MCHUNGAJI NA KONDOO

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SIKU YA KUICHAMBUA BIBLIA

 

SOMO:  MCHUNGAJI NA KONDOO

S

iku hii ya leo ya Kuichambua Biblia, tunaendelea kujifunza Kitabu cha YOHANA, katika Biblia zetu.  Leo tunatafakari kwa undani YOHANA 10:11-29.  Katika mistari hii, pamoja na mafundisho mengine, kuna mengi tunayojifunza kuhusu “MCHUNGAJI NA KONDOO“.  Tutayagawa mafundisho tunayoyapta katika mistari hii, katika vipengele vinane:-

(1)      MCHUNGAJI MWEMA YESU KRISTO (MST. 11);

(2)      WAJIBU WA MCHUNGAJI (MST. 12-15);

(3)      WAJIBU WA KONDOO (MST. 26-27);

(4)      MATAIFA, KONDOO WENGINE (MST. 16);

(5)      KUFA KWA YESU KUTOKANA NA MAKUSUDI MAALUM (MST.

       17-18);

(6)      MBONA MNAMSIKILIZA (MST. 19-21);

(7)      HEKIMA YA KUWAJIBU WATU WANAFIKI (MST. 22-25);

(8)      JINSI YA KUFANYA ILI TUSIPOTEE (MST. 27-29).

 

(1)      MCHUNGAJI MWEMA YESU KRISTO (MST. 11)

Yesu Kristo, hapa anajitambulisha kwetu kama Mchungaji mwema anayeutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.  Daudi, kama mchungaji wa kondoo, aliwalinda sana kondoo wake.  Alipokuwa akija simba, au dubu na kumkamaa kondoo, Daudi alimfuata na kumpiga na kumpokonya kinywani mwake, kwa ujasiri mkubwa (1 SAMWELI 17:34-35).  Yesu Kristo, alikuja kwetu kama Mwana wa Daudi (MARKO 10:46-52).  Daudi, alikuwa mfano tu wa Yesu Kristo.    Yesu Kristo, ni Mchungaji mwema kuliko Daudi.  Shetani kama simba aungurumaye, anapotujia na kutukamata na kutaka kutumeza, hatuna haja ya kubabaika, bali tuliitie Jina la Yesu Mchungaji Mwema na Yeye atatuokoa mara moja.  Kama kondoo wa Mchungaji mwema Yesu Kristo, hatupaswi kuogopa mabaya.  Tukiwa na Yeye, na kumtumaini katika maisha yetu, hatutapungukiwa na kitu (ZABURI 23:1-6).  Mchungaji Mwema Yesu Kristo, aliyekuwa tayari hata kuutoa uhai kwa ajili yetu pale msalabani, anatujali sana kututakia mema, kuliko wengi wetu tunavyowaza.  Bwana ampe neema kila mmoja wetu kuifahamu kweli hii (1 PETRO 5:7).

 

(2)      WAJIBU WA MCHUNGAJI (MST. 12-15)

Kila mtu aliyeokoka, amepewa wajibu wa kichungaji, na siyo kazi ya Mchungaji mmoja tu katika Kanisa.  Ishara halisi ya kumpenda Yesu, ni kuzichunga kondoo zake (YOHANA 21:16).  Kiongozi wa Zoni, Kiongozi wa Seksheni, Kiongozi wa Kanisa la Nyumbani, Mwalimu wa Ufuatiliaji, wote hawa wanafanya kazi za kichungaji na hivyo kila mmoja anapaswa kufahamu wajibu wa Mchungaji na kuutekeleza.  Wajibu mmojawapo wa Mchungaji ni KUWATANGULIA KONDOO au kuwa kielelezo kwao (MST.4, 1 TIMOTHEO 4:12).  Mchungaji hapaswi kabisa kufanya lolote ambalo likiigwa na kondoo anaowachunga, litakuwa chukizo kwa Mungu.  Anapaswa kuwatangulia kondoo katika kuwahi Kanisani, kuwa mbali na masengenyo, uongo, na kila namna ya dhambi.  Siyo hilo tu, mambo ya kondoo iwe, ni ugonjwa, msiba n.k., yanapaswa kuwa kitu kwake, na anapaswa kufurahia kujitoa kiwa gharama yoyote katika kuwahudumia kondoo bila kujali malipo, muda n.k., na kuwa tayari hata kuutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo na kujitofautisha na mchungajiwa  mshahara (MST. 12-13).  Anapaswa pia kuwajua kondoo wake na kuwaita kwa MAJINA (MST. 3,14).  Anapokuwa haonekani kondoo mmoja katika ibada, ni wajibu wa Mchungaji kumtafuta (EZEKIELI 34:6-10).  Katika kanisa hili, kazi hizi ni za Walimu wa Ufuatiliaji, Viongozi wa Makanisa ya Nyumbani, Viongozi wa Seksheni, na Viongozi wa Zoni.  Kuna baraka tele katika kutekeleza wajibu huu (1 PETRO 5:2-4).

(3)      WAJIBU WA KONDOO (MST. 26-27)

Watu wote duniani, wametengwa katika makundi mawili.  Wengine wanaitwa MBUZI na wengine KONDOO.  Siku ya mwisho, makundi haya mawili, yatakuwa dhahiri.  Mbuzi watakwenda motoni na kondoo wataingia mbinguni (MATHAYO 25:31-34, 41).  Ni muhimu kwa kila mmoja wetu kujifahamu kwamba yuko kundi lipi.  Tutajuaje kwamba tuko miongoni mwa kondoo?  Jibu ni hili, ni wale wanaoisikia sauti ya Yesu, kisha wakamsadiki na kumfuata.  Tukifahamu kwamba sisi ni kondoo, tunatakiwa pia kufahamu wajibu wetu.  Tunatakiwa kuwa chini ya uongozi wa Mchungaji wetu na kumsikia na kumfuata yeye tu, na kuwakimbia wageni wanaotaka kutupoteza.  Hiyo ndiyo siri ya kushinda (MST. 4-5).

(4)      MATAIFA, KONDOO WENGINE (MST. 16)

“Kondoo wa zizi hili“, ni Waisraeli, (MATHAYO 10:5-6).  Katika mpango wa Mungu, Yesu alikuja kushughulika KWANZA na Waisraeli, hata hivyo hawakumpokea (YOHANA 1:11).  Katika kukamilisha mpango wake, ilimpasa kuwaleta KONDOO WENGINE.  Hawa wengine, ni MATAIFA, watu ambao siyo Waisraeli (pamoja na Watanzania).  Yesu alikuja akafa siyo kwa ajili ya Waisraeli tu kama wengisne wasiojua wanavyosema, bali kwa ajili ya ulimwengu mzima (YOHANA 3:16; 11:49-52).

(5)      KUFA KWA YESU KUTOKANA NA MAKUSUDI MAALUM (MST. 17-18)

Yesu Kristo alikufa kutokana na kupenda kwake.  Ilikuwa ni mpango wa Mungu kwetu.  Hakufa kwa bahati mbaya, au katika hali ya kifo cha kawaida ya wanadamu, kwa sababu alitabiri mapema juu ya kufa na kufufuka kwake, na ikawa hivyo (MARKO 8:31; 9:31; 10:32-34).  Hakika alikufa kwa ajili yetu ili ghadhabu ya Mungu iwe mbali nasi (WARUMI 5:8-11).

(6)      MBONA MNAMSIKILIZA (MST. 19-21)

Shetani hapendi kabisa kuwaona watu wanamsikiliza Mhubiri yeyote anyefundisha kweli ya Neno la Mungu.  Atafanya kila namna kuwazuia watu kumsikiliza, kwa kuwaletea kila namna ya uzushi kwamba Mhubiri huyo ni pepo, ana wazimu, ni nabii wa uongo n.k.  Alifanya hivyo kwa Yesu kwa kuwa aliifundisha Kweli (LUKA 20:21).  Tunapaswa kuzifahamu fikra hizi za shetani na kupuuza uzushi wake ili tupate kumshinda, na kuendelea kuisikia kweli ili ituweke huru (2 WAKORINTHO 2:11; YOHANA 8:31-32).

(7)      HEKIMA YA KUWAJIBU WATU WANAFIKI (MST. 22-25)

Sikukuu ya Kutabaruku, ni sikukuu iliyokuwa inaadhimisha jinsi YUDA MAKABAYO alivyolisafisha hekalu baada ya wapagani kuliteka nyara na kulinajisi.  Watu waliandamalna, huku wakichukua matawi mabichi ya miti na ya mitende.  Wakati kama huu, ndipo wanafiki Wayahudi walipomzunguka Yesu na kumtaka awaambie waziwazi kama Yeye ni Kristo, na kuacha kuwaambia kwa mithali au mafumbo.  Nia yao ilikuwa kwamba akitamka tu, basi wapate njia ya kumshitaki kwamba amesema yeye ni “Mfalme“ wa Wayahudi, ili auawe.  Yesu aliwajibu “NALIWAAMBIA“, ila hakutaja vile walivyotaka ataje.  Hiyo ni hekima ya kuwajibu watu wanafiki ambao wana nia mbaya katika kuuliza maswali yao.  Tunapaswa kuangalia jinsi ya kuwajibu ili tusiwape faida na malengo yao yakatimia.

(8)      JINSI YA KUFANYA ILI TUSIPOTEE (MST. 27-29)

Ahadi ya Yesu Kristo kwa kila mmoja anayemwokoa, ni kwamba hatapotea kamwe wala hakuna mtu awezaye kumpokonya katika mkono wa Baba yake.  Hata hivyo tuna sehemu yetu ya kufanya, ili jambo hili lipate kutimia.  Inatubidi kuisikia sauti yake Yesu katika Neno lake na kumfuata.  Tukifanya hivyo hatuwezi kupotea.  Tukiwasikia wazazi wetu, wakwe zetu, marafiki zetu, au wanadamu wengineo na kuacha kulisikia Neno la  Mungu na kulifuata, tujue tutapotea milele na milele.  Hatupaswi kuusikiliza uongo wa Shetani anaposema “tumepotea“ kwa kuokoka na kulifuata Neno la Kristo.  Ni kinyume chake kabisa.

…………………………………………………………………………………………………………………………………..

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “somo” hili, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe..

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s