SIFA NA THAWABU ZA MTUMWA MWEMA

Normal
0

false
false
false

EN-US
X-NONE
X-NONE

MicrosoftInternetExplorer4

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SIKU YA KUICHAMBUA BIBLIA

SOMO:      SIFA NA THAWABU ZA MTUMWA MWEMA

Leo, tunajifunza Biblia kkutoka MATHAYO 25:14-46.  Katika mistari hii, tunajifunza SIFA NA THAWABU ZA MTUMWA MWEMA.  Baada ya kuokolewa, yaani baada ya kuwekwa huru mbali na dhambi, tumefanywa WATUMWA WA MUNGU na WATUMWA WA KRISTO (WARUMI 6:22; WAEFESO 6:6; YAKOBO 1:1).  Kazi ya mtumwa, ni kumtumika Bwana wake, kwa kumzalishia mali.  Sisi nasi, kama watu tuliookolewa, ni muhimu kufahamu kwamba tumeitwa kumtumikia Mungu, kwa kumzalishia mali nyingi na kuhakikisha kwamba, Mungu wetu anapata faida kubwa.  Tukiwa watumwa wema, tutapewa thawabu tele na Bwana wetu Yesu.  Katika mistari tunayoiangalia leo, tunajifunza mengi kuhusu jambo hili.  Tutayagawa mafundisho tunayoyapata katika mistari hii, katika vipengele viwili:-

(1)     MFANO WA TALANTA (MST 14-30);

(2)     KONDOO WA MUNGU WALIOBARIKIWA  (MST 31-46)

 

(1)       MFANO WA TALANTA  (MST 14-30)

Katika mistari hii, tunajifunza yafuatayo:-

  1. MTU ATAKAYE KUSAFIRI – Mtu atakaye kusafiri aliyewaita watumwa wake na kuweka kwao mali zake, ni Yesu Kristo.  Kabla ya Yesu Kristo kupaa na kwenda mbinguni, aliwapa watumwa wake vipawa (WAEFESO 4:7-8).  Kila mtu aliyeokoka amepewa kipawa au vipawa, na Yesu Kristo ambaye ni kichwa au Bwana wa Kanisa.  Katika mfano huu, vipawa hivi vinafananishwa na TALANTA.  Yeyote aliye mtumwa wa Kristo yaani yeyote aliyeokolewa, hana chochote anachoweza kukiita cha kwake, kasoro DHAMBI tu.   Vingine vyote vinatoka kwa Mungu wetu aliyetuokoa, ni vipawa tulivyopewa ili kufaidiana (1 WAKORINTHO 12:7; 1 PETRO 4:9-10).
  2. KILA MTUMWA AMEPEWA TALANTA – Kila mtu aliyeokoka amepewa talanta au vipawa mbalimbali.  Neno “TALANTA”, linalotumika hapa, linatokana na neno la Kiyunani, “TALANTON” ambayo ni aina ya fedha yenye thamani kubwa.  Thamani ya TALANTON MOJA, kwa thamani ya sasa, ni karibu na dola za Kimarekani elfu thelathini (US$ 30,000), ambazo ni karibu sawa na Tshs 15,000,000/=.  Kila kipawa alichopewa mtu, ni cha thamani kubwa na kinaweza kutumika kuwafaidia wengi na kumzalishia Bwana Yesu faida.  Bwana wetu Yesu, anatarajia tuzifanyie biashara talanta hizi tulizopewa na kumzalishia faida kubwa.  Tunawezaje kufahamu kwamba talanta zetu zinazalisha faida?  Ni kwa jinsi ambavyo watu wengi wanavyofaidika kutokana na talanta zetu.   Talanta ambayo kila mtu aliyeokoka amepewa ni WOKOVU.  Wokovu ni kipawa cha thamani kubwa.  Ikiwa wokovu wetu unawafaidia wengi, basi kwa kufanya hivyo, tujue tunaifanyia biashara talanta yetu ya wokovu na kumpatia faida Bwana  Yesu.  Kwa mfano, kutokana na wokovu wetu tunaweza tukawa tunawapa watu haki zao bila kuwadai rushwa na wakafaidika na kuufurahia wokovu wetu.  Tukiona hivyo tujue tunaizalisha talanta yetu.  Tukiwapa watu tiketi za usafiri, au huduma mbalimbali ziwe za hospitali, Uhamiaji, Kodi ya Mapato, Idara ya Ushuru wa Forodha n.k; watu hao wanafaidika kutokana na wokovu wetu.  Lolote tunalolifanya ambalo tusingeweza kulifanya kama siyo kutokana na wokovu wetu, basi, ni talanta ya wokovu tunayoifanyia biashara.  Vilevile, tumeokolewa ili tuwahubiri na kuwafudisha wengine hata na wao waokolewe (ZABURI 51:12-13).  Unapokuwa unawashuhudia watu wakaokoka, na kufaidika, kutokana na jinsi ulivyowashuhudia; ujue umezalisha talanta yako ya wokovu.  Ikiwa umepokea muujiza wowote wa Mungu, ujue hicho ni KIPAWA, ni TALANTA.  Yesu anatarajia uitumie talanta hiyo kwa kuizalisha.  Utakapowashuhudia watu wengi juu ya muujiza wako na wakafaidika kwa kuinuliwa imani zao, ujue umeizalisha talanta yako.  Unapowafuatilia na kuwafundisha watoto wachanga kiroho ili waukulie wokovu, na wakafaidika wengi; ujue unaizalisha talanta yako ya ualimu wa Ufuatiliaji.  Tunapofanya yote haya, tunamtumikia Mungu na tunaweza tukaona kana kwamba hakuna faida yoyote bali tunatumia nguvu zetu bure, lakini Bwana wetu atakaporudi kufanya hesabu nasi, tutaona thawabu yake (ISAYA 49:4).  Kipawa au talanta ni chochote ulichopewa ambacho wengine hawana.  Ikiwa ni utajiri, ufundi wa kuimba au kupiga chombo cha kwaya, ufundi wa kuchora, ufundi wa umeme au uashi, huruma kwa wagonjwa na kupenda kuwasaidia, elimu, ufundi wa kupiga chapa,VYOTE HIVI NI VIPAWA AU TALANTA.  Ikiwa ni ukarimu, nafasi yoyote unayopata kumtumikia Mungu Kanisani, karama yoyote, vyote hivyo ni vipawa.  Ukitumia vipawa hivyo kumtumikia Mungu na vikawafanya wengi kufaidika, ujue umezalisha talanta.  Katika mfano huu, aliyepewa talanta tano alizalisha nyingine tano, na aliyepewa mbili alizalisha nyingine mbili.  Bali aliyepewa moja, hakuenda kufanya biashara nayo, aliizika chini kutokana na ubaya na ulegevu wake.  Huyu anafanana na watu wengi waliookoka ambao hawajui maana ya kuzalisha talanta zao.
  3. THAWABU ZA WATUMWA WEMA NA HUKUMU YA WATUMWA WABAYA – Watumwa wema, ni wale ambao wanavitumia vipawa vyao kwa faida ya wengine.  Hawa wataambiwa na Bwana Yesu, “VEMA” au kwa Kiingereza “WELL DONE” na watapewa thawabu tele na kuingia katika furaha ya Bwana wao (MST 19-23).  Watumwa wabaya ni wale ambao wamezikalia talanta zao tu na hawazifanyii biashara.  Hawa ni walegevu na wabaya, na ni watu wa kutoa sababu wakati wote (MITHALI 26:16), lakini pamoja na sababu zao, hawa ni watumwa wasiofaa, watatupwa katika giza la nje (MOTONI) kwenye kilio na kusaga meno (MST 24-30).

(2)  KONDOO WA MUNGU WALIOBARIKIWA    (MST 31-46)

Nyakati za Biblia, mchungaji aliwachanganya kondoo na mbuzi na wakala malisho wakati wa mchana; lakini ilipofika jioni, aliwabagua kondoo na mbuzi na kuwaweka mazizi tofauti.  Vivyo hivyo kwetu.  Leo kondoo na mbuzi wako pamoja duniani, kanisani na kwingineko lakini USIKU WAJA, na kondoo watatengwa mbali na mbuzi.  Kondoo ni wanyama wasikivu, watii, wanaoonekana kama wajinga, wanaomfuata Mchungaji wao, na wanaotulia mahali pamoja.  Mbuzi hawana sifa hizo.  Mtu yeyote asiyeweza kutulia na mke au mume mmoja, huyo ni mbuzi.  Mtu ambaye ni mkaidi, mbishi na mwenye jeuri kwa Watumishi wa Mungu na maneno ya Mungu, huyo ni mbuzi, siyo kondoo.  Kondoo wa Mungu, ni watu wanaotii na kulifuata neno la Mungu, na kuyaangalia maagizo yake yote (ZABURI 119:6,9).  Hata hivyo, kondoo ambao watakuwa miongoni mwa kondoo waliobarikiwa, wakati Mchungaji Mkuu Yesu atakapokuja kubagua kondoo na mbuzi, watakuwa ni wale ambao watawaangalia wale wenye NJAA na KIU na kuwalisha na kuwanywesha.  Siku hizi watu wana njaa na kiu kubwa ya Neno la Mungu (AMOSI 8:11-12).  Heri wao watakaotoa muda wao mwingi kuwahubiri na kuwafundisha watu hawa.  Kwa kufanya hivyo, watakuwa wanamlisha na kumywesha Yesu (MST 40).  Kondoo waliobarikiwa watakuwa ni wale wanaowakaribisha wageni.  Namna yoyote ya kuwakaribisha watu ili wasikie Neno la Mungu Kanisa la Nyumbani, Kanisa Kuu au katika Mkutano wa Injili, na kuwapenda na kuwajali hadi wao nao wanaokoka na kuendelea katika wokovu; kufanya hivyo ni kumkaribisha Yesu.  Kondoo waliobarikiwa pia watawavika walio uchi kwa kutoa mali zao kwa ajili ya Injili na pia watajishughulisha kuwatazama wagonjwa wa kiroho yaani waliookoka ambao wamerudi nyuma, na wagonjwa wa kimwili pia katika Makanisa ya Nyumbani.  Kondoo waliobarikiwa pia watajishughulisha na wale walio kifungoni, yaani wale waliotengwa na jamaa zao kwa ajili ya wokovu wao, au walio katika mateso yoyote kwa ajili ya wokovu wao au walio katika misiba au waliopatwa na mabaya yoyote ambayo yanaweza kuwarudisha nyuma katika wokovu kama wasipopata msaada wowote wa faraja n.k.  Namna yoyote ya kuwatendea mema watu hawa, ni kumtendea Yesu. Hatuna budi kumhudumia Yesu kwa jinsi hii ili tuwe miongoni mwa kondoo wale waliobarikiwa ambao watau

rithi ufalme waliowekewa tayari (MST 34).  Kinyume na hapo, tusipohusika katika huduma, tutajikuta tunakwenda pamoja na wasio haki katika moto wa milele (MST 41-46).  Tumeokolewa ili tuwahudumie wengine! (1 WAKORINTHO 15:45-49).

…………………………………………………………………………………………………………………………………..

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “somo” hili, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe..

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-qformat:yes;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin:0in;
mso-para-margin-bottom:.0001pt;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:10.0pt;
font-family:”Times New Roman”,”serif”;}

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s