inatupasa kuhusiana hivyo.  Kila mmoja inambidi amuangalie na kumjali mwenzake.  Mmoja wetu katika Kanisa la Nyumbani anapoumia, wote inatupasa kuumia pamoja naye.  Mmoja wetu akitukuzwa, inatupasa wote kufurahi pamoja naye.  Wote tulioko katika Kanisa la Nyumbani, ni viungo vya mwili mmoja.  Mmoja wetu katika Kanisa la Nyumbani anapoteswa na ndugu au wazazi wake mataifa kwa ajili ya wokovu wake; inatupasa wote kuteseka pamoja naye kwa kumsaidia kimwili katika mahitaji, na kumfariji; na pia kufanya maombi ya nguvu kila siku kwa ajili yake.  Mmoja wetu katika Kanisa la Nyumbani anapoumwa, inatubidi kumtembelea na kumwona; iwe ni kwake nyumbani au hospitali, na kumfariji; pamoja na kumpa mahitaji ya kimwili yakiandamana na kufanya maombi ya nguvu kwa ajili yake.  Mmoja wetu katika Kanisa la Nyumbani anapofiwa; anapofukuzwa kazi, anapoibiwa vitu nyumbani na wezi, ni lazima kila mmoja wetu ahusike kumpa faraja, kumpa mahitaji ya kimwili na kufanya maombi ya nguvu kwa ajili yake.  Mmoja wetu anapokuwa hana chumba cha kupanga au hana kazi n.k; ni lazima liwe jambo linalotuhusu viungo vyote vya mwili.  Vivyo hivyo upande wa furaha.  Mmoja wetu anapojifungua mtoto; anapooa au kuolewa, anapopandishwa cheo kazini, anapohamia katika nyumba mpya aliyoijenga, au kupata mafanikio yoyote; inatubidi kufurahi wote pamoja naye, na kumuonyesha furaha yetu kwa vitendo, na kumshukuru Mungu pamoja naye na kumuombea baraka na mafanikio zaidi. Kufanya hivi, ndiyo kuhurumiana na kupendana kama ndugu na KUCHUKULIANA MIZIGO kama viungo vya mwili mmoja.  Biblia inatuagiza katika WAGALATIA 6:2; “Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.”  Biblia inasema pia kwamba yeye ambaye hana upendano wa ndugu ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali na hana matunda, amesahau kutakaswa dhambi zake za zamani [SOMA 2 PETRO 1:7-9].  Pasipo Yesu kutupenda tungali wenye dhambi, tungekuwa wapi leo?  Kwa sababu hiyo, sisi nasi inatupasa kupendana kama Yeye alivyotupenda.

 

JINSI YA KUDUMISHA UPENDO

Jambo lile unalotaka kutendewa wewe na kuona kuwa ni upendo, lifanye WEWE KWANZA kwa wengine [MATHAYO 7:12].  Ukiwa miongoni mwa wale wanaolalamikia upendo kwa kutaka ufanyiwe mema wewe tu, basi ujue wewe ndiye chanzo cha kuvuruga upendo.  Mkristo hapaswi kuwa na ulimi wa kulaumu na kukosoa wenzake wakati wote.  Upendo haulaumu na kupenda kukosoa tu!  Kwa muda mrefu zaidi, kila aliye na upendo, katika mazungumzo yake, atayatafakari mema ya mwenzie na yale yaliyo mazuri, ya staha, ya kupendeza na sifa njema [SOMA WAFILIPI 4:8].  Kila aliye na upendo kwa ndugu, inampasa pia kutafuta kuwa na amani na watu wote wakati wote [WAEBRANIA 12:14].  Ikiwa mwenzio anakupita kila siku bila kukusalimu, kumwonyesha upendo na kutafuta amani, wewe ndiye unayepaswa kumsalimu kwanza.  Usingoje tu kumlaumu na kumkosoa kwa kusema “Fulani hana upendo”.  Kufanya hivyo kutaleta faraka badala ya kudumisha upendo.

 

M  A  S  W  A  L  I

 

1.         Taja mambo sita kati ya mambo tuliyoitiwa ili kuirithi baraka yaliyoorodheshwa katika

1 PETRO 3:8

(a)————————————————————————————————————-

(b)————————————————————————————————————-

(c)————————————————————————————————————-

(d)————————————————————————————————————-

(e)————————————————————————————————————-

(f)————————————————————————————————————–

 

2.         Ni jinsi gani ambayo mataifa au watu ambao hawajaokoka watakavyoweza kutambua sisi kwamba  ni wanafunzi wa Yesu?  [YOHANA 13:35]

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

3.         Watu tuliookoka, ingawa tuko wengi, katika Roho mmoja, tulibatizwa kuwa

———————————————– bila kujali—————————————————-

————————- na tulinyweshwa —————————————————————-

1 WAKORINTHO 12:13.

4.         Katika mwili, viungo vya mwili huhusiana namna gani?1 WAKORINTHO 12:25-27.

Uhusiano huu wa viungo vya mwili, unatufundisha nini juu ya uhusiano wa kila Mkristo na mwenzake?

—————————————————————————————————————-

<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><

1.Usikose faida zilizomo katika somo la kwanza ” KULIFUATA NENO LA MUNGU”, tafadhari bonyeza hapa ili ujifunze somo hili https://davidcarol719.wordpress.com/kulifuata-neno-la-mungu/

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

                                                         UBARIKIWE NA BWANA YESU!!!

<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s