KUOGOPA VITA NA KURUDI MISRI KUSIKOKUWA NA VITA

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SOMO LA 6 :   KUOGOPA VITA NA KURUDI MISRI KUSIKOKUWA  NA VITA

NENO LA MSINGI:

YEREMIA 42:13-17:

“Lakini mkisema, Hatutaki kukaa katika nchi hii, msiitii sauti ya BWANA, Mungu wenu; mkisema, La! lakini TUTAKWENDA NCHI YA MISRI, AMBAYO HATUTAONA VITA, wala kuisikia sauti ya tarumbeta, wala kuona njaa kwa kukosa chakula; nasi tutakaa huko; basi lisikieni neno la BWANA, enyi mabaki ya Yuda, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Ikiwa mwakaza nyuso zenu kuingia Misri, na kwenda kukaa huko; basi, itakuwa, UPANGA MNAOUOGOPA UTAWAPATA HUKO, katika nchi ya Misri, nayo NJAA MNAYOIOGOPA ITAWAFUATIA MBIO HUKO MISRI, nanyi mtakufa huko.  Haya ndiyo yatakayowapata watu wote waelekezao nyuso zao kwenda Misri, na kukaa huko; watakufa kwa upanga, na kwa njaa, na tauni, hapana mtu awaye yote miongoni mwao atakayesalia, au kuokoka katika mabaya nitakayoyaleta juu yao”.

<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><>< 

T

ulitoka Misri katika utumwa na kutolewa katika utumwa huo, pale tulipokata shauri kuokolewa.  Sasa tunakwenda Kanaani nchi yenye maziwa na asali – mbinguni kwa Baba yetu.  Hata hivyo safari nzima ya kwenda Kanaani ni safari iliyojaa vita na kila mtu aliyeokolewa, lazima atapambana na vita.  Maisha yetu yatakuwa ya vita.  Vita nyumbani, ofisini, kiwandani, katika familia au ukoo, vita kwa mumeo au mkeo, vita kwa ndugu, vita kwa mataifa, vita kila mahali.  Yesu alisema, hakuja kuleta amani duniani, bali mafarakano.  Atakapomuokoa mtu yeyote basi atafarakana na babaye, mamaye, mkwewe na wale wa nyumba moja [SOMA LUKA 12:51-53].  Safari ya Kanaani haitakuwa safari ya mtelemko.  Ulimwengu yaani watu wasiookoka pamoja na mkuu wa ulimwengu yaani shetani, wote watatupiga vita, na kutukatisha tamaa ya kuendelea na safari.  Shetani anajua kulivyo kuzuri mbinguni, na hana nafasi tena ya kufika huko.  Kwa sababu hiyo atafanya kila njia kuturudisha Misri.  Baada ya kuokolewa na kuacha kupokea au kutoa rushwa, kuacha uasherati, kuacha kutumia uongo kuandika ovataimu (overtime au matumizi ya masurufu ya safari (imprest), kuacha wizi, kuachana na marafiki wabaya, kuacha biashara zilizo kinyume na Neno la Mungu kama kuuza sigara, kuuza pombe n.k.; unaweza kupambana na njaa ya kukosa chakula ulichokizoea, na kushawishika kurudi katika nchi ya Misri yaani katika dhambi; kwa matumaini ya kupata chakula hicho.  Wana wa Israeli katika safari ya Kanaani iliyojaa vita, walikufa moyo kwa sababu ya ile njaa; wakamnung’unikia Mungu na Musa, wakisema “Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri ili tufe jangwani?  maana hapana chakula wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu [SOMA HESABU 21:4-5; KUTOKA 16:3].  Matokeo yake, Mungu alituma nyoka za moto kati ya watu hao na kuwauma, watu wengi wakafa [HESABU 21:6].  Hatutapata faida yoyote, tutakapoamua kurudi nyuma katika wokovu na kwenda Misri kwa sababu ya njaa.  Biblia inasema kwamba, kurudi nyuma kwao wajinga, kutawaua [SOMA MITHALI 1:32a]. Unapookoka pia, utashangaa kwamba uhusiano wako wa mwanzo na nduguzo utapungua bila sababu ya maana.  Utashangaa kwamba Baba hafurahii mwanae kuokoka na kuacha pombe, sigara na disco.  Ni kwa sababu Ibilisi anatenda kazi ndani yake.  Utashangaa kwamba mume hafurahii mkewe akiokoka kwa sababu tu kwamba hawatakwenda kwenye anasa.  Yote ni vita ya shetani dhidi yetu ili tumrudie.  Utapambana na vita kila sehemu.  Usiogope vita na kutamani kurudi Misri kusikokuwa na vita, sauti ya tarumbeta au njaa ya kukosa chakula.  Mungu anasema ukifanya hivyo, njaa unayoiogopa na vita unavyoviogopa vitakufuatia mbio huko Misri nawe utakufa.  Kwa nini tuogope vita?  Hakuna sababu ya kuogopa kwa sababu Bwana wetu Yesu ni mtu wa vita, ni BWANA wa Vita na Jemadari wetu wa vita.  Tunapopambana na vita, vita si yetu ila ni yake Bwana wetu [SOMA KUTOKA 15:3; 2 NYAKATI 20:15].  Tunapaswa kumweleza BWANA vita vyetu na yeye atatupigania [SOMA KUTOKA 14:14].  Mpango wa Mungu, ni kumfundisha vita kila mtu aliyeokoka.  Sisi sote ni askari wa Yesu na hivyo inatubidi kuvifahamu vita. [SOMA 2 TIMOTHEO 2:3-4].  Mungu mwenyewe aliwafundisha vita wale wote ambao hawakuvijua vita vya Kanaani.  Sababu ni kwamba Mungu wetu anafurahishwa sana na mtu atakayeweza kuzishika amri za BWANA na kuzidi kumpenda Yesu wakati wa vita bila kunung’unika.  Huo ndio upendo kwa Mungu.  [SOMA WAAMUZI 3:1-4].  Hatupaswi kamwe kuacha wokovu kwa kuogopa vita na kurudi Misri, bali tukaze mwendo mpaka mwisho na kushinda.  Biblia inasema Uwe mwaminifu hata kufa na utapewa taji ya uzima na ukishinda, hutapatikana na madhara ya mauti ya pili [UFUNUO 2:10-11].  Soma pia UFUNUO 2:17, 25-28; UFUNUO 3:11-13, 21-22].  Kumbuka, kwamba watu waliookoka waliompa ibilisi nafasi, wanaweza pia kutupiga vita.  [SOMA MIKA 7:6].

 

M   A   S   W   A   L   I:

 

(1)       Safari nzima ya kwenda Kanaani ni safari iliyojaa nini?

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

(2)       Yesu anatuambia nini katika LUKA 12:51-53?

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————

 

(3)       Ukiwa hutaki kukaa katika nchi ya wokovu, kwa kuogopa vita na njaa ya kukosa chakula; na kuamua kurudi Misri utapatwa na nini huko?  [YEREMIA 42:13-17].

 

—————————————————————————————————————-

 

—————————————————————————————————————-

 

—————————————————————————————————————-

 

—————————————————————————————————————-

(4)       Kurudi nyuma kwao wajinga na kurudi Misri kutawaletea madhara gani?

[MITHALI  1:32a].

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

(5)       Hatupaswi kuogopa vita tunapopambana na vita kwa sababu gani?

[2 NYAKATI 20:15; KUTOKA 15:3].

—————————————————————————————————————-

sikose faida zilizomo katika somo lililotangulia “KIPIMO KIKUBWA CHA MTU MKAMILIFU”, ingia hapa ujifunze Neno la Mungu https://davidcarol719.wordpress.com/kipimo-kikubwa-cha-mtu-mkamilifu/

<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><>< 

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

                                                         UBARIKIWE NA BWANA YESU!

<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><> 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s