TOFAUTI YA KUPUNGA PEPO NA KUTOA PEPO

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

 

SOMO:  TOFAUTI YA KUPUNGA PEPO NA KUTOA PEPO

Nyakati hizi za mwisho kutakuwa na roho nyingi zidanganyazo. Roho hizi zitawadanganya wengi na kuwafanya kuona  kuona kwamba wako na Mungu kumbe Mungu hayupo kati yao.

( 1 TIMOTHEO 4:1 ).

“Basu Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza  roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani”. Miongoni mwa mambo ya siku hizi za mwisho ni roho hizo kuwafanya watu wadanganyike na kufuata mafundisho ya uongo. Hao ni wale wanaoikataa ile kweli.

( 2 TIMOTHEO 4:3-5 )

“Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia walimu makundi makundi kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo”.

( 2 WATHESALONIKE 2:7-12 )

     Watu ambao hawataki mafundisho ya utakatifu lakini wanataka kuona nguvu za Mungu maishani mwao, watadanganywa kwa ishara na ajabu za uongo.

Katika nyakati hizi tunaweza kuona jinsi watu wanavyofanyiwa maombezi kwa kuangushwa chini na hatimaye kusimama bila kupokea muujiza wa uponyaji. Utaweza kuona watu wamejazana madhabahuni wakigaagaa chini na baadaye husimama na kuondoka lakini wakati mwingine huchukua muda mrefu kwao kusimama na kuondoka. Jambo la kushangaza ni siku zote kuonekana watu haohao , mapepo yao hayatoki. Miujiza hii imeenea kote duniani, uatakuta watu wanapiga kelele lakini pepo hawawatoki watu hao. Miujiza ya kimungu huondoa pepo kabisa ndani ya mtu tena kwa mamlaka na kumwacha akiwa mzima. Watu hawa hawafanyi miujiza ya uponyaji bali wanapunga pepo. Ni muhimu kujua kuwa  hata wapagani wanaweza kupunga pepo na kuwafanya wapige kelele. Waganga wa kienyeji wanaweza kupunga pepo lakini hawawezi kuwatoa. Tunawaona wapunga pepo wakitaka kutoa pepo lakini wanashindwa  ( MATENDO 19:13-16 ). Watu hawa walikuwa wa kawaida lakini leo tungewaita walokole kwa kuwa walikuwa watu wa dini.

Jina jingine linalotumika kwa wapunga pepo ni” wapandisha pepo”. Mungu anasema kila anayepandisha pepo ni chukizo mbele zake ( KUMBUKUMBU LA TORATI 18:9-14 ). Waganga wa kienyeji ni wapandisha pepo au wapunga pepo. Kuna mazingira fulani  yanaandaliwa ili pepo wajidhihirishe kwao. Wanaimba na kuchezacheza ili nguvu hiyo ya shetani  iwe dhahiri kwa mfano  wetu tunavyofanya  katika kusifu au kuabudu ili nguvu ya Mungu ionekane  au idhihirike. Mfano Paulo na Sila gerezani walimsifu Mungu na nguvu za Mungu zikashuka milango ya gereza ikafunguka.

Kazi tuliyoitiwa  ni ya kutoa pepo na siyo kupunga au kupandisha pepo ( MARKO 16:17 ‘Na ishara hizi zitafuatana nao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo”. MATHAYO 12:22-28 ). Kazi ya kupunga pepo ni ya shetani. Yesu aliuliza,” je, wana wenu huwatoa kwa nani?”. Swali hili la Yesu lilielekezwa kwa afarisayo walioishangazwa na mamlaka yake ya kuponya wagonjwa na kutoa pepo. Kimsingi hapo alikuwa akiuliza kuhusiana na wapunga pepo au wapandisha  pepo, kwamba wao wanatumia nguvu gain?

Kuna madaraja katika majeshi ya pepo. Katika kutoa kafara tofautitofauti kubwa au ndogo ndipo Mganga anapoweza  kupata pepo wa daraja la juu au la chini. Huyo anayelipa  leseni kubwa yaani kafara , anapewa uwezo mkubwa wa kipepo. Anakuwa na mamlaka makuu kama kamanda wa Jeshi hivyo anaweza kuwaamuru pepo kumwingia mtu na kunyamanzisha pepo wadogo waliomo ndani ya mtu lakini hatimaye hari ya huyo mtu baadaye inakuwa mbaya zaidi kwa sababu idadi yao ( pepo ) imeongezeka.

                                      ( MARKO 6:7 )

“Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu”. Pepo wachafu wanakaa ndani ya mtu mchafu. Ni mfano wa Inzi, hukaa katika uchafu. Kwa hiyo pepo wachafu hukaa ndani ya mtu mwenye dhambi. Dhambi ni uchafu ( ZEKARIA 3:3-4 ). Baba ( mwanzilishi ) wa maovu yote ni Ibilisi ( Shetani ) na huyo ndiye baba yao watendao dhambi ( YOHANA 8:44 ).

 ( YAKOBO 4:4 )

Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu” Shetani ni mungu wa dunia hii ( 2 WAKORINTHO 4:4 ). Kuwa rafiki wa dunia ni kufanya yaleyale wanayoyafanya watu wa dunia hii ambao hawajaokolewa kwa kiumwamini Yesu Kristo. Watu wa dunui maisha yao ni maisha ya dhambi tu maana wao wanayafanya mapenzi ya mungu wa dunia ( baba yao ). Tukianza kuiga kuvaa kwao, kuongea kwao,  kucheza kwao, na mambo mengine mengi yasiyompendeza Mungu, Tutamfungulia Shetani mlango wa kuingia na kufanya maskani ndani yetu. Machizo yote tuwe mbali nayo ( YEREMIA 32:33-34; KUMBUKUMBU 7:26 ). Machukizo yanamfanya Mungu kutuacha kabisa ( 2 NYAKATI 36:14-16 ). Uweza wa Mungu wa kuponya unaweza usiwepo mahali kwa sababu ya kuwepo kwa machukizo. Makuhani nao wanaweza kutenda dhambi na kuingiza machukizo ndani ya nyumba ya Mungu kama tunavyoona katika andiko hilo juu. Watumishi wengi wanatamani kuziona nguvu za Mungu katika huduma zao kama wakati wa Mitume lakini gharama zake zinawashinda. Mungu hawezi kumtumia mtu mchafu ambaye siyo mtakatifu ( WAEBRANIA 1:9 ).

Hivyo basi, vitu vyote tunavyovaa katika miili yetu ambavyo siyo vya mwili kwa asili yake  ni machukizo kwa Bwana. Kuvaa Mapambo na nywele za bandia ni machkizo kwa Bwana. Kama ingekuwa ni mapenzi ya Mungu tuvae Kwa mfano Heleni, Mungu angeweka tundu kwenye masikio yetu ili kutuandaa kwa ajili ya mapambo. (  1 TIMOTHEO 2:9-10; 1 PETRO 3;3-5;  ISAYA 29:16; WARUMI 9:19-21 ). Hatutaweza kuziona nguvu za Mungu katika maisha yetu kama nyakati za Mitume ni mpaka kanisa la sasa litakapotambua kuwa msingi wa Mitume na Manabii ulishaachwa ( WAEFESO 2:20 ). Mitume waliwafundisha watu kutokufuata fasheni ( namna ) za ulimwengu huu lakini leo hii mafundisho yamna hii ni dadra sana kuyasikia ( WARUMI 12:2 ). Pia waliweka msisitizo juu ya kutokufuata mataifa kufanya hili au lile wafanyalo kwa sababu nia za Mataifa ni batiri ( WAEFESO 4:17 ). Kati ya mataifa kuna makahaba ambao kazi yao ya ukahaba inawafanya kutafuta mavazi ya kuvaa ambayo yatawafanya hao wanaotafutwa kuvutika na kuwafuata katika uchafu. Biblia yetu imetaja mavazi ya kikahaba ( MITHALI 7:10 ). Fasheni nyingi za kidunia zinadizainiwa  na mkuuwa dunia na mfalme wa uwezo wa anga  ( WAEFESO 2:1-3 ).

…………………………………………………………………………………..

        JE UNAPENDA  KUMPA YESU MAISHA YAKO?

Mpendwa msomaji, baada ya kusikia yote haya kutoka kwa nabii aliyetumwa kukuletea ujumbe huu, usifanye moyo wako kuwa mgumu.  Hii ni nafasi ya kipekee ya kuokoka.  Je, unajuaje kama utaamka kitandani baada ya kulala usiku wa leo?  Wakati uliokubalika wa wokovu ni sasa (2 WAKORINTHO 6:2).  Labda utaniuliza, ili uokoke, ufanyeje?  Jibu ni rahisi, kwa imani ukitubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, na kumwambia Yesu Kristo akusamehe, utasamehewa sasa hivi, na msamaha wa dhambi, huambatana na wokovu (LUKA 1:77).  Je, uko tayari kuokoka sasa hivi?  Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii kwa dhati toka moyoni, Mungu baba asante kwa kuniletea ujumbe huu.Natubu dhambi zangu zote, kwa kumaanisha kuziacha. Yesu Kristo nakuomba unisamehe dhambi zangu na kunipa uwezo wa kushinda dhambi na kuniokoa kutoka katika mateso ya moto wa milele. Asante, kwa kuniokoa katika Jina la Yesu.  Amen.  Tayari sasa umeokoka, na kwa hakika unakwenda mbinguni sasa, hata ukifa leo.  Ili uzidi kuukulia wokovu, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!. .

                                     . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook, Twitter n.k,  kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

                                                         UBARIKIWE NA BWANA YESU!!!

Advertisements

2 comments on “TOFAUTI YA KUPUNGA PEPO NA KUTOA PEPO

  1. HAKIKA MUNGU AKUBARIKI SANA, NIMEBARIKIWA SANA SOMO HILI HATA NIMEAMUA KU-SHARE SOMO HILI KATIKA FACEBOOK.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s