KULIZOEA NENO LA MUNGU

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SOMO:  KULIZOEA  NENO LA MUNGU

Somo hili ni muhimu sana kwa kila mtendakazi. Ufahamu wa somo hili utatuwezesha kufufuliwa kiroho na kutufanya tupige hatua mbele zaidi kiroho. Tunajifunza somo hili kwa kuligawa katika vipengele vitatu:-

(1).  NINI MAANA YA KULIZOEA NENO LA MUNGU?

(2).  MADHARA YA KULIZOEA NENO LA MUNGU.

(3)   DALILI ZA KULIZOEA NENO LA MUNGU.

(1). NINI MAANA YA KULIZOEA NENO?

Ili tufahamu ni nini maana ya kulizoea Neno la Mungu, ni muhimu kujifunza kwanza kinyume chake. Mtu ambaye hajalizoea Neno la Mungu anapokuja katika ibada huwa mnyonge mwenye shauku ya kusikia  ni Neno gain ambalo BWANA atalisema siku hiyo kupitia kwa watumishi wake. Mtu huyu huwa na roho iliyopondeka hivyo hutetemeka alisikiapo Neno la Mungu, na kupondeka kirahisi na kuwa tayari kulitendea kazi Neno la Mungu. Biblia inasema  katika ISAYA 66:2, “Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote,  vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu”. Mtu ambaye amekwisha kulizoea Neno la Mungu, yeye huwa hawi na shauku ya kulisikia  wala hatetemeki alisikiapo Neno la Mungu maana roho yake ni ngumu, haoni lolote la ziada katika Neno la Mungu.

(2).  MADHARA YA KULIZOEA NENO LA MUNGU

Wana wa Israeli waliangamizwa jangwani kwa sababu walilizoea Neni la Mungu, ingawa kila siku walikuwa wakilisikia (1WAKORINTHO 10:1-5). Wana wa Israeli walifikia mahali pa kudai wapewe mfalme mwanadamu badala ya Mungu aliyekuwa amewachosha, kwasababu walilizoea Neno lake (1SAMWELI 8:4-7), kwa  sababu hiyo, wpte hawakuingia Kaanani isipokuwa watu wawili tu, Kalebu mwana wa Yefune na Yoshua mwana wa Nuni (KUMBUKUMBU LA TORATI 1::35-38). Yuda Iskariote yeye naye yuko motoni leo kwasababu alilizoea Neno la Yesu Kristo ingawa alikuwa naye kila siku. Watu waliookoka siku nyingi au Watendakazi wengi huingia katika mtego wa kulizoea Neno. Tukiisha kulizoea Neno , tujue hatuwezi kuingia Kanaani, yaani mbinguni, bali mahali petu nin motoni. Bwana  atusaidie tusilizoee Neno la Mungu, katika jina la Yesu.

(3).  DALILI ZA KULIZOEA NENO LA MUNGU.

Zipo dalili kadha ambazo tunaweza kuziona kirahisi, kwa watu waliolizoea Neno la Mungu. Tukiziangalia, zitatusaidia kuwa na tahadhari:-

  • Watu waliolizoea Neno la Mungu, huhesabu kwamba Neno linalotoka katika

Kinywa cha Mtumishi   wa Mungu, ni neno lake huyu mwanadamu na wala siyo Neno la Mungu. Watu ambao hawajalizoea Neno la Mungu, huhesabu kwamba neno la ujumbe litokalo katika vinywa vya Watumishi wa Mungu, ni Neno la Mungu mwenyewe (1 WATHESALONIKE 2:13).

  • Watu waliolizoea Neno la Mungu, wanakuwa hawana shauku tena ya

Kuhudhuria  ibada zote. Watu hawa wanachagua kuhudhuria ibada fulanifulani tu na hata wakihudhuria wanaweza wakawa wanazurura nje tu bila kufuatilia Neno. Kwao kuwemo ndani ya nyumba ya Mungu siku zote siyo muhimu tena (LUKA 2:49), tofauti na mwanzoni walipokuwa wachanga kiroho, ambapo waliumia sana kukosa Neni la Mungu siku yoyote.

  • . Watu waliolizoea Neno hujiona wanajua Neno lote na kuona kwamba   maneno yanayofundishwa ni ya wachanga kiroho na siyo ya wale waliookoka siku nyingi. Mtu akijiona anajua Neno, hajajua Neno lolote bado kama impasavyo kujua        (1 WAKORITHO 8;2), ila tu ni kwamba amelizoea.
  • Mtu aliyelizoea Neno, hata akiketi kulisikia Neno, anakuwa mzito sana  kubadilishwa na Neno hilo, na kulitendea kazi kwa sababu roho yake ni ngumu, siyo roho iliyopondeka. Hufikiri ni mjanja kwa jinsi asivyo litendea kazi Neno la Mungu kwa bidii kama wakati wa uchanga wake, kumbe sasa ndiyo amekuwa mpumbavu (MATHAYO 7:24-27).

Bwana atusaidie, ili tusilizoee kamwe Neno la Mungu, na kama tumekwisha kulizoea, tutubu na kumwomba Mungu atuumbie roho iliyopondeka kama ile tuliyokuwa nayo mwanzo na kuzidi, katika jina la Yesu. https://www.facebook.com/david.carol.754

                                                       . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .         

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook, Twitter n.k,  kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

                                                         UBARIKIWE NA BWANA YESU!!!

Advertisements

3 comments on “KULIZOEA NENO LA MUNGU

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s