MOYO ULIOGAWANYIKA

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

 

SOMO:  MOYO ULIOGAWANYIKA

     Ni muhimu kufahamu kuwa mtu anapookoka anapewa uwezo wa kushinda dhambi.( YOHANA 1:12 ) “ Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake”. ( WARUMI 1:16 ) “Kwa maana siionei haya injili, kwa sababu ni uweza wa Mungu uletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia”. ( WAKOLOSAI 1:10-11 ), “Mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema na kuzidi katika maarifa ya Mungu; mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na faraja”.

Tunawezaje kuishi maisha yanayompendeza Mungu na kuwa na matunda? Jibu ni kwamba tunawezeshwa na Mungu mwenyewe.

     Mtu aliyeokoka hawezi kutenda dhambi na ndani yake anaumbi, na huyo ndiye anayepewa kuushinda ulimwengu. Yesu Kristo aliushinda ulimwengu kwa kwa sababu alikuwa mtoto wa Mungu . ( 1 YOHANA 5:3 )

“Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda  kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu”. ( WAEFESO 2:1-2 ),Ninyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zeni ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi”.Mtu aliyeokoka haishi kwa kawaida ya ulimwengu huu. Hawezi kuzifuata fasheni za ulimwengu huu. Dunia nzima itachukuliwa na ulimwengu lakini atakuwepo Nuhu au Ruthu wa kusema hapana ( LUKA 17:26-37 ). Tunaishi sikuza mwisho ndiyo maana tunaona upendo wa kwanza  wa kumpenda Yesu na kuyatii maagizo yake yote, haupo leo kwa waliowengi. Maasi yameongezeka siku hizi za mwisho ( MATHAYO 24:12 ),’Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa”.

Mtu mwenye dhambi katika ulimwengu war oho anakuwa ameukalia usukani wake mwenyewe. Akitaka kwenda kwenye pombe, uasherati, wizi n.k anaenda. Ili apokee uwezo wa kushinda dhambi ni lazima ampokee Bwana Yesu, yaani amkaribishe ndani ya moyo wake. Kwa kufanya hivyo, Yesu Kristo anashika usukani wa moyo wake Yesu sasa hatampeleka kule alikokuwa akienda kutenda dhambi.

                                      ( WALAWI 26:13 )

“Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu niliyewaleta mtoke katika nchi ya Misri, ili msiwe watumwa wao; nami nimeivunja miti ya kongwa lenu, nikawaendesha mwende sawasawa”.

Awaye yote ambaye ni mwenye dhambi ni mtumwa wa dhambi kwa namna ileile ya utumwa wa Waisraeli Misri.

Ni muhimu kufahamu kuwa, si kila mtu anayeongozwa sala ya toba anayempokea Yesu ( Wokovu ) (WAGALATIA 6:7 )”Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna”. Ndani ya moyo wa mtu kuna vyombo kwa namna ileile ya nyumba. Yesu anataka tumfungulie milango ya vyumba vyote siyo kuja mbele zake  kuomba toba  na huku tukiwa na nia ya kutoacha baadhi ya dhambi.  Moyo wa mtu kama huyo unakuwa umegawanyika. ( HOSEA 10:2 ), “Moyo wao umegawanyika; sasa wataonekana kuwa na hatia; yeye anazipiga madhabahu zao, ataziharibu  nguzo zao”.Mungu wetu hawakubali watu ambao mioyoyao iegawanyika. Watu wasiotaka kumfungulia Yesu Kristo vyumba vyote. Watu wanaotaka kutubu baadhi ya dhambi na kuziacha zingine. Watu ambao wanakuja mbele zake kutaka toba lakini moyoni wakijua kuwa hawatayatendea kazi maagizo yake yote ( ZABURI 119:6 ).

      Mungu anapendezwa na mtu anayemrudia yeye kwa moyo wote. Mtu yule ambaye ana utayari wa kuyatendea kazi maagizo yote ya Mungu au ambaye yuko tayari kumfungulia Yesu Kristo vyumba vyote, huyo anapokea msamaha au toba ya kweli. Mtu wa namna hii ndiye atakayepewa msamaha wa dhambi zote ambao utaambatana na uwezo wa kushinda dhambi ( 1 WAFALME 8:46-50 ). Wokovu unakuja baada ya kusamehewa dhambi ( LUKA 1:77 ), “ Uwajulishe watu wake wokovu, Katika kusamehewa dhambi zao”.  Yuda alitubu lakini aliendelea kutenda dhambi kwa sababu alitubu kwa unafiki. Mtu akitubu kwa unafiki hawezi kupokea Wokovu wa kweli (YEREMIA 3:8,10). Watu wanataka wapate wokovu kwa viwango vyao wenyewe

     Mungu anasema kuwa anatujaribu kuona kama tunampenda kwa mioyo yetu yote( KUMBUKUMBU LA TORATI 13:3 ). Pia anataka tumtafute kwa ioyo yetu yote ( YEREMIA 29:12-13 ). Hatuwezi kumwona Mungu maishani mwetu kama hatutamfungulia vyumba vyote katika mioyo yetu ili atuendeshe mwenyewe.

      Shetani anajua kuwa vuguvugu watatapikwa siku ya mwisho Anafahamu kuwa vuguvugu hataingia mbinguni. Kama wewe ni vuguvugu kaa mkao wa kwenda motoni. Ndiyo maana shetani anataka watu waendelee kuishi kinyume na Neno la Mungu kwa kusuka nywele, kuvalia mapambo, nywele za bandia, wakipaka wanja, wanawake kuvaa suruali, nguza za kubana makalio kwa wanawake, kimini, nguo zinazoacha matiti nje, transparent (nguo zinazoonesha nguo tulizovaa ndani) n.k. Mtu yeyote anayevaa mavazi haya ni Vuguvugu. Yesu anakushauri kuwa moto au baridi ili ujulikane waziwazi wewe niwa upande upi ( UFUNUO 3:13-16 ). Wana wa Israeli kwa wingi wao wote waliotoka Misri waliangamizwa Jangwani isipokuwa Yoshua na Kalebo tu. Mungu hakuwaangamiza kwa sababu walimwandama Bwana kwa mioyo yao yote ( HESABU 14:22-24; KUMBUKUMBU LA TORATI 1:35-39 ). Wote waliokuwa na nia mbiliwaliangamizwa. Mungu hapendezwi na Mtu anayetaka kuingia Kanaani wakati huohuo akitamani mambo ya Misri alikotoka. Ukiamua kuingia katika utakatifu ingia kweli kweli. Utakatifu ni mwili na roho ( 2 WAKORINTHO 7:1; 1WAKORINTHO 7:34; MATHAYO 23:25-26 1 WATHESALONIKE 5:23 ).

       Je, unataka kumpa Yesu maisha yako? Ukiamini kwa moyo wako wote itawezekana kabisa ( MATENDO 8:35-37 ). Fatisha sala hii ya toba sasa.

Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

                                     . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

                                          UBARIKIWE NA BWANA YESU!!!

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s