UJUMBE KWA KANISA LA TANZANIA

UJUMBE KWA KANISA LA TANZANIA
TAREHE 20/ 03 /2012 SAA 9:11

MCHUNGAJI ADAM JOSEPH
Nikiwa nyumbani kwangu majira ya saa8 nikitafakari mwenendo wa Dunia ulivyo, ndipo Neno la Bwana likanijia kusema, “Adam mwanadamu nakutuma kwa Kanisa langu la Tanzania nzima mjini na vijijini, ukaseme maneno yote ninayokuambia. Usiogope wala usitetemeke mbele yao nisije nikakutetemesha, uwe na moyo mkuu na wa uhodari maana najua wengi watakupinga kwasababu mioyo yao imetiwa ganzi soma YEREMIE 1:17-19, jitie nguvu ukaseme usiogope mimi niko pamoja nawe nikuokoe usiogope wala usifadhaike simama imara usiogope.

Liambie kanisa langu limeacha kweli yangu na kugeukia njia zake, litambue huu sio wakati wa kustarehe wakati watu wanaangamia na kupotea. Kanisa langu limeacha upendo wa kwanza, kila mmoja anajijari nafsi yake na watoto wake soma UFUNUO 2:4-5. Kanisa langu limekosesha watu wengi wasiniamini kwa sababu hakuna utofauti wa matendo yao. Kama ni kutembea nusu uchi, na watoto wangu wanatembea nusu uchi, na kama ni kuvaa mavazi ya kigeni na watoto wangu wanavaa mavazi ya kigeni SEFANIA 1:8. Ole kwa wachungaji wanaokula na kupuliza wanapoza maneno yangu. Nyumbani mwangu hamna chakula cha kutosha, imebeki ni kufarijiana amani wala hapana amani soma YEREMIA 6:14. Hawawaambii watu makosa yao wanaogopa kukimbiwa wanafurahi kujaa watu ndani ya majengo makubwa lakini siyo kuwaambia watu makosa yao soma MATENDO YA MITUME 5:1-4. Kanisa langu limeikaribisha Dunia nyumbani mwangu. Hofu haimo, watoto wangu hawalipi zaka kamili bali ni uongo mtupu. Wachungaji wameruhusu mitindo ya Dunia iingie nyumbani mwangu soma WARUMI 12:2. Wanawake wanavaa mavazi ya kubana wamejaa tamaa ya kidunia. Nimewaambia wanawake wavae mavazi ya kujistiri lakini wamekataa soma 1TIMOTHEO 2:9-10. Waimbaji nao sijui wanamsifu nani, nani anayekubaliana na uchafu maana kusifu kunawapasa wanyoofu wa moyo. Waimbaji wamejaa majivuno, masengenyo, wivu, hasira, chuki na hawana moyo wa rehema ndiyo maana utukufu wangu haushuki kama hapo mwanzo, soma 2 NYAKATI 5:12-14.

Nimeliagiza Kanisa langu kupendana lakini upendo haupo. Watoto wangu wanabaguana na kuchukiana hata wachungaji hawawafundishi watoto habari ya upendo bali mafanikio na kuwafariji kuwa wanakwenda mbinguni, kwa nani? Huko wanakokwenda ni wapi? Maana mimi Bwana Mungu wao ni Upendo. Soma 1 YOHANA 4:19.

Jinsi Dunia iendavyo ndivyo baadhi ya watoto wangu wanavyoenenda. Wengine wameacha matumizi ya asili. Soma WARUMI 1:26. Naja kama Mwizi, siku msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja kuchukua Kanisa lake lililosafi, takatifu.

Watoto wangu wanaangalia picha za ngono wanajitia unajisi. Kanisa langu nalipa shauri, huu sio wakati wa kucheka na kustarehe bali liomboleze maana siku za kujiliwa kwake zinafanya haraka kuja. Soma YOELI 1:13-15. Omboleza Ee Kanisa langu, maana siku usiyodhani unakwenda kunyakuliwa asema Bwana wa majeshi.

Wanawake hawawatii waume zao, wamejaa kiburi za dharau wakati nimewafananisha na Kanisa. Soma WAEFESO 5:22-24. Watoto wangu hawawatii viongozi wao kama nilivyoagiza. Soma WAEBRANIA 13:17. Nasema tendeni mema, acheni maovu ambayo mwisho wake ni mbaya. Omboleza wewe uliyependwa, tangaza wokovu kwa watu, matendo yako yawe nuru wapate kujifunza kwako. Epuka mapema ghadhabu yangu inayokwenda kuikumba Dunia na wote wakaao ndani yake. Kanisa linitafute. Soma AMOSI 5:5-9. Enyi mnaopuuza maneno yangu, siku zinakuja ambazo mtanitafuta wala hamtaniona, mtalia sitasikiliza vilio vyenu. Geukeni basi mkatende haki, nawapenda nitafuteni nami nitaonekana asema Bwana”.
MCHUNGAJI ADAM JOSEPH,
KANISA LA EVANGELISTIC ASSEMBLIES OF GOD,
SIMU +2755 768 657482 / +255 688 856581.
Ujumbe huu umeandikwa na David Carol na kutumwa kwenye mtandao
Simu , +255 764 847847 / +255 782 847747
Email: davidcarol04@gmail.com
Blog: WWW.davidcarol719.wordpress.com
Mungu akubariki sana kama utaona vema ku”share” au ku “like”

Advertisements

One comment on “UJUMBE KWA KANISA LA TANZANIA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s