PUNJE YA HARADALI NA CHACHU

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Mkuu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.o

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobemini

 Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SIKU YA KUICHAMBUA BIBLIA.

SOMO:  PUNJE YA HARADALI NA CHACHU

(MATHAYO 13:31-33)

(1)      PUNJE YA HARADALI:

Nyakati za Biblia, katika nchi ya Uyahudi, kulikuwa hakuna mbegu yoyote ndogo kama mbegu ya Haradali.   Punje ya Haradali au mbegu ya Haradali ilikuwa ndogo sana kiasi kwamba kama ikichanganyika na mchanga, ilikuwa vigumu kuiona tena mpaka mtu awe na macho makali.  Mbegu hii ilipopandwa, na kuota, hatimaye ilikuwa mti mkubwa uliokuwa na urefu kati ya futi 10 hadi 12.  YESU KRISTO alikuwa kama punje ya haradali.  Alizaliwa katika kijiji kidogo sana cha Bethlehemu (MIKA 5:2) na akaanza na wanafunzi wachache sana (12) lakini hatimaye, ufalme wake umeifunikiza dunia kwa miaka mingi.

(a)              MTI:  Mti katika Agano la kale umetumika sehemu kadha kuwakilisha taifa au ufalme:

  • Mzabibu (Taifa la Israeli) – ZABURI 80:7-11;
  • Mwerezi (Ufalme wa Ashuru) – EZEKIELI 31:3-9;
  • Mti Mkubwa (Ufalme wa Babeli) – DANIELI 4:10-12.

(b)              NDEGE: Katika MATHAYO 13:4,19; ndege wanafananishwa na mwovu au Shetani.  Ni muhimu kufahamu kwamba katika Biblia, kitu kimoja kinaweza kufananishwa na vitu vingi sehemu mbalimbali.  Kwa mfano katika Biblia siyo kila ndege anafananishwa na Ibilisi.  KUTOKA 19:4.  Ndege – Mungu:  ZABURI 103:5, ISAYA 40:31 – Ndege ni WATAKATIFU:  MATHAYO 3:16 – Ndege ROHO MTAKATIFU.

Angalia mifano mingine:

SIMBA:           –           ZABURI 57:4 – WATU WAOVU;

–                      MITHALI 28:1 – WENYE HAKI;

–                      1 PETRO 5:8 – SHETANI;

–                      UFUNUO 5:5 – YESU KRISTO.

NYOKA:          –           MATHAYO 23:23 – WASIOOKOKA;

–                      MATHAYO 10:16 – WALIOOKOKA;

–                      UFUNUO 20:2 – SHETANI

–                      YOHANA 3:14-15 – YESU KRISTO.

Kwa hiyo hapa ndege wanaokaa juu ya mti ni watakatifu katika Ufalme wa Mungu au Ufalme wa Mbinguni.

MAFUNDISHO MUHIMU KATIKA MFANO HUU:

Hatupaswi kamwe kudharau siku ya mambo madogo (ZEKARIA 4:10).  Mungu haanzi na sisi katika makubwa.  Tunapaswa kwanza kuonyesha uaminifu wetu katika mambo madogo (LUKA 16:10).  Hatimaye, ijapokuwa mwanzo wetu ulikuwa mdogo, mwisho wetu utakuwa mkubwa.

2.         CHACHU:

Chachu katika Biblia inatajwa kama mafundisho potofu (MATHAYO 16:11-12);    Uovu na ubaya (1 WAKORINTHO 5:8).  Katika Kanisa ni lazima tuwe macho na mafundisho potofu, haya kama chachu huweza kuchachua donge zima (WARUMI 16:17; 2 WATHESALONIKE 3:14).  Watu wasiolitii neno na kuwatii viongozi wao na kutaka kufundisha yasiyowapasa miongoni mwetu, hawa inatupasa KUZIBA VINYWA VYAO (TITO 1:10-12).  Vivyo hivyo, hatupaswi kuuona uovu na ubaya na kuunyamazia kimya.  Tunapokuwa na ushahidi kamili juu ya uovu na ubaya unaofanywa na wanaojiita wakristo kati yetu, ni lazima tuseme wazi kwa viongozi wetu ili hatua ichukuliwe ya kumuondoa mbaya miongoni mwetu (1 WAKORINTHO 5:1-2, 9-13).  Kuwa radhi na waovu na kuwatunzia siri, ni kuishiriki dhambi yao (ZABURI 50:18; WARUMI 1:32).

Hata hivyo kwa upande wa pili, chachu kwa muda mfupi bila kuonekana kazi yake kwa macho, hubadilisha unga wote.  Neno la Mungu, Maombi, na kuyatendea kwetu kazi mafundisho huweza kubadilisha mji wote na hata nchi yote.

Tutaendelea kuhubiri, kufundisha, kuomba, kuangaza kwa matendo yetu na tutavuna kwa wakati wake tusipozimia Roho (WAGALATIA 6:9).  Tutaona chachu yetu ikichachua Mji wote na Nchi yote katika Jina la Yesu.

Usikose faida zilizomo katika somo “MFANO WA MAGUGU” katika link hii

https://davidcarol719.wordpress.com/mfano-wa-magugu/

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe..

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s