MIFANO YA YESU

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SIKU YA KUICHAMBUA BIBLIA.

SOMO:      MIFANO YA YESU

Sura ya 13 ya Kitabu cha MATHAYO, ni SURA YA MIFANO.  Yesu Kristo anazungumza mambo mengi kwa mifano (MST. 3).  Wanafunzi wa Yesu walimwuliza Yesu kwa nini alikuwa anazungumza na watu kwa mifano (MST. 10).  Sisi nasi ni muhimu kufahamu kwa nini Yesu alikuwa akizungumza na watu kwa mifano:-

(1)              Mifano inafanya watu waweze kuzijua siri za Ufalme wa Mungu au kweli ya Neno la Mungu iliyofichika kwa kulinganisha mambo yasiyoeleweka ya Ufalme wa Mungu kwa mambo yanayoeleweka ya duniani (MATHAYO 13:10-11; MARKO 4:20);

(2)              Mifano inatumika kuwafanya wale wasioipenda kweli ya Neno la Mungu kuzidishiwa kuifahamu kweli yote ya Neno la Mungu (MST. 12);

(3)              Mifano inatumika kuwafanya wale wasioipenda kweli ya Neno la Mungu, kunyang’anywa hata kile walicho nacho (MST. 12);

(4)              Mifano inaifunua kweli kwa namna inayowavutia wasikilizaji na kuwafanya wawe na hamu zaidi ya kusikia (MST. 10-11, 15);

(5)              Mifano inatumika kumkemea, kumuonya mtu na kumpa maelekezo au mafundisho ya kweli ya Neno la Mungu bila yeye, kuchukia, kuudhika, kuumia moyoni au kukwazwa mpaka anashtukia kwamba tayari kweli hiyo imemmeza (2 SAMWELI 12:1-12).

MUHIMU KUFAHAMU: Mifano haitupi kibali cha kuzungumza uongo.  Mifano yote Yesu aliyoitumia kuhusu watu fulani, ni mifano ya kweli (LUKA 15:11-32; LUKA 16:19-31; LUKA 18:1-5) na pia alizungumzia vitu vilivyopo na mambo yaliyokuwa yanatendeka waziwazi katikati ya watu.  Hatupaswi kutumia mifano kwa lengo la kutafuta kuwachekesha watu tu hata kwa kutafuta hadithi za uongo.  Yesu hakufanya hivi. Ili kuelewa mifano ya Yesu, ni muhimu kufahamu mazingira ya tukio alilokuwa akilizungumzia, historia iliyotangulia kabla ya tukio hilo, na desturi au mambo yanayohusiana na watu aliokuwa akiwaambia mifano hiyo.  Kwa mfano akitumia neno “TAA ZA WANAWALI”, ni muhimu kufahamu taa za wakati huo kwa Wayahudi zilikuwaje.  Hazikuwa taa za Umeme n.k.

MFANO WA MPANZI – (MATHAYO 13:3-9; 18-23)

Ili tuweze kuzaa matunda mengi kutokana na mbegu ya Neno la Mungu inayopandwa kwetu, inatupasa tuwe na sifa za udongo mzuri.  Udongo mzuri ni LAINI, UNALIMIKA na kuweza kutiwa MBOLEA, unakuwa na MAJI ya kutosha na hata Jua likiwaka, mimea haiwezi kukauka.  Udongo mzuri pia unapokea maji kwa urahisi na kuyatunza:-

(1)  NI MUHIMU KUWA TAYARI KULISIKIA NENO TUKIWA NA NIA YA KULITENDA NA SIYO NIA YA KULISAHIHISHAEZEKIELI 33:30-32; ZABURI 73:22, 24; 1 WAKORINTHO 8:2

(2)  KUWA MBALI NA HALI YA UKAIDI (UGUMU) WA KUTOKUWA TAYARI KUBADILISHWA NA NENO LA MUNGU   – YEREMIA 44:15-17; 1 SAMWELI 8:19-20; 2 NYAKATI 24:19; ZEKARIA 7:11-12; MATENDO 7:51.

(3)  KUWA MBALI NA HALI YA KULIDHARAU NENO LA MUNGU NA KUTOKUWA TAYARI KULITII  – MITHALI 13:13; ZABURI 119:9; MATENDO 3:19; MATENDO 5:29.

(4)  KUTOKUYATUPA MANENO YOYOTE YA MUNGU YANAYOPANDWA KWETU  – YEREMIA 36:21-23; MARKO 7:5, 8-9,13.

(5)  KUWA TAYARI KULITENDA NENO LA MUNGU HATA KAMA LINAAMBATANA NA DHIKI AU UDHIA  – MATENDO 14:21-22; MATHAYO 13:20-21.

(6)  KUTORUHUSU KUSONGWA NA LOLOTE AMBALO LINATUFANYA TUWE MBALI NA MAPENZI YA MUNGU  – MATHAYO 13:22; 1 WAFALME 20:39-40;

(7)  KULISOMA NA KULITAFAKARI NENO TULILOSIKIA TENA NA TENA  – UFUNUO 1:3; 1 TIMOTHEO 413; WAKOLOSAI 4:16; YOSHUA 1:8.

(8)  KUMWOMBA MUNGU KWA BIDII ILI AT

UWEZESHE KULIELEWA NENO NA KULITENDA BAADA YA KULISIKIA  – ZABURI 119:34; DANIELI 9:2-3.

Usikose faida zilizomo katika somo hili linalofuata (MFANO WA MAGUGU) katika link hii, https://davidcarol719.wordpress.com/wp-admin/post.php?post=336&action=edit

…………………………………………………………………………………………………………………………………..

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe..

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s