MFANO WA MAGUGU

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.o

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobemini

 Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SIKU YA KUICHAMBUA BIBLIA.

SOMO:      MFANO WA MAGUGU (MATHAYO 13:24-30, 36-43)

Katika MATHAYO 13:24-49, tunapata mfululizo wa mifano inayotufundisha mengi kuhusu Ufalme wa Mbinguni.  Mfano wa Magugu ni mmoja kati ya mifano saba katika mistari hii.

1.         MAANA YA MAGUGU

Nyakati za Biblia, kulikuwa na mmea uliojulikana kwa lugha ya Kiyunani “ZIZANIA“ na katika Kiswahili unaitwa hapa “GUGU“.  Mmea huu tangu ulipoota na kuendelea kukua, ulifanana sana na ngano kwa kila hali – umbile, rangi n.k.; na ilikuwa vigumu sana kuutofautisha na ngano.  Hata hivyo mmea huu ulipokomaa na kutoa matunda ndipo ulipojidhihirisha kuwa ulikuwa “ZIZANIA“ au GUGU.  Masuke yake yalikuwa marefu zaidi kuliko masuke ya ngano halisi na mbegu zake zilikuwa NYEUSI tofauti na zile NYEUPE za ngano na zilikuwa ni SUMU kali.  Ilikuwa ni kawaida katika Nchi za Biblia adui kupanda magugu ya namna hii au mimea mingine yenye sumu katika mashamba ya wale anaowachukia.

Magugu katika mfano huu ni Wana wa yule mwovu (MST.38) ambao wanaweza kuonekana kama wana wa Mungu katika kusema “Bwana Asifiwe“, kushika Biblia na kwenda Kanisani, kufanya maombi na kutoa sadaka, kuimba na kupenda pambio na kwaya, na hata mavazi n.k.  Wanakuwa kama wana wa Mungu huku matunda yao ni MEUSI na yenye SUMU kali (EZEKIELI 33:31; ZABURI 78:35-37; MARKO 7:6; MATHAYO 7:21; 2 WAKORINTHO 11:13-15; TITO 1:6).  Ni wenye machukizo na watendao maasi (MST. 41).

2.         MAANA YA KUTENDA MAASI (MST. 41)

Kutenda uasi au maasi ni kama dhambi ya uchawi na ukafiri na vinyago (kuabudu sanamu) 1 SAMWELI 15:23.  Kutenda uasi ni:-

(a)  Kukataa kuongozwa na Neno la Mungu na kulitenda (HESABU 27:14; 1 WAFALME 13:21-22; ZABURI 107:11; WARUMI 2:21-23).  Kuasi ni kumvunjia Mungu Heshima.  Uasi ni dhambi (1 YOHANA 3:4).

(b)  Kukataa mpango wa Mungu (WARUMI 5:19);

(c)   Kuichukia nuru (AYUBU 24:13; YOHANA 3:20-21);

(d)  Kuzikataa amri za Bwana na kutaka kuwa huru mbali na haki (KUMBUKUMBU LA TORATI 1:43; WARUMI 6:20).  Uhuru wetu katika Ukristo ni uhuru mbali na dhambi (WARUMI 6:22).  Uhuru wowote mbali na haki ni uasi.

(e)   Kutowatii wenye mamlaka ni uasi na ni kushindana na Agizo la Mungu (WARUMI 13:2).  Kazi yoyote au Agizo lolote JEMA tunalopewa na wenye mamlaka ni lazima tulitii (TITO 3:1).

 

3.         MWISHO WA MAGUGU

Mwisho wa magugu yaani wale watendao uasi na machukizo ni kutupwa katika moto wa milele (MST. 42).

 

4.         ADUI NDIYE ALIYETENDA HIVI   (MST. 28)

Adui yetu ni Ibilisi (MST. 39), (LUKA 10:19; MARKO 13:10)

5.         KAZI ZA ADUI IBILISI  (MST.28)

(a)       KUPEPETA KAMA NGANO  (LUKA 22:31)

  • Kupepeta ni kutenganisha chakula halisi na uchafu.  Adui hutaka kutuondolea vitu vizuri na kutuachia vichafu.

(b)              KUCHINJA NA KUHARIBU  (YOHANA 10:10)

(c)               KUHARIBU FIKRA   (2 WAKORINTHO 11:3)

(d)              KUDANGANYA  (UFUNUO 20:10; 1 WAFALME 22:20-22; KUMBUKUMBU LA TORATI 11:16; YAKOBO 1:14)

(e)               KUTEGA (2 TIMOTHEO 2:26);  Tukeshe na kuwa macho kuiangalia mitego yote ya Shetani (MITHALI 1:17); Tumwombe Mungu kila siku atuokoe na mitego ya Ibilisi (ZABURI 141:9; ZABURI 91:3)

(f)                KUZUIA (1 THESALONIKE 2:18)

(g)              KUSHTAKI (UFUNUO 12:10)

(h)              KUMFANYA MTU ASIIFANYE KAZI YA MUNGU (MATHAYO 16:21-23)

(i)                KUIBA (YOHANA 10:10).

Shika sana ulicho nacho kama unacho.  Kama huna kitafute (UFUNUO 3:11,17-20).  Mpinge shetani naye atakimbia (YAKOBO 4:7).  Dumu kuwa Ngano, dumu kuwa miongoni mwa wana wa Ufalme, utang’aa kama jua katika Ufalme wa Baba yako.

MWENYE MASIKIO NA ASIKIE  (MATHAYO 13:38-43)

Usikose faida zilizomo katika somo la kwanza “MFANO WA YESU” katika  link hii https://davidcarol719.wordpress.com/mfano-wa-yesu/

                  Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.. 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s