MBINGU MPYA NA NCHI MPYA

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SOMO: MBINGU MPYA NA NCHI MPYA

Baada ya kujifunza masomo mengi mfululizo kuhusu “matukio ya mwisho”, leo tunajifunza somo la mwisho kabisa katika mfululizo huu. Baada tu ya hukumu ya kiti cha enzi kikubwa cheupe, ndipo utakapofuata “         MWISHO WA MIISHO YOTE”. Ni makusudi  basi ya somo letu la leo kujifunza juu ya mwisho wa miisho yote. Tutaligawa somo letu la leo katika vipengele vinne:-

  1. KUUNGUZWA NA KUFUMULIWA KWA MBINGU NA NCHI ZA SASA
  2. UUMBAJI WA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA
  3. MAISHA KATIKA YERUSALEMU MPYA
  4. SIFA ZA KUISHI MILELE KATIKA YERUSALEMU MPYA.

1.     KUUNGUZWA NA KUFUMULIWA KWA MBINGU NA NCHI ZA SASA

 Mara tu baada ya hukumu ya kiti cha enzi kikubwa cheupe, ndipo utakapofuata mwisho wa miisho yote. Yesu Kristo katika mafundisho yake, alirudia tena na tena akieleza kwamba, mbingu na nchi za sasa ZITAPITA, yaani zitatoweka ( MATHAYO  24:35; MARKO 13:31; LUKA 21:33 ). Wakati wa tukio hili ndio huu. Tangu mapema kabisa Mungu wetu anatufundisha kwamba, mbingu na nchi za sasa zitachakaa na kuharibika, na kama mavazi, Mungu ATAZIBADILISHA (ZABURI 102:25-26 ). Nchi ya sasa yaani dunia hii au ulimwengu, umechosha na kuchakaa mno Baaya ya kukaliwa na mamilioni ya wenye dhambi wanaofanya machukizo mbele za Mungu. Dunia hii imechakazwa kwa gharika wakati wa Nuhu na vita vya kila namna mpaka vita ile ya mwisho “GOGU NA MAGOGU”. Miti yake mizuri imetumika kutengeneza sanamu za kuabudu, kila namna ya matambiko na machukizo yamefanywa ulimwenguni. Damu ya watu imemwagwa kwa wingi wake tangu damu ile ya Habili.     Dunia imejaa harufu ya damu. Haifai kukaliwa tena. Siyo hilo tu, mbingu hizi zilizojuu yetu yaani anga na sayari, vyote vimejaa rekodi ya maneno ya wanadamu ya matusi, na lugha chafu za kumkufuru Mungu na mpango wake wa Wokovu. Vimejaa harufu za uzinzi na uasherati za matendo ya Sodoma. Mbingu hii ya kwanza nay a pili vyote havifai. Siyo mbingu hizi tu. Hata mbingu ya tatu yaani mbinguni kwa sasa hakufai pia. Hapa ndipo mahali palipotunza kumbukumbu zote za dhambi za wanadamu katika vitabu vya hukumu kwa maelfu ya miaka. Rekodi hizi pia zimeifanya mbingu hii pia kuchukiza, haifai nayo! Kwa hiyo Mungu atazikamata nchi na mbingu hizi za sasa na kuziunguza, na kila kitu ndani yake, kitafumuliwa na kutoweka kama moshi kwa MSHINDO MKUU ( 2PETRO 3:7, 10-13 ; ISAYA 51:6 ). Mamilioni ya tani za gesi za Oxgen, HydrogenAcetylene n.k, vyote vitateketea na kuyeyushwa kabisa. Na madini ya kila namna yatayeyuka kila kitu, majengo, miti yote na vinginevyo kama Bahari n.k kisha vitawaka kama moshi na kutokuonekana tena kabisa. Huu ndio mwisho wa miisho yote. Baada ya hapo ndipo Bwana Mungu mwenye uwezo wote atakapoumba mbingu na nchi mpya mbele za macho yetu.

  1. 1.      UUMBAJI WA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA.

       Tutamuona Mungu wakati huu akisimama kama Muumbaji. Kama alivyoumba mbingu na nchi za sasa. Ndivyo ATAKAVYOZIFANYA mbingu mpya na nchi mpya. Hizi kwa sasa hazijaumbwa kabisa. Zitaumbwa wakati huu. Tazama atayafanya yote kuwa mapya ( ISAYA 66:22; ISAYA 65:17; 2PETRO 3:13; UFUNUO 21:1-7 ). Mbingu hizi na nchi mpya zitakuwa ni nzuri mno, hakuna mfano wake uliowahi kuwako au utakaokuwako. Ufundi wote wa uumbaji wa Mungu utaishia hapa. Hapa ni mahali watakapoishi wateule wake Mungu milele na milele. Wala walio ndani ya Kristo Yesu ni VIUMBE VIPYA na hivyo wanastahili kukaa katika MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. Hapa ni zaidi sana ya Bustani ya Edeni. Ni zaidi sana ya mbingu ya sasa wanaoikaa Watakatifu.

  1. 2.      MAISHA KATIKA YERUSALEMU MPYA

Nami nikaona mji ule mtakatifu, YERUSALEMU MPYA, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mmewe ( UFUNUO 21:2 ). Yerusalemu mpya ndio utakaokuwa MAKAO MAKUU ya mbingu hii mpya na nchi mpya. Neno “YERUSALEMU”, linatokana na maneno ya kiebrania, Y’ RU-SHALAIM. Y’RU maana yake “KUWEKA” na SHALAIM maana yake “MISINGI YA AMANI”. Hivyo Y’RU-SHALAIM maana yake KUWEKA MISINGI YA AMANI. Vivyo hivyo neno Yerisalemu linatokana pia na maneno JIREH-SHALOM. Neno “ JIREH” maana yake ATAWAPA na Neno “SHALOM” maana yake AMANI. Hivyo JIREH-SHALOM, maana yake ATAWAPA AMANI. Yerusalemu ya sasa iliitwa hivyo kwasababu ndipo ambapo Yesu Kristo alipokuja kutuwekea misingi ya Amani kwa kutupatanisha na Mungu kwa damu yake. Kisha akasema ‘AMANI NAWAACHIENI; AMANI YANGU NAWAPA” ( YOHANA 14:27 ). Baada ya mtu kuwa na Amani kwa Mungu na kuwa na amani ya Mungu ipitayo fahamu zote, hatimaye ataingia YERUSALEMU, mji uliojengwa juu ya MISINGI YA AMANI.

Biblia inaeleza kwa sehemu juu ya jinsi mji huu utakavyokuwa. Lugha zetu tulizonazo duniani zinaweza tu kutuelewesha juu ya udongo, milima, maji, mito n.k, kwa jinsi tunavyoifahamu katika dunia hii,. Sasa duniani hautakuwapo wa jinsi hiyo na yote mengine. Hata hivyo, tukisoma  katika UFUNUO 21:10-27; 22:1-5, tunapata kuelewa mambo kadhaa. Mwangaza wa Yerusalemu mpya siyo kama mwangaza huu tulionao. Mwangaza huu uko kama madini yanayoghara sana yenye rangi ya kijani iliyochanganyikana na bluu yanayoitwa YASPI. Hata hivyo ni mwangaza unaokufanya uone ndani yake kama bilauli yaani gilasi ya maji. Mji huu umejengwa juu ya misingi kumi na mbili ( 12 ) yenye majina ya mitume kumi na mbili ( 12 ) wa Yesu Kristo. Mtume wa 12 bada la Yuda atakuwa Mathia aliyefuatana na wale kumi na moja wakati wote wa Bwana Yesu na akahesabiwa pamoja na wale kumi na moja ( MATENDO 1:16-26 ). Mji huu marefu yake, mapana yake na kwenda juu ni sawasawa ( maili 1500 ). Majengo yake ni marefu sana, maili 1500 kwenda juu! Mji wa New York haufui dafu yoyote pamoja na majengo yake mengine yenye orofa 160! Ukuta wake ni dhiraa 144 ( karibu futi 300 ). Kuta hazikujengwa kwa tofariza simenti au udongo! Ni madini ya ajabu! Dhahabu safi mfano wa kioo safi-hakuna dhahabu ya namna hii duniani. Madini ya ajabu yanatumika katika ujenzi huu, YASPI, tulioiona hapo mwanzo, YAKUTISAMAWI, mawe ya bluu yenye ugumu unaofuatia madini ya almasi. KALKEDONI, aina ya madini mazuri sana yenye rangi aina nne mbalimbali-nyekundu iliyochanganyikana na njano, brown iliyochanganyikana na nyeusi, bluu iliyochanganyikana na nyeupe, rangi ya maziwa. ZUMARIDI, madini ya kijani, SADONIKI, madini yenye rangi tatu, bluu, nyeupe na nyekundu. AKIKI, madini yenye rangi ya damu, KRISOLITHO, madini yaliyo kama dhahabu ila yana rangi ya kijani iliyochanganyikana na njano. ZABARAJADI, madini yanayoonesha ndani yenye rangi ya bluu iliyochanganyikana na kijani.. YAKUTI MANJANO, madini mazuri yenye rangi tatu pamoja, njano, kkijani na bluu. HIAKINTHO, madini yenye rangi nyekundu iliyochanganyikana na njano. AMETHISTO, madini yenye rangi ya dhambarau yenye bluu na wekundu ndani yake. Milango yake ni LULU moja kila mmoja . Madini ya lulu yanayopatikana duniani yana umbo dogo sana kama mawe madogo tu siyo ukubwa wa mlango mkubwa kama huu. Lulu ni aina fulani ya madini ya thamani kubwa ambayo hupatikana katika wanyama fulani wa baharini wenye gamba au kombe wa aina ya chaza ( oyster ). Lulu hizi hupatikana kutoka kwa wanyama hawa, wanapopatwa na aina fulani ya maradhi yanayosadikika kuchukua miaka saba. Kama lulu hizo hazipatiakni katika kipindi hicho, wanyama hao hufa, na lulu zikapotea. Thamani ya lulu moja ni karibu US 400,000, ambazo ni karibu sawa na Tshs. 200,000,000! ( kwa mwaka 1993 ). Barabara za mji huu ni dhahabu safi kama kioo!siyo lami! HAKUNA USIKU HUMO! Maisha katika mji huo, yatakuwa maisha ( UFUNUO 19:1 ; 7:9-12 ; 5:11-14 ). Leo tunafahamu kwa sehemu yale tu tuliyofunuliwa, lakini huko tutajua yote ( KUMBUKUMBU 29:29; 1WAKORINTHO 13:12 ). Maswali ya kupumzika ( UFUNUO 14:13 ), furaha tele, hakuna maombolezo wala kilio ( UFUNUO 21:4 ), kumtumikia Mungu ( UFUNUO 22:3 ), kumwabudu na kumsifu Mungu mengi tuliyonayo yasiyo na majibu leo, hayatakuwako tena.

  1. 3.            SIFA ZA KUISHI MILELE KATIKA YERUSALEMU MPYA.
  1. 1.      Utakatifu ( WAEBRANIA 12:14 ). Wenye dhambi hawataingia mji huu                 ( UFUNUO 21:8; 22:14-15 ).
  2. 2.      Kuacha kupunguza neno lolote katika maagizo ya Mungu aliyotupa kuyafanya. Kuyaangalia yote ( UFUNUO 22:19; ZABURI 119:6 )
  3. 3.      Kuwa  mbali na uvuguvugu yaani kuipenda dunia na kumpenda Yesu wakati huohuo. Huu unaitwa unyonge. Wanyonge hawataingia hapa. Ni wale tu waliotayari kuishikilia imani hata kwa gharama ya kifo ( UFUNUO 3:16-17; 21:27; 2:10 ).

             ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

        Mpendwa msomaji, baada ya kusikia yote haya kutoka kwa nabii aliyetumwa kukuletea ujumbe huu, usifanye moyo wako kuwa mgumu.  Hii ni nafasi ya kipekee ya kuokoka.  Je, unajuaje kama utaamka kitandani baada ya kulala usiku wa leo?  Wakati uliokubalika wa wokovu ni sasa (2 WAKORINTHO 6:2).  Labda utaniuliza, ili uokoke, ufanyeje?  Jibu ni rahisi, kwa imani ukitubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, na kumwambia Yesu Kristo akusamehe, utasamehewa sasa hivi, na msamaha wa dhambi, huambatana na wokovu (LUKA 1:77).  Je, uko tayari kuokoka sasa hivi?  Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii kwa dhati toka moyoni, Mungu baba asante kwa kuniletea ujumbe huu.Natubu dhambi zangu zote, kwa kumaanisha kuziacha. Yesu Kristo nakuomba unisamehe dhambi zangu na kunipa uwezo wa kushinda dhambi na kuniokoa kutoka katika mateso ya moto wa milele. Asante, kwa kuniokoa katika Jina la Yesu.  Amen.  Tayari sasa umeokoka, na kwa hakika unakwenda mbinguni sasa, hata ukifa leo.  Ili uzidi kuukulia wokovu, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

       Masomo ya matukio ya mwisho wa Dunia. Unaweza kuingia kwenye link ya kila somo.
1. KUNYAKULIWA KWA KANISA
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/01/02/kunyakuliwa-kwa-kanisa/
2. DHIKI KUBWA
https://davidcarol719.wordpress.com/dhiki-kubwa/
3. TAJI KWA WATAKATIFU NA HARUSI YA MWANAKONDOO
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/02/10/taji-kwa-watakatifu-na-harusi– ya-mwanakondoo/
4. KUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI NA VITA VYA HAR-MAGEDONI
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/02/10/kuja-kwa-yesu-kristo-mara-ya-pili-duniani-na-vita-ya-har-magedoni/
5. MIAKA 1,000 YA UTAWALA WA YESU KRISTO DUNIANI NA VITA VYA GOGU NA MAGOGU
https://davidcarol719.wordpress.com/miaka-1000-ya-utawala-wa-yesu-kristo-duniani-na-vita-vya-gogu-na-magogu/
6. UFUFU WA WAFU
https://davidcarol719.wordpress.com/187-2/
7. JEHANUM YA MOTO
https://davidcarol719.wordpress.com/jehanum-ya-moto/
8. KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE CHA HUKUMU
https://davidcarol719.wordpress.com/?s=KITI+CHA+ENZI+KIKUBWA+CHEUPE+CHA+HUKUMU
9. MBINGU MPYA NA NCHI MPYA
https://davidcarol719.wordpress.com/mbingu-mpya-na-nchi-mpya/

               . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

              Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook, Twitter n.k  kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

              UBARIKIWE SANA KWA KAZI YAKO NJEMA

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s