PIGA KELELE, USIACHE KUHUBIRI

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SOMO LA 7:  PIGA KELELE, USIACHE KUHUB

NENO LA MSINGI:

ISAYA 58:1

“PIGA KELELE, USIACHE, paza sauti yako kama tarumbeta; UWAHUBIRI Watu wangu kosa lao, na nyumba ya Yakobo dhambi zao.”

<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><>< 

B

aada ya mtu kusikia Injili na kukata shauri kutubu dhambi zake na kuokolewa, wajibu alio nao kila siku baada ya hapo ni kuwahubiri wengine juu ya dhambi zao, na kuwaeleza kwamba mshahara wa dhambi ni mauti [WARUMI 6:23].  Tunapaswa kupaza sauti na kueleza jinsi Mungu alivyomleta Yesu Kristo kwa kuupenda ulimwengu ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.  Mtu aliyeokoka ambaye hawashuhudii au kuwahubiri wengine juu ya dhambi zao, ANAKUWA NA HATIA MBELE ZA MUNGU na GHADHABU YA MUNGU ITAMJIA.  Angalia maandiko:-

2 MAMBO YA NYAKATI 19:10:

“Na kila mara watakapowajia na teto ndugu zenu wakaao mijini mwao, kati ya damu na damu, kati ya torati na amri, sheria na hukumu, MTAWAONYA, wasiingie hatiani mbele za BWANA, mkajiliwa na ghadhabu NINYI na ndugu zenu; FANYENI HAYA WALA HAMTAKUWA NA HATIA.”

 

Kutokuhubiri na kuamua kukaa kimya ni kuingia katika hatia.  Tunapaswa kupiga kelele wala tusiache kuhubiri na kuwaeleza watu dhambi zao na msamaha wa dhambi ulio katika damu ya Yesu iliyomwagika msalabani.  Tusipowaonya watu ili waokolewe, damu yao itatakwa juu yetu.

EZEKIELI 3:18:

“Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; WEWE USIMPE MAONYO, WALA HUSEMI NA HUYO MTU MBAYA ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake, LAKINI DAMU YAKE NITAITAKA MKONONI MWAKO.”

Tutaweza kupendwa na Mungu na kuziokoa roho zetu pale tu tutakapofanya maisha yetu kuwa ya kuwahubiri wengine.  Tukiwahubiri halafu wao wakawa hawataki kuziacha dhambi zao, hapo tutakuwa tumejisalimisha nafsi zetu.  [SOMA EZEKIELI 3:19, EZEKIELI 33:9].

 

SIFA TATU ZA MTU ALIYEOKOKA ASIYEWAHUBIRIA WENGINE JUU YA WOKOVU ALIOUPOKEA

1.         MTU HUYU NI MCHOYO:

Bado kuna nafasi kubwa mbinguni kwa ajili ya watu wanaotaka kuingia katika karamu ya Mwana Kondoo.  Mungu anataka nafasi ipate kujaa na anataka tuwaalike watu wengi [LUKA 14:16, 23].  Tunapokataa kuwaalika watu zaidi kwa kuwahubiri Injili, tendo hilo linamaanisha kwamba; tunataka tuile karamu peke yetu.  Huo ni uchoyo, na wachoyo hawataingia mbinguni.  Kila mmoja aliye katika utakatifu, hapaswi kutafuta faida yake mwenyewe tu, bali ya wenzake [SOMA 1 WAKORINTHO 10:24; WAFILIPI 2:4].  Biblia inasema “Mwenye haki hutoa wala hanyimi” [SOMA MITHALI 21:26].  Hatupaswi kuwa na choyo na kung’ang’ania chakula chote na kuwasahau wengine.

2.         MTU HUYU NI MLEGEVU, NA MZEMBE ASIYEJALI WENZIE:

Unapomshuhudia au kumhubiri mtu na akaokoka, ilivyo ni kwamba unakuwa umemnyakua katika moto wa milele [SOMA YUDA 1:22-23].  Mtu asiyewashuhudia Injili wengine, amefananishwa na mtu mwenye gari la zimamoto na vifaa vyote vya kuwaokoa watu kutoka motoni, ambaye baada ya kupata taarifa kwamba watu wanaungua moto mahali fulani na kuombwa afanye haraka kwenda kuwasaidia, alipuuza na kuegesha gari lake la zima moto kwenye hoteli, na kuanza kunywa soda na kucheza karata huku akichekelea.  Mtu huyu ni mzembe na mwuaji.  Mwenye haki hatafanya hivyo.  Hatupaswi kuwa walegevu katika kuifanya kazi ya BWANA.  Biblia inasema “Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya BWANA kwa ulegevu”  [SOMA YEREMIA 48:10].  Hatupaswi kutowajali wengine kama ilivyo katika MATHAYO 22:5.

3.         MTU HUYU HATAKI KUMSAIDIA BWANA ILA AMEAMUA KUSHINDANA NAYE

Kuwaleta watu kwa Yesu, ni kumsaidia Mungu katika kazi aliyoianzisha Mungu mwenyewe kuifanya, alipokuja ulimwenguni katika nafsi ya Mwana wa Mungu.  Ni neema ya ajabu kwamba tunamsaidia BWANA wetu tunapohubiri.  Wakati wa Musa na Haruni, Mungu alimwambia Musa kwamba Haruni ndiye atakayekuwa msemaji wake kwa watu na mfano wa kinywa chake na Musa atakuwa mfano wa Mungu wa Haruni [KUTOKA 4:16].  Baada ya Yesu Kristo kuhubiri mwenyewe kwa kinywa chake duniani na kupaa mbinguni na kutuachia kazi hiyo, mtu aliyeokoka ndiye msemaji wa Yesu kwa watu na mfano wa kinywa cha Mungu.  Mtu aliyeokoka akiamua kufumba kinywa na asishuhudie Injili, basi anachokifanya ni kwamba hataki ujumbe wa Mungu na hataki kumsaidia BWANA wake kuifanya kazi kwa kutumia kinywa hicho kuhubiri.  Matokeo yake ni nini?  Mtu asiyetaka kumsaidia BWANA, yuko chini ya laana.

            WAAMUZI 5:23:

“Ulaanini Merozi, alisema malaika wa BWANA, walaanini kwa uchungu wenyeji wetu, kwa maana hawakuja kumsaidia BWANA, juu ya hao wenye nguvu.”

Wenye nguvu, ni hao majeshi ya Wafalme wa giza ambao wanawatumikisha ndugu zetu katika dhambi.  Kwa Injili tu ndipo watu haawa wanapokuwa huru mbali na utumwa wa dhambi.

KUHUBIRI NI KAZI YA WATU WOTE WALIOOKOKA:

Kuhubiri siyo kazi ya Mchungaji pekee au Mwinjilisti fulani, wote tumeambiwa twende kuhubiri Injili kwa kila kiumbe [MATHAYO 28:19; MARKO 16:15].  Wote tunapaswa kila siku kuwa vitani, na kumsaidia BWANA juu ya hao wenye nguvu na kuwanyang’anya watu wa BWANA.  Hatupaswi kuketi na kuacha kwenda vitani.

            HESABU 32:6:

“Musa akawaambia wana wa Gadi na wana wa Reubeni, Je!  ndugu zenu waende vitani nanyi mtaketi hapa?”

Jambo la kukumbuka ni kwamba, wale tunaowapata katika Injili inatubidi tuwaongoze katika makanisa ya nyumbani na Kanisa Kuu ili waweze kuukulia wokovu, au siyo kazi yetu itakuwa haina faida; maana watajaribiwa na mjaribu na kuiacha imani [1 WATHESALONIKE 3:5].

NAMNA NYINGINE TATU ZA KUHUBIRI:

1.         KUWAKARIBISHA NA KUWALETA WATU WENGI KATIKA KANISA LA NYUMBANI NA KANISA KUU (ZEKARIA 8:21).

Kwa kuwaleta wengi Kanisani, kunakuwa pia na nafasi kubwa kwao kuhubiriwa na kuokolewa.  Wakati mwingine ni rahisi zaidi mtu kupokea Injili anapokuwa kati ya watu wengi na akihubiriwa na mtu asiyemzoea.  Nabii hapati heshima nyumbani kwake.  Kila wiki lazima kila mmoja apange jinsi ya kuongeza watu katika Kanisa la Nyumbani na Kanisa Kuu.  Kuja peke yako Kanisani ni uchoyo.  Ni kupenda kula vyote mwenyewe!  Kanisa la Nyumbani kama haliongezeki katika idadi ya watu, inaonyesha watu walio katika Kanisa hilo ni wachoyo.  Vivyo hivyo katika Kanisa Kuu.  Ni lazima kila mmoja awe na lengo la kuleta watu wageni kila siku ya Ibada ya Kanisa Kuu na kuwa tayari hata kuwalipia nauli.  Hii ni njia mojawapo ya kuhubiri.

2.         KUFANYA MAOMBI KILA SIKU KWAMBA WASIOOKOKA WAIPOKEE INJILI NA KUOKOLEWA (WARUMI 10:1).

Hatupaswi kuwa na maombi ya uchoyo kila siku tunapomwomba Mungu.  Maombi ya uchoyo ni yale ya kusema wakai wote “Mungu nipe mimi.”  Pamoja na kumwomba Mungu juu ya mahitaji yetu ya binafsi, inatubidi kila siku kuwaombea wale wasiojua kweli, wakutane na Injili na kuokolewa.  Mungu anasikia na kutenda tumwombapo.  Kufanya maombi ya namna hii ni njia ya pili nyingine ya Kuhubiri.

 

3.         KUTOA MALI ZETU KWA WINGI KWA AJILI YA INJILI (MITHALI 3:9).

Bila kujitoa kwa wingi katika mali zetu, Injili haiwezi kuwafikia wengi.  Injili ni gharama na ni lazima sisi wenyewe tutoe vyote tulivyo navyo kwa ajili ya Injili.  “Watahubirije wasipopelekwa?” [WARUMI 10:15].  Kutokutoa mali zetu kwa wingi kwa ajili ya Injili, ni uchoyo mkubwa.  Ni kutaka kwamba wengine wafe bila kuijua kweli na kuangamia.  Wakati wote lazima tutoe na kuhakikisha kwamba kasha la Injili limejaa fedha tele wakati wote.  Hiyo ni kodi iliyowekwa na Mungu kwa kila mtu aliyeokoka.  Ni lazima tutoe kwa furaha kodi hii ili wengi waokolewe [SOMA 2 NYAKATI 24:8-11].

J A M B O   L A   K U K U M B U K A

Pamoja na kwamba tunapaswa kuzitumia njia hizi tatu, kukaribisha na kuwaleta wageni Kanisani, kutoa mali na kuomba kwa ajili ya Injili, HATA HIVYO, KILA MMOJA LAZIMA AHUBIRI KWA KUTUMIA KINYWA CHAKE.  Yesu aliomba, alijitoa mno kwa ajili ya Injili na kuomba, lakini hata hivyo, alikitumia kinywa chake mno kuhubiri.  Sisi sasa ndiyo vinywa vya Mungu.  Piga kelele wala usiache kuhubiri.

M A S W A L I

1.         Wajibu wa kila siku wa kila mtu aliyeokoka baada tu ya kuokolewa kwake, ni kufanya

nini?

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

2.         Mtu aliyeokoka ambaye hawashuhudii au kuwahubirii wengine juu ya dhambi zao, na kuwaonya anakuwa na hati mbele za Mungu.  Je hii ni kweli?  Kama ni kweli, mambo yapi yatampata kutokana na hatia hiyo?

(a)————————————————————————————————————-

(b)————————————————————————————————————-

3.         Tukiwahubiri watu halafu wakawa hawataki kuziacha dhambi zao na kumfanya Yesu

awe BWANA wao, je  bado tutakuwa na hatia?  [EZEKIELI 33:9].

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————

4.         Taja sifa tatu za mtu aliyeokoka asiyewahubiria wengine juu ya wokovu alioupokea.

(a)————————————————————————————————————-

(b)————————————————————————————————————-

(c)————————————————————————————————————-

5.         Taja namna tatu nyingine za kuhubiri ukiacha kuhubiri kwa kutumia kinywa:

(a)————————————————————————————————————-

(b)————————————————————————————————————-

(c)————————————————————————————————————-

6.         Je inatosha kutoa mali, kufanya maombi kwa ajili ya Injili na kukaribisha watu Kanisani na kuacha kutumia kinywa kuhubiri Injili?

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

7.         Haruni alikuwa msemaji wa Musa kwa watu, na mfano wa Kinywa chake na Musa alikuwa mfano wa Mungu kwa Haruni.  Leo, mtu aliyeokoka ni nani kwa Mungu kwa mfano wa Musa na Haruni?

—————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

8.         Mtu aliyeokoka akifumba kinywa na kutokuhubiri Injili, anakuwa anafanya nini mbele

za Mungu?

(a)————————————————————————————————————-

—————————————————————————————————————-

(b)————————————————————————————————————-

            —————————————————————————————————————-<>

sikose faida zilizomo katika somo lililotangulia “KUOGOPA VITA NA KURUDI MISRI KUSIKOKUWA NA VITA”, ingia hapa ujifunze Neno la Munguhttps://davidcarol719.wordpress.com/kuogopa-vita-na-kurudi-misri-kusikokuwa-na-vita/

<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><>< 

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

                                                         UBARIKIWE NA BWANA YESU!

<><><><><><><><><><><><><><><><><><><>><><><><><><><><><><><><><><>

Advertisements

One comment on “PIGA KELELE, USIACHE KUHUBIRI

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s