KUYASHIKA MAPOKEO YA WAZEE

Neno la Uzima kutoka kZACHARY KAKOBEwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SIKU YA KUICHAMBUA BIBLIA.

SOMO:  KUYASHIKA MAPOKEO YA WAZEE 

(MATHAYO 15:1-20)

          Katika MATHAYO 15:1-20, tunajifunza mengi katika somo letu la leo kuhusu mapokeo ya wazee.  Tutaligawa somo letu katika vipengele vinne:-

(1)NINI MAANA YA MAPOKEO YA WAZEE?

(2)MAPOKEO YA WAZEE KATIKA MISTARI HII;

(3)MADHARA NA MAONYO YA KUYASHIKA MAPOKEO YA WAZEE;

(4)WAJIBU WETU WA KWENDA KINYUME NA MAPOKEO YA WAZEE, NA GHARAMA ZAKE.

 

(1)      NINI MAANA YA MAPOKEO YA WAZEE?

Ili tufahamu kwa undani kuhusu jambo hili, tutagawa pia kipengele hiki katika sehemu mbili:-

  1. 1.     NINI MAANA YA WAZEE;
  2. 2.     NINI MAANA YA MAPOKEO.

 

  1. 1.     NINI MAANA YA WAZEE?

Ni muhimu kufahamu “Wazee”, nyakati hizi za Mafarisayo na waandishi katika Biblia,

 walikuwa watu gani ili kulielewa vizuri somo letu.  Walimu wa torati ambao walikuwa

wanaitafsiri na kuielezea torati au Neno la Mungu, walipewa majina kadha.  Waliitwa

“WAANDISHI”, “MARABI” au “WAZEE”.  Viongozi wa dini waliheshimiwa sanana    

Wayahudi na maneno yao yalichukuliwa kuwa ni yenye uzito kuliko hata Neno la Mungu  mwenyewe.

  1. 2.     NINI MAANA YA MAPOKEO

         Wazee hawa, waliongeza maneno yao na amri zao katika maneno ya Mungu na pia kupunguza katika Maneno ya Mungu.  Wayahudi katika ujinga wao, walihesabu kwamba kuongeza au kupunguza huku kulikokuwa kunafanywa na wazee eti ni sawa na “KULIPIGA MSASA NA KULING’ARISHA NENO LA MUNGU”.  Yote yaliyoongezwa na kupunguzwa na wazee yalishikwa na Wayahudi kwa uzito zaidi kuliko Neno la Mungu.  Waliwafundisha watoto wao na watoto wakawafundisha watoto wao.  Watu walipokea mafundisho ya wanadamu na kuyakubali kuliko Neno la Mungu.  Haya ndiyo yanaitwa MAPOKEO YA WAZEE.  Baadaye yalikusanywa na kuandikwa pamoja katika kitabu kinachoitwa “MISHNAH”, kitabu cha mapokeo ya wazee.

(2)      MAPOKEO YA WAZEE KATIKA MISTARI HII   (MST.2)

(a)       Kunawa kabla ya chakula, kulikuwa na masharti kadha katika mapokeo ya wazee.  Mtu alitakiwa kunawa hadi kiwiko kabla ya kula na yalikuwepo mabalasi au mapipa fulani maalum ambayo yakijazwa maji, mtu akichovya mikono yake, maji yaliufunika mkono kupita kiwiko (MARKO 7:1-5; YOHANA 2:6).  Wanafunzi wa Yesu walinawa mikono kawaida tu na wakahesabiwa wana mikono najisi.

(b)       Watoto walifundishwa kwamba msaada wowote ambao wangetakiwa kutoa kwa wazazi wao ikiwa watawaambia kuwa ni “Korbani“ au “Wakfu“ basi watakuwa hawawajibiki kuwasaidia wazazi wao (MST. 4-6; MARKO 7:10-13).  Yote haya, yalikuwa ni tofauti na Neno la Mungu.

(3)      MADHARA NA MAONYO YA KUYASHIKA MAPOKEO YA WAZEE

1.         Biblia inaonya vikali kuhusu kupunguza au kuliongeza Neno la Mungu na kwamba wafanyao hivyo wanatafuta mapigo na kuondolewa sehemu yao mbinguni (KUMBUKUMBU LA TORATI 4:2; 12:32; UFUNUO 22:18-19);

2.         Yesu anatuonya kutokulitangua Neno la Mungu na kulikataa na kukubali kuyashika mapokeo ya wazee (MATHAYO 15:3; MARKO 7:8-13);

3.         Neno la Mungu linazidi kutuonya kulishika Neno la Mungu na kuyatupilia mbali mapokeo ya wazee au mafundisho na maagizo ya wanadamu (WAKOLOSAI 2:8; 1 TIMOTHEO 1:13-14; TITO 3:9);

4.         Kumwabudu Mungu na wakati huohuo mtu anashika mafundisho na maagizo ya wanadamu ni kumwabudu Mungu “BURE“ yaani bila faida yoyote tutakayoipata.  Ni kumheshimu Mungu kwa mdomo na moyo uko mbali naye.  Ni unafiki (MATHAYO 15:7-9).  Mungu anawahitaji watu watakaomwabudu katika ROHO NA KWELI – wakiongozwa na Neno la Mungu ambayo ndiyo kweli pekee.

(4)      WAJIBU WETU WA KWENDA KINYUME NA MAPOKEO YA WAZEE NA GHARAMA ZAKE

Ili Ukristo wetu uwe wa kweli, basi ni lazima tujiepushe kabisa na mapokeo ya wazee.  Mila zozote za kikabila zilizo kinyume na Neno la Mungu pamoja na mafundisho yoyote ya “kidini“ yaliyo kinyume na Neno la Mungu; ni lazima tuwe mbali nayo.  Kwa kufanya hivi, ndugu, wazazi wetu na viongozi wa dini walioshika mapokeo haya, watachukizwa (MATHAYO 15:12).  Pamoja na kuchukizwa kwao, tunapaswa kuhakikisha tunang’oa kila pando asilolipanda Baba yetu wa Mbinguni kwa kuwaeleza yote yaliyo kinyume na Neno la Mungu bila kuhofu wala kujali (MATHAYO 15:12-13).  Kisha hatupaswi kukubali maongozi yao yote yanayoendana na mapokeo ya wazee.  Kiongozi yeyote ambaye hawafundishi watu sawa na Neno la Mungu bali anafundisha sawa na mapokeo ya wazee, huyo anaitwa KIONGOZI KIPOFU WA VIPOFU.  Hatupaswi kukubali kuongozwa na watu jinsi hii maana tutatumbukia shimoni pamoja nao (MATHAYO 15:14).  Tunatiwa unajisi kwa kuliasi Neno la Mungu na siyo kuyaasi mapokeo ya wazee (MATHAYO 15:18-20).

Hatupaswi kubabaishwa kwa vitisho vya Mafarisayo wanaotaka tufuate mapokeo ya wazee.  Yesu Kristo kama alivyokuwa upande wa wanafunzi wake walipokwenda kinyume na maagizo ya wanadamu yuko upande wetu pia tukifanya hivyo.  Wakitutisha kwamba watatuachia laana, ni muhimu kufahamu kuwa laana hiyo haitatupata (MITHALI 26:2).

JE, UNATAKA KUOKOKA SASA?

Tunasoma haya katika LUKA 1:77, “Uwajulishe watu wake wokovu, katika kusamehewa dhambi zao”.   Hii ina maana kwamba ukiisha kutubu dhambi zako leo utasamehewa kwa hakika, na hivyo kupata wokovu mara moja.  Je, kweli utasamehewa?  Jibu ni Ndiyo!  Yesu mwenyewe anasema katika YOHANA 6:37, “……….Wala yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe”.  Hivyo kwa dhahiri, leo hii, dakika hii hii, utasamehewa na kupata wokovu.  Je, uko tayari kuokoka sasa na kuhesabiwa miongoni mwa wale watakaoingia mbinguni na kuishi na Mungu milele, hata wakiiaga dunia sasa hivi?  Ukiwa tayari kuifuatisha sala ifuatayo ya toba, mara tu baada ya sala hii, nitakuombea na kwa ghafla utawezeshwa kushinda dhambi.  Je, uko tayari kuifuatisha sala hii sasa?  Najua uko tayari.  Basi sema maneno haya“Mungu Baba, natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Naomba unisamehe na kuniosha dhambi zangu kwa damu ya Yesu iliyomwagika msalabani.  Niwezeshe kushinda dhambi kuanzia sasa.  Liandike sasa jina langu katika kitabu cha uzima mbinguni.  Asante kwa kuniokoa, katika Jina la Yesu, Amen”.  Sasa ninaomba kwa ajili yako, “Mungu Baba msamehe kiumbe wako huyu dhambi zake zote, na mpe uwezo wa kushinda dhambi kuanzia sasa na kumuokoa. Mbariki kwa baraka zote katika Jina la Yesu, Amen”.  Tayari umeokoka.  Ili uzidi kuukulia wokovu, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI!!!

                                     . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .   . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .         

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “somo hili”  kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.Amina!!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s