KULIFUATA NENO LA MUNGU

ZACHARY KAKOBE

Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe


SOMO LA 1   :    KULIFUATA NENO LA MUNGU

NENO LA MSINGI:

ZABURI 119:9:

“Jinsi gani kijana aisafishe njia yake?  Kwa kutii, AKILIFUATA NENO LAKO”.

<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><>< 

H

atupaswi kusitasita katikati ya mawazo mawili.  Mtu hawezi kumtumikia Baali yaani shetani na wakati huo huo akamtumikia Mungu.  Wakati wa kukata shauri kuokolewa, ni wakati wa kuamua yupi wa kumfuata; Mungu au Baali [1 WAFALME 18:21].  Ukristo, ni kuviacha vyote na kumfuata Yesu na kumtumikia.  Yesu anasema mtu akimfuata, basi atakwenda mbinguni kule aliko yeye [YOHANA 12:26].  Yesu Kristo anatufundisha jinsi mtu anavyoweza kufahamu kama yeye yuko miongoni mwa kondoo wa Kristo au la.  Kondoo wa Kristo, waijua sauti yake na KUMFUATA [YOHANA 10:26-27].  Katika Biblia, tunaona mifano ya watu waliomfuata Yesu alipokuwa duniani.  Petro na mitume wale wengine kumi na mmoja, waliacha vyote na wakamfuata Yesu [MARKO 10:28].  Wanawake wengi pia waliacha vyote na kumfuata Yesu na kumtumikia [MATHAYO 27:55-56].  Nyakati hizi tulizo nazo, Yesu Kristo, hayuko hapa duniani, katika mwili; amekwisha paa kwenda mbinguni kwa Baba.  Sasa basi, tutamfuata namna gani Yesu Kristo wakati hatumwoni kwa macho?  Jibu la swali hili, ndilo msingi wa somo letu leo katika Kanisa la Nyumbani.  Biblia inatoa jina jingine la Yesu Kristo.  Anaitwa Neno la Mungu [UFUNUO 19:13; YOHANA 1:1].  Katika YOHANA 14:6; Yesu Kristo anasema yeye ndiye NJIA na KWELI na UZIMA.  Neno la Mungu pia linaitwa UZIMA [YOHANA 6:63] KWELI [YOHANA 17:17] na NJIA [MATENDO 19:9;MITHALI 6:23].  Hapa tena tunaona kwamba Yesu Kristo ni Neno la Mungu.

Hivyo, tunajifunza kwamba KUMFUATA YESU NI KULIFUATA NENO LA MUNGU.  Hii ndiyo namna ya pekee ya kuisafisha njia yetu ya kwenda Mbinguni – KULITII na KULIFUATA NENO LA MUNGU [SOMA ZABURI 119:9].  Katika Ukristo, hatupaswi kuongozwa na mila na mapokeo ya wazee, desturi za mataifa au mazoea ya tangu utoto.  Inatubidi katika KILA JAMBO tuongozwe na Neno la Mungu na kulifuata.  Nyayo zetu lazima zishikamane na njia au nyayo za Yesu Kristo kwa Neno lake, na hii ndiyo njia ya kujiepusha na njia pana ya wale mataifa wenye jeuri [ZABURI 17:4-5].

Neno la Mungu ni taa na nuru au mwanga wa njia yetu [ZABURI 119:105; ZABURI 119:130;ZABURI 19:8].  Tukitaka kuhakikisha tunafika kwenye maskani ya Mungu, basi ni lazima tuongozwe na nuru na kweli ya Mungu au Neno la Mungu [SOMA ZABURI 43:3].  Wakati wote tunapopambana na jambo lolote, ni lazima tujiulize kwamba “Neno la Mungu linasema tufanye nini katika jambo hili au mazingira haya?”  Tukiliangalia Neno la Mungu kama taa ing’aayo mahali penye giza, tutafanya vema; na nyota ya asubuhi Yesu Kristo atazuka mioyoni mwetu; kutakapopambazuka wakati wa kuja kwake Yesu Kristo kulinyakua Kanisa lake [SOMA 2 PETRO 1:19].  Neno la Mungu katika maisha yetu, inabidi lipewe uzito kuliko chakula cha kimwili, maana Neno la Mungu ndilo chakula kishukacho kutoka juu mbinguni kwa ajili yetu [KUMBUKUMBU LA TORATI 8:3; AYUBU 23:12; YEREMIA 15:16].  Kwa ajili hii, tutakuwa safi na kuwa tayari wakati wote kunyakuliwa na Yesu ajapo kulinyakua Kanisa lake; kwa sababu tunasafishwa na Neno la Mungu kila siku maana Neno hutusafisha [SOMA YOHANA 15:3].  Neno la Mungu linafananishwa na KIOO [YAKOBO 1:23].  Tunapojiangalia katika kioo na kuona nywele zimejikunjakunja, huzichana na kuzinyosha.  Ikiwa kwa kutumia kioo, tunajigundua kwamba tuna tongotongo machoni; husafisha macho hayo.  Ikiwa tuna meno machafu, tunayasafisha kwa kupiga mswaki n.k.  Vivyo hivyo, inatupasa kuangalia maisha yetu – kusema kwetu, kutenda kwetu, kuwaza kwetu na kujiangalia katika kioo au Neno la Mungu na kujipima.  Ikiwa tumepinda mahali, basi tumruhusu Yesu kutunyosha.  Ikiwa ni wachafu mahali, tumruhusu Yesu kutusafisha.  Wakati wote tunapaswa kukubali kubadilishwa na Neno la Mungu.  Huku ndiko kulifuata Neno la Mungu au kumfuata Yesu na ndiyo njia pekee ya kuukulia wokovu.  KWA KUONGEZA MAARIFA, ANGALIA MAANDIKO, KUKUWEZESHA KUJIBU MASWALI YAFUATAYO:

MASWALI

 

1.         Kila anayelidharau Neno la Mungu na kukataa kulifuata na kuongozwa nalo, atajiletea hasara  zipi? [MITHALI 13:13; ISAYA 5:24]

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

  1. 2.            Neno la Mungu linapewa majina mengine kumi.  Yataje.  ZABURI 119:105; YEREMIA 23:29; WARUMI 1:16;  WAEFESO 6:17; YOHANA 6:63; YOHANA 17:17; ZABURI 119:103-104.

(i)—————————————-(ii)————————————- (iii)————————

(iv)————————————–(v)————————————–(vi)————————

(vii)————————————(viii)————————————- (ix)———————–

(x)—————————————————-

3.         Taja sifa TANO za Neno la Mungu [WAEBRANIA 4:12]

(i)————————————————————————————————————–

(ii)————————————————————————————————————-

(iii)————————————————————————————————————

(iv)————————————————————————————————————

(v)————————————————————————————————————-

4.         Tutafika maskani ya Mungu tukikubali kuongozwa na nini? [ZABURI 43:3].

—————————————————————————————————————-

Kusitasita kati ya mawazo mawili na kujaribu kumtumikia Mungu pamoja na Baali; ni

kuchagua maneno fulani katika Biblia aliyoyasema Yesu na kuyafuata, na mengine kuyakataa.  Hasara ya kufanya hivi ni nini?  [ZABURI 119:6]

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

Kumfuata Yesu na kuongozwa naye maana yake ni nini?  Ni kwa jinsi gani tunaweza

kuongozwa na Yesu na  kumfuata, ingawa hatumwoni kimwili?

—————————————————————————————————————-

Usikose faida zilizomo katika somo linalofuata “KUHURUMIANA NA KUPENDANA KAMA NDUGU”, bonyeza link hii ili ujifunze https://davidcarol719.wordpress.com/kuhurumiana-na-kupendana-kama-ndugu/

<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><>

          Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  “Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen”.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s