NEEMA JUU YA NEEMA

ZACHARY KAKOBE

Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SOMO: NEEMA JUU YA NEEMA.

                ( YOHANA 1:16-17 )

Ni vigumu mno mtu aliyeokoka kuendelea na kudumu katika wokovu bila kutetereka, kama hajui kitu kuhusu somo hili. Kwa sababubu hii, kila mmoja wetu anapaswa kujifunza somo hili kwa moyo wote, na kulitunza moyoni mwake ilin awe miongoni mwa washindao. Tutaligawa somo hili katika vipengele vitatu:-

                   (1). UMUHIMU WA MAFUNDISHO KUHUSU NEEMA.

                   (2). MAANA YA NEEMA.

                   (3). NEEMA KATIKA MPANGO WA MUNGU.

(1)    UMUHIMU WA MAFUNDISHO KUHUSU NEEMA..

Watu waliookoka katika kanisa la kwanza walikuwa waaminifu kuishika imani hata ikibidi kufa; kwa sababu walijifunza tena na tena kuhusu somo hili la Neema. Epafra Mtume aliwafundisha watu wa kanisa la Wakolosai kuhusu Neema kwa msisitizo mkubwa (WAKOLOSAI 1:3-7). Paulo na Barnaba waliwatia watu moyo wadumu katika Neema ya Mungu (MATENDO 13:43). Sisi nasi tunapaswa kudumu katika  neema ya Mungu, Sasa basi tutawezaje kufanya hivyo ikiwa hatujui hata maana ya kitu hiki  cha thamani kubwa, “Neema ya Mungu”? ingawa tu warithi wa kitu hiki chenye thamani lakini tutakuwa kama watoto kama hatujui maana ya Neema (WAGALATIA 4:1).

(2).   MAANA YA NEEMA.

Nini basi maana ya neema? Watu wengi wamekuwa wakiimba ,”Neema, neema imefunuliwa” na kukariri na kuisema Neema ya Bwana (2 WAKORINTHO 13:14) kama Kasuku huku hawajui wayasemayo. Nini basi maana ya  neema?

 1. Neema, ni upendeleo wa kuchaguliwa, bila kustahili kutokana na matendo yoyote aliyoyafanya mtu au  sifa aliyonayo mtu.
 2. Neema pia, ni uwezo wa kushinda katika tabia na utumishi wa Mungu sawasawa na mapenzi yake, tunaopewa na Mungu bila gharama yoyote au nguvuzetu au kufanyia kazi yoyote.
 3. 1.      Upendeleo wa kuchaguliwa bila kustahili- Kutokana na matendo yake, hakuna mwanadamu yeyote mwenye haki mbele za  Mungu (WARUMI 3:20). Tangu kabisa  amekuwa akimhuzunisha Mungu (MWANZO 6:5-7). Wakati wa Nuhu, watu waliangamizwa kwa Gharika. Wakati wa Musa, Mungu alitaka pia kufuta  kabisa kizazi  cha Wausraeli na kubaki na Musa tu kama siyo maombi ya Musa (HESABU 14:11-20). Wakati wote, wanadamu wote wamepotoka na kuoza (WARUMI 3:12). Ni Yesu peke  yake tu ambaye siku zote alifanya yanayompendeza Mungu (YOHANA8:29).Alijaribiwa sawasawa na sisi lakini hakutenda dhambi (WAEBRANIA  4:14-15). Yesu huyu anayempendeza Mungu ndiye aliyekufa msalabani na Baraba aliyekuwa mhalifu mkubwa akafunguliwa. Kama Baraba alivyofunguliwa pamoja na ukosaji wake, kila mwanadamu amefunguliwa, akiamini tu. Mbele za Mungu kila mtu amepimwa na kuonekana amepungua (DANIELI 5:27). Sasa kwa kuamini tu kwamba Yesu alizichukua dhambi zetu pale msalabani, sisi tunaokolewa. Watu wengi hawaokolewi kwa  sababu  hawajui tunaokolewa kwa neema tu kwa njia ya imani peke yake (WAEFESO 2:5). Kazi aliyoifanya Yesu msalabani imetupa kuirithi mbingu aliyokwenda  bila sisi kuifanya. Ni kama ambavyo bondia anavyopigana ulingoni kwa shida kubwa na kasha akishinda na kupewa mamilioni ya fedha,  mke wake aliyebaki nyumbani bila kupigana naye atakuwa milionea. Hii ndiyo neema.
 4. 2.      Uwezo wa kushinda bila kutumia nguvu zetu- Neema ni uwezo wa kushinda dhambi na kumtumikia Mungu apendavyo. Neema ndiyo inayotufundisha (inayotuwezesha) kukataa ubaya na tama za kidunia na kuishi kwa kiasi na haki na utakatifu (TITO 2:11-12; WAGALATIA 2:8). Maisha ya wokovu siyo ya kutumia nguvu zetu au kujitahidi. Uweza wa Mungu unatimilika kwetu katika udhaifu wetu yaani kutokuweza kwetu. Hatupaswi kujitumainia wenyewe katika kufanya lolote  (2 WAKORINTHO 1:8-9).

(3). NEEMA KATIKA MPANGO WA MUNGU.

         Sheria ya Kristo, ni sheria ngumu kuliko sheria ya Musa (MATHAYO 5:27-28, 38-41, 43-44). Ingawa Yesu amekuja kwetu na sheria ngumu zaidi kuliko ya Musa hata hivyo, tofauti yake ni kwamba kwa Musa hakukuwa na msaada wowote wa mtu kuifanya sheria lakini Yesu amekuja  na msaada unaoitwa Neema (YOHANA 1:16-17). Hivyo tumepata siyo tu neema ya kuokolewa ila neema pia ya kutuwezesha kudumu katika wokovu. Ni neema juu ya neema..Mafunuo ya mtume Paulo  katika WARUMI 7:1-4 yanatufananisha na mwanamke aliyeshindwa viwano vya usafi vya mumewe, na hatimaye akatokea mwanamume mwenye viango vya usafi vya juu zaidi; lakini pamoja na msaada wa kumwezesha kuvimudu. Mwanamke huyu asingeweza kuolewa na mume huyu mpya mpaka  kwanza afe, au yeye afe, afufuke na kuva huru kuolewa na mwingine. Yote haya aliyafanya Yesu kwa niaba yetu na kasha akatuoa. Viwango vyake vya usafi ni vya juu sana, hata hivyo ametupa neema  ambayo ni sawa na wasaidizi wengi wa kazi nyumbani wa kike na wa kiume. Hivyo tukikosa uwezo wowote wa kufanya mapenzi yoyote ya Mungu, tunachotakiwa kufanya ni kukikaribia kiti cha neema cha Yesu na kuomba neema tunayoihitaji kuyafanya mapenzi yake (WAEBRANIA 4:16). Watu wengi wanashindwa kufanya wanayopaswa  kwa kuwa hawatumi fomu za maombi ya neema kwa Yesu.

Ili kukamilika katika kila tabia ya Kristo na kuitenda kazi kama Kristo, tunahitaji neema. Kwa muhtasari, ebu tuangalie  zaidi kuhusu neema katika mpango wa Mungu kwetu:-

 1. Yesu alipopaa alikupa neema ya kufanya kila jambo (WAEFESO 4:7-8).
 2. 2.      Tunaweza tu kuwa wakristo hodari  kwa kutumainia neema ya Mungu kwa utimilifu, na siyo jitihada zote (2TIMOTHEO 2:1; 1PETRO 1:13).
 3. 3.      Watakatifu walio vielelezo vyetu katika Biblia walifanya hayo kutokana na neema ya Mungu waliyoitumainia kwa utimilifu (2WAKORINTHO  1:12; 1WAKORINTHO 15:10).
 4. 4.      Kanisa la kwanza walitajirika katika Yesu,  kwa neema katika maneno yote na maarifa yote na karama zote (1WAKORINTHO 1:4-7).
 5. Hata katika kumtolea Mungu inahitaji neema ya Mungu, kinyume cha hapo utatoa huku ukilalamika (2WAKORINTHO 8:1-3).
 6. Katika uimbaji inahitajika neema (WAKOLOSAI 3;16).
 7. 7.      Katika mazungumzo ya wakati wote, mkristo anahitaji neema kuzungumza yale tu yanayompendeza Mungu (WAKOLOSAI 4:6).
 8. Kila tabia  na utumishi wa Kristo unategemea neema (2WAKORINTHO 8:1-2, 8)
 9. Hatuwezi kuwa watumishi wa Mungu tunaoweza kutenda kazi ya Mungu kipekee bila neema ya Mungu (MATENDO 15:40).
 10. Ni neema tu inayoweza kutusimamisha katika kweli ya Neno la Mungu. Bila hiyo, tutaikimbia Kweli (WARUMI 16:24-25; 1PETRO 5:12). Yesu pekee ndiye anayefanya ndani yetu yale yampendezayo mbele zake tunapomwomba neema (WAEBRANIA13:20-21).
 11. 11.  Hatupaswi kuipungukia neema ya Mungu na kuacha kuitumia (WAEBRANIA 12:14-17).
 1. 12.  Ni wale tu waliopokea wingi wa neema siku hadi siku watakaotawala pamoja na Kristo, siyo wale wanaojitumainia nafsi zao, Mungu huwapinga wale wajikuzao na kuona wanaweza kufanya wenyewe (WARUMI 5:17; YAKOBO 4:6).

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!.

                                     . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

                                                          . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .         

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

                                                         UBARIKIWE NA BWANA YESU!!!

Advertisements

One comment on “NEEMA JUU YA NEEMA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s