KUKARIBISHANA NA KUANGALIANA SISI KWA SISI

ZACHARY KAKOBE

Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe


SOMO LA 3 :   KUKARIBISHANA NA KUANGALIANA SISI KWA SISI

NENO LA MSINGI:

1 PETRO 4:8-9

“Zaidi ya yote, iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi MKARIBISHANE NINYI KWA NINYI pasipo kunung’unika”.

WAEBRANIA 10:24

“TUKAANGALIANE SISI KWA SISI, na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri”.

<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><>< 

M

oja ya wajibu wetu katika wokovu, ni kukaribishana na kuangaliana sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo, kumpenda zaidi Yesu na kumtendea kazi nzuri.  Tuangaliane sisi kwa sisi kama kutembeleana na kufahamiana hali zetu za kiroho na kimwili tunapokuwa majumbani mwetu.  Haitoshi tu kukutana katika ibada za Kanisa Kuu na Kanisa la Nyumbani.  Ni lazima kwa kila mmoja katika Kanisa kufahamu majumbani kwao ndugu zake wote katika Bwana, walio katika Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, na zaidi sana kuwatembelea makwao wale walio katika Kanisa lake la nyumbani.  Sisi wote tulio katika Kanisa la Nyumbani ni lazima tutembeleane na kuangaliana majumbani mwetu, ili kujuana hali zetu wakati wote.  Ziko faida kadhaa ambazo zinamfanya Mungu atuagize katika Neno lake kukaribishana na kuangaliana sisi kwa sisi.

 

(1)       KUTAZAMANA KATIKA UGONJWA, MISIBA NA SHIDA MBALIMBALI

 

(a)       KUTAZAMANA KATIKA UGONJWA

Kutazamana sisi kwa sisi mmoja wetu anapokuwa akiumwa, ni wajibu mmojawapo katika upendo wa watu tuliookoka.  Tunapokuwa tunakwenda kumtazama mgonjwa nyumbani kwake, au anapokuwa hospitali na kumfariji na kufanya maombi kwa ajili yake; tunamtuliza moyo na kumfanya ajione yuko miongoni mwa ndugu wanaomjali, kumtambua, kuhusika naye, na kumpenda kama ndugu mwenzao.  Kinyume cha hapo hujisikia upweke na kujaribiwa.  Wajibu huu unapaswa kutimizwa na kila mmoja kwa mwenzie aliye katika Kanisa la Nyumbani.

Angalia mifano katika Biblia:

(i)         Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda, alikwenda kumtazama Mfalme Yoramu alipokuwa anaumwa [SOMA 2 WAFALME 8:29].

(ii)        Yehoashi Mfalme wa Israeli alikwenda kumtazama Nabii Elisha alipokuwa ameshikwa na             ugonjwa na kulia mbele zake katika maombi [SOMA 2 WAFALME.13:14].

(iii)       Yesu akitufundisha jinsi inavyotupasa kuwatendea watu waliookoka anasema “Nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama”  [MATHAYO 25:36,40]

 

(b)       KUTAZAMANA KATIKA MISIBA NA SHIDA MBALIMBALI

Kuna vipindi ambavyo mtu anaweza kupatwa na msiba akiwa amefiwa na jamaa yake, au kupatwa na mabaya mbalimbali kama kuibiwa vitu nyumbani baada ya kuingiliwa na wezi au majambazi n.k.  Inatupasa watu tuliookoka kwenda kumtembelea, kumfariji, kumtuliza moyo na kufanya maombi pamoja naye [ANGALIA MFANO: AYUBU 2:11-12].  Mungu anatuagiza pia katika Neno lake, kuwatuliza watu wake (waliookoka) mioyo yao, katika hali za misiba na shida mbalimbali [SOMA ISAYA 40:1].

(2)        KUJENGANA KILA MTU NA MWENZAKE KATIKA UPENDO

Kwa kutembeleana, tunazidi kufahamiana maisha yetu ya kiroho na kuangaliana, tukionyana na kuhimizana kusonga mbele katika utakatifu, katika safari yetu ya kwenda mbinguni [WAEBRANIA 10:24-25].  Bila kutembeleana na kufahamiana kwa karibu zaidi, mtu ataonekana kuwa ni kondoo akiwa katika ibada za Kanisa Kuu, kumbe ni mbwamwitu akiwa nyumbani kwake.  Kwa kutembeleana, yeye aliye na nguvu, anauchukua udhaifu wa mwenzie na kumjenga.  Mwenzetu anaweza kuwa mchanga kiroho au mwenzetu akawa na upweke akizungukwa na mataifa na kukosa faraja.  Hatupaswi kujipendeza wenyewe bali kwenda kumtembelea na kumjenga [SOMA WARUMI 15:1-3; I WATHESALONIKE 5:11].  Kuna siri kubwa katika kutembeleana.  Wageni wanaongeza kitu cha pekee nyumbani hasa wanapokuwa ni ndugu katika BWANA.  Wanaleta hali ya kupendana zaidi, na kila mmoja kujisikia anapendwa.  Kila mtu anahitaji kupendwa, na hii ndiyo njia pekee ya kuliondoa hitaji hili la kila mtu.  Kwa kutembeleana pia, tutaweza kuwaepusha ndugu zetu wachanga kiroho, katika hatari ya kudanganywa na kupotezwa na watu werevu wanaoweza kutoa ushauri potofu kwao.  [SOMA WAEFESO 4:14; 2 YOHANA 1:10-11].

(3)       KUFURAHI PAMOJA KINDUGU

Siyo kwamba nyakati zote ni za misiba, ugonjwa na mabaya katika maisha.  Nyakati nyingi zaidi, huwa ni nyakati za  furaha; na ni ukristo kushirikiana furaha.  Inaweza ikawa ni furaha ya kubatizwa katika maji tele, furaha ya kupokea Utakaso au furaha ya kujazwa au kubatizwa kwa Roho Mtakatifu; furaha ya harusi au kupata mtoto, au furaha ya kuhamia nyumba mpya baada ya ujenzi mgumu n.k.  Biblia inatuagiza katika hali hii, kufurahi pamoja na wafurahio [SOMA WARUMI 12:15].  Mungu anatuambia pia kufurahi katika yale anayotubarikia Bwana [SOMA KUMBUKUMBU 12:7].  Furaha inatimilika zaidi kwa mtu, anapoishiriki pamoja na wengine.  Furaha yetu sisi tuliookoka, inakuwa vema kuishiriki na ndugu zetu waliookoka; maana lugha yetu ya shukrani kwa Mungu na jinsi ya kufurahi ni ya namna moja.  Katika furaha zetu, hatutumii vileo au disco tofauti na mataifa.

MAMBO YA KUZINGATIA

Ikiwa tunakutana tu katika Kanisa Kuu au Kanisa la Nyumbani, ni vigumu kufahamu kama mwenzetu ana tatizo siku nyinginezo; bila kutembeleana mara kwa mara.  Hii ni hatari maana matokeo yake; tunaweza kupata taarifa za ugonjwa wa ndugu mwenzetu, wakati zimekwisha pita siku nyingi.  Huu siyo upendo ambao utawavuta mataifa kumtafuta Yesu aliye hai ndani yetu.  Inatupasa mara kwa mara kuangaliana kama watoto wa Baba mmoja aliye mbinguni.  Mara nyingi pia, baada ya ibada za Kanisa Kuu, hatupati nafasi kubwa ya mazungumzo na hii kutufanya kukosa kufahamiana kwa karibu na kupendana.  Ni mtu asiyetembea nuruni, ndiye pekee ambaye atapenda aje katika ibada za Kanisa Kuu, lakini asifahamike maisha yake nyumbani na kweli haimo ndani ya mtu wa jinsi hii [SOMA I YOHANA 1:5-7].

Matokeo ya kukaribishana na kuangaliana sisi kwa sisi, ni kwamba tutaweza kuwa na Kanisa lililojaa upendo; na Biblia inasema, upendo husitiri wingi wa dhambi jambo ambalo litatufanya kuishi katika utakatifu kila siku [I PETRO 4:8].  Matokeo mengine ni kwamba Kanisa la Nyumbani litakuwa na ongezeko la watu siku hadi siku, na hatimaye kusababisha ongezeko kubwa la watu katika Kanisa Kuu, kwa sababu Imani hutenda kazi kwa upendo [WAGALATIA 5:6b].  Jambo la kukumbuka, ni kwamba kupendana kwa kukaribishana na kuangaliana sisi kwa sisi; KUNAHITAJI JUHUDI NA JITIHADA YA KILA MMOJA [I PETRO 4:8; WARUMI 12:13].  Kila mmoja wetu, anapaswa kujua wajibu wake yeye, wa kuwatembelea wengine, kabla ya kupenda yeye tu kutembelewa.  Inampasa KILA MMOJA kuanza kwa juhudi na jitihada, kuwatembelea ndugu zake katika BWANA.  Tunapokuja katika Kanisa la Nyumbani, tunaangalia kwamba nani hakufika, na baada ya kusanyiko letu; tunakwenda kumwangalia nyumbani, na kumuuliza kwa nini hakufika.  Ikiwa mwenzetu hakufika katika ibada za Kanisa Kuu, tunamtembelea na kumjulia hali, na kama ni kutokana na uvivu, tunamhimiza katika upendo.

M  A  S  W  A  L  I

1.         Taja faida tatu za kukaribishana na kuangaliana sisi kwa sisi.

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

2.         Taja mifano miwili ya watu waliokwenda kuwatazama wenzao wagonjwa katika Biblia:

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

3.         Taja mfano wa ki-Biblia wa watu waliokwenda kumuangalia rafiki yao alipokuwa amepatwa na mabaya  ili kumtuliza moyo [AYUBU 2:11-12]

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

4.         Nini matokeo ya kukaribishana na kuangaliana sisi kwa sisi?

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

————————————————————————————————————–

1. Usikose faida zilizomo katika somo la 2 “KUHURUMIANA NA KUPENDANA KAMA NDUGU”, bofya hapa ili ujifunze somo hili https://davidcarol719.wordpress.com/kuhurumiana-na-kupendana-kama-ndugu/

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe hkwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. HaBaraka za Mungu zitakuwa pamoja nawe   

UBARIKIWE NA BWANA YESU!!!     <

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s