MASHARTI YA KUMFUATA YESU

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SIKU YA KUICHAMBUA BIBLIA

SOMO:          MASHARTI YA KUMFUATA YESU  (MATHAYO 16:21-28)

Katika MATHAYO 16:21-28, kuna mengi ya kujifunza kwa mwanafunzi wa Biblia.  Ingawa kichwa cha somo letu ni “MASHARTI YA KUMFUATA YESU”, ni muhimu kufahamu kwamba hiki ni kipengele kimoja tu katika vipengele vinne vinavyotuongoza katika kuyatafakari yote tunayoyapata katika mistari hii.  Vipengele hivi vinne vya somo letu la leo, ni hivi vifuatavyo:-

 

(1)KUTABIRIWA KWA KIFO NA KUFUFUKA KWA YESU (Mst. 21);

(2)KUSHAWISHIWA KWENDA MBALI NA MPANGO WA MUNGU (Mst. 22-23);

(3)MASHARTI YA KUMFUATA YESU (Mst. 24-26);

(4)KUTABIRIWA KWA KUJA KWA YESU MARA YA PILI (Mst. 27-28).

 

(1)      KUTABIRIWA KWA KIFO NA KUFUFUKA KWA YESU (Mst. 21)

Kifo cha Yesu Kristo hakikuwa kifo cha kawaida.  Yesu Kristo hakukutwa na kifo chake bila kufahamu mapema kama wanadamu wengine.  Mapema sana, Yesu Kristo, alitabiri na kufundisha jinsi atakavyokufa na kwamba atafufuka siku ya tatu.  Alirudia mara kwa mara kueleza hivyo (MATHAYO 17:22; 20:17-19; 26:1-2; MARKO 8:31; 9:31; 10:32-34; LUKA 9:22,44; 18:31-34).  Ilikuwa ni mpango wa Mungu, Yesu Kristo kufa.  Alikuja duniani ili afe kwa sababu zifuatazo:-

  1. Awe ni mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu (YOHANA 1:29;        1 WAKORINTHO 5:7; 1 PETRO 1:19; ISAYA 53:7; 1 YOHANA 3:5; WAGALATIA 1:4);
  2. Afe kwa niaba yetu, achukue adhabu yetu ya mauti ya milele (WAEBRANIA 2:9; WAGALATIA 3:13; 1 PETRO 3:18).

Kufufuka kwake kulionyesha ushindi juu ya mauti.  Sisi nasi kwa kumwamini tunapewa kushinda uchungu wa mauti yaani dhambi (1 WAKORINTHO 15:56-57).

 

(2)      KUSHAWISHIWA KWENDA MBALI NA MPANGO WA MUNGU (Mst. 22-23)

Tunapodhamiria kutekeleza mpango wowote wa Mungu kwetu, ni muhimu kufahamu kwamba watakuwepo watu watakaotumiwa na Shetani kutushawishi kuuacha mpango wa Mungu kwetu.  Watu hawa watakuwa watu wa nyumbani kwetu yaani ndugu zetu wa kimwili na kiroho walio karibu nasi.  Watatumia maneno ya kutuonea huruma kwa yale yatakayotugharimu au kutupata katika kutekeleza mpango huo.  Hatupaswi kuwasikiliza.  Siyo wao ila ni shetani anayewatumia.  Kazi yetu ni kumtii Mungu na kumpinga Shetani naye atatukimbia (YAKOBO 4:7).

 

MASHARTI YA KUMFUATA YESU (Mst. 24-26)

  1. KUJIKANA MWENYEWE KILA SIKU – Kuyaacha mapenzi yetu, furaha zetu na matakwa ya miili yetu yaliyo kinyume na Mungu.  Kukataa uhuru wowote ulio mbali na haki na kutafuta kila siku uhuru ulio mbali na dhambi (WARUMI 6:20-22; 8:12-13);
  2. KUJITWIKA MSALABA – Tunapaswa kujitwika msalaba kila siku katika kumfuata Yesu (LUKA 9:23).  Msalaba ni dalili ya aibu, kudharauliwa, kudhihakiwa, kulaumiwa, kutukanwa na pia kupata maudhi na mateso.  Kila siku lazima tukubali kuyabeba haya na kudumu tu katika imani (2 TIMOTHEO 3:12; WAFILIPI 1:29-30; WAKOLOSAI 1:23).
  3. KUMFUATA YESU KILA SIKU – Ili tukae na Yesu milele, tunapaswa kumfuata Yesu kila siku, saa na dakika; siyo kwa muda fulani tu wakati wa raha, mahitaji n.k. (YOHANA 10:27).

 

(4)      KUTABIRIWA KWA KUJA YESU MARA YA PILI (Mst. 27-28)

Kama Yesu alivyotabiri kufa na kufufuka kwake na ikatokea vivyo hivyo, ni muhimu kufahamu pia utabiri huu utatimia wakati wowote ujao.  Ni muhimu kuifanya kazi ya Mungu kwa bidii ili tulipwe kadri ya matendo yetu (1 WAKORINTHO 15:58; UFUNUO 14:13).

Katika Mst. 28, wanafunzi wanaotajwa kwamba hawataonja mauti mpaka wamemwona Yesu akija katika Ufalme wake, ni Petro, Yakobo na Yohana ambao walipelekwa juu ya mlima mrefu faraghani na huko wakamwona Yesu katika utukufu wa Ufalme wake (MATHAYO 17:1-2)

…………………………………………………………………………………………………………………………………..

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “somo” hili, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa naw

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s