UTAKASO 1

ZACHARY KAKOBE

Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SOMO:     UTAKASO

Somo la “Utakaso” au kwa kiingereza “Sanctification” na kiyunani “Hagiasmos” ni moja kati ya mafundisho ya msingi sana Katika kanisa la Mungu. Kukosa mafundisho haya katika Kanisa la Mungu, kunawafanya watu waliookoka, waonekane “Sub-standard”, yaani wenye viwango vya chini; vinavyowafanya wasitambulike  au kudhihirika vizuri kwa ulimwengu, kwamba kweli wameokoka. Mtu ambaye ameokoka lakini hajatakaswa; ni vigumu kuwa nuru ya dunia. Hauwezi kusitirika au kufichika. Kila mmoja atauona mji huo.

       Watu wengine waliookoka wamefikiri, na wengine kufundisha kwamba, mtu anatakaswa na kuwezeshwa kuishi maisha ya Utakatifu, pale anapojazwa  au kubatizwa kwa Roho Mtakatifu. Hii sio Kibiblia. Ubatizo wa Roho Mtakatifu, haumfanyi mtu kuwa na uwezo wa kuishi maisha Utakatifu. Ubatizo wa Roho Mtakatifu, unamfanya mtu aliyeokoka awe shahidi aliyevikwa “uwezo utokao juu”, unaomuwezesha kujizalisha mwenyewe kwa wingi au kuwaleta watu wengi kwa Yesu anapowahubiria ( LUKA 24:47-49; MATENDO 1:8; MIKA 3:8 ). Makusudi ya ujazo wa Roho Mtakatifu, ni zaidi ya kumwezesha mtu kunena kwa lugha mpya. Lugha mpya ni ishara ya kwanza itakayoonekana kwake, lakini uthibitisho halisi wa kujazwa au kubatizwa kwa Roho Mtakatifu, ni kuwa na uwezo wa kuwaleta watu wengi kwa Yesu. Wanafunzi wa Yesu kabla ya Ubatizo wa Roho Mtakatifu hawakuwa na matokeo ya kuridhisha katika ushuhudiaji wao, lakini baada ya kujazwa Roho Mtakatifu maelfu ya watu waliokolewa katika huduma yao. Ukimsikia mtu leo anasema alijazwa Roho Mtakatifu miaka kumi iliyopita , lakini hajamleta mtu yeyote kwa Yesu au ameleta watu wawili watatu tu kwa Yesu; huu siyo ubatizo wa Roho Mtakatifu.

                 KUOKOKA NA KUTAKASWA NI MAMBO MAWILI TOFAUTI

        Ni mafundisho yasiyosahihi kudhani mtu anapookolewa, wakati huo huo anatakaswa pia. Kuzaliwa mara ya pili au kuokoka, na kutakaswa au kupokea utakaso; ni mambo mawili tofauti kabisa. Kuzaliwa mara ya pili au kuokoka, ni kwa watu wasiomjua Yesu kama Bwana na Mwokozi wao au Mataifa; lakini Utakaso, ni kwa watu waliokwisha kuokolewa tayari. Mtu anaweza akawa ameokoka, lakini bado akawa anaishi maisha yaliyo mbali na Utakaso. Hasira, wivu, chuki, kusengenya, kugombana na kugombania ukubwa, kiburi, majivuno, kutokusamehe, kinyongo. Kupenda dunia n.k;  bado vinaweza kuonekana kwa mtu aliyeokoka ambaye hajatakaswa. Watu wa namna hii siyo nuru ya ulimwengu. Mataifa wakiwaangalia watu wa namna hii, wanaweza kuona  kwamba hawajaokoka. Hata mtu ambaye ameokoka lakini bado ana hali ya namna hii, anaweza kuijiwa na mashaka na kuwaza, “Hivi mimi nimeokoka kweli au najidanganya?” Hii ni hatari sana kwa mtu mwenye mawazo ya namna hii, hali hii ikijengeke ndani yake anaweza kuacha wokovu na kurudi nyuma. Mtu wa namna hii anahitaji Utakaso tu maana amekwisha okoka.

                   UTAKATIFU MAANA YAKE NINI?

        Neno “Utakatifu” linatajwa sana katika Kanisa la Mungu, lakini ni wachache wanaofahamu maana yake. Sasa, bila kufahamu maana yake tunawezaje kufahamu  kwamba tunaishi katika Utakatifu? Hii ni hatari, maana Biblia inasema katika WAEBRANIA 12:14, kwamba, hakuna  mtu atakayemwona Bwana asipokuwa na Utakatifu. Sasa basi, Utakatifu maana yake nini?  Utakatifu ni kuwa kama Yesu Kristo katika moyo, nia, tabia. Mawazo na matendo Utakatifu ni hotuba ya Yesu alipokuwa mlimani katika MATHAYO SURA 5. 6 na 7 zote. Ikidhihirika na kushuhudiwa kwa mtu aliyeokoka.

         Utakatifu siyo suala la kufanya matendo ya nje tu yanayoonyesha tabia ya Kristo. Mungu anaangalia yale ambayo wanadamu hawawezi kuyajua. Je, unaposema au unapofanya jambo, una nia ipi au unawaza nini? Ulivyo nje ndivyo ulivyo moyoni.

                    KUTOKUIPENDA DUNIA NA MAMBO YAKE YA KUKOSESHA

                                     ( 1 YOHANA 2:15-17 ; YAKOBO 4:4 )

       Je, furaha za kidunia hazikutamanishi moyoni? Unaposikia habari za ligi ya vilabu vya mpira, hutamani moyononi kuifatilia ligi hiyo, na kujua klabu ipi inayoongoza katika ligi, na ipi inafuata? Je, unaposikia kwa watu kwamba klabu Fulani, uliyokuwa unaipenda kabla ya kuokoka, imeshindwa katika ligi, hakuna namna yoyote ya kuumia au kuhuzunika moyoni? Ushabiki wa Simba na Yanga bado unakuvuta moyoni? Unapoona maelfu ya watu wanakwenda mpirani, na wengine wanabaki majumbani kusikia mpira ukitangazwa Redioni , na siku hiyo ndiyo siku ya ibada Kanisani; Je, hakuna namna yoyote ya kujing’ang’aniza kuja Kanisani siku hiyo? Ukiwa una hali hii, ujue hujatakaswa.

      Je, moyoni hakuna tamaa ya kusikia kipindi cha michezo cha saa mbili kasorobo? Je huna tamaa ya moyoni ya kusikia vipindi mbalimbali vya kidunia vya redioni kama Mchezo wa Redio, vipindi vya maigizo na vichekesho katika televisheni kama The Comedy, Ariginal Comedy, Fataki la wiki, Futuhi n.k ? Unaweza ukawa umeifunga redio au televisheni yako, lakini unaposikia vipindi hivi katika redio au televisheni za wengine, vinakutamanisha. Kama ni hivyo, bado hujatakaswa. Jiulize mwenyewe, unapoangalia na kusikiliza vipindi vya kielimu tu kwenye televisheni yako au redio yako kama Taarifa ya habari, Majira, Sayansi na Teknolojia n.k; halafu ukaizima televisheni au redio yako ili usiangalie  au kusikiliza vipindi vingine visivyofaa au vilivyokinyume na Imani ya Wokovu, hakuna kujilazimisha na kuumia moyoni kiasi cha kuona Ukristo ni mgumu mno? Je, unaposikia vipindi hivi halafu ikafata miziki ya dansi redioni au katika televisheni unaweza ukavumilia kuisikia au kuiona na ukaifurahia moyoni? Kama ni hivyo hujatakaswa.

       Je, vichekesho vya kidunia, kama vichekesho vya katuni magazetini au katika televisheni na video na vipindi vcya vichekesho, vinakufurahisha moyoni? Kama ni hivyo, udunia bado umejaa moyoni mwako. Unahitajika kutakaswa.

      Je, huvutwi na michezo mingine inayowapa furaha watu wa dunia kama karata, darts, snake & ladder, bao, drafti, kuogelea, riadha au boxing? Ikiwa ulikuwa mwanariadha au mchezaji wa mpira wa miguu au netiboli kabla ya kuokoka, na huenda hushiriki michezo hiyo kwa sasa; Je, unapowaona wengine wakishiriki michezo hiyo au unaposikia habari za michezo yao, Je, hakuna lolote  moyoni linalokushawishi kuona michezo hiyo kuwa ni kivutio kiasi cha kukufanya uwaze,”Ningekuwa ninaendelea na michezo hiyo ningekuwa leo ningekuwa nyota kama fulani?” Kama ni hivyo, bado hujatakaswa. Yesu Kristo hakujihusisha na michezo ya namna hii na Biblia inasema Mwana ( YESU ) hawezi kutena neon mwenyewe ila lile ambalo amuona Baba analitenda kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vilevile ( YOHANA 5:19 ). Jiulize mwenyewe, Mungu anaweza kucheza mpira, riadha, bao, drafti, snakes, ladder, daets au karata? Jibu unalo mwenyewe. Utaona kwamba hata kutamka michezo hii na kuihusisha na Mungu inazishitaki dhamiri zetu. Kama Mungu hawezi basi na sisi hatuwezi.

      Je, kabla ya kucheza michezo hii unaweza kuifungua kwa katika jina la Bwana Yesu, ukimshukuru Mungu Baba kwa michezo hiyo? Kama siyo basi Biblia inatuonya tusifanye lolote ambalo hatuwezi kulifungua kwa sala ya jinsi hii ( WAKOLOSAI 3:17 ). Wakati wa kanisa la kwanza la Mitume, michezo mbalimbali ilikuwepo. Wakati huo ilikuwepo michezo ya “Olympic”, “Pythian”, “Nemean” na “Ishimian” lakini mtume Paulo anaeleza wazi wazi kuwa michezo yetu Wakristo ni michezo ya rohoni, ni mashindano ya rohoni, tukiutumikisha na kuutesa mwili kwa kujizuia yote, na kuukatalia matakwa yake, ili tukubaliwe na Mungu na kupata taji isiyo haribika ( 1WAKORINTHO 9:24-27 ). Ni mashindano ya rohoni ambayo yatampa manufaa makubwa yeye ashindaye ( UFUNUO 2:7, 11, 17, 26; UFUNUO 3:5,12,21 ).

     Jiulize mwenyewe tena. Je, mziki wa dansi haukuvutii? Bado unatamani moyoni kufungua redio yako na “kuburudika” na mziki wa dansi? Watu wa dunia redioni wanasema “tuburudike” na mziki ufuatao unaopigwa na bendi Fulani ya dansi. Je wewe nawe mziki wa dansi ni “burudani” moyoni mwako? Kama una hali hiyo ujue hujatakaswa. Endelea kujiuliza mwenyewe. Unapojitahidi kufunga redio yako, moyoni mwako hakuna tamaa ya kufungua, unaposikia muziki wa dansi katika redio za wengine? Unapopita mitaani kwenye maduka yanayouza kaseti za muziki wa dansi, muziki huo unakutamanisha  unapousikia ukipigwa katika maduka hayo? Je hakuna wakati wowote  unapojikuta umejisahau, na ukawa unatikisa mwili wako kucheza muziki wa dansi? Unapokuwa katika basi la abiria ambalo kuna muziki wa dansi, unaopigwa kwenye kaseti ndani ya gari hiyo; Je, muziki huo haukusisimui moyoni?

      Je, kama wewe ni mpiga gitaa au kinanda katika kwaya ya kanisa, huvutwi kutoka moyoni kuzifanyia zoezi nyimbo za wapiga muziki wa mataifa kwa kutumia gitaa hilo au kinanda, na kuzileta nyimbo hizo katika Ukristo? Kama ni hivyo, moyo wako umejaa udunia! Je, hakuna tamaa moyoni ya kuangalia sinema au video za kidunia au ngoma za asili kama mdundiko, sindimba n.k? Kama ni hivyo, unahitaji utakaso.

      Mtu yeyote aliyetakaswa, furaha zote za dunia zinakuwa ni chukizo kubwa kwake. Kutoka moyoni kabisa, ametengwa na furaha za kidunia, na wote walio katika furaha hizo anawahurumia. Hakuna namna yoyote ya kuchota kidogo kutoka duniani na ukampendeza Mungu, maana mungu wa dunia hii ni Ibilisi. Kewa kidogo kwa Mungu na wakati huo huo  kuwa duniani kwa Ibilisi, ni kufanya uzinzi. Biblia inasema kwamba atakayekuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa ADUI WA MUNGU. Mungu anatutamani  sana na kuona wivu juu yetu na hataki kabisa tuchangamane na kufanya unafiki  tena na dunia  ambayo mungu wake ni Shetani ( YAKOBO 4:4-5; 2WAKORINTHO 4:3-4 ).  Mtu akiipenda dunia na mambo yaliyomo katika dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake ( 1 YOHANA 2:15-17 ). Mtu aliyetakaswa, kwake, mambo yote ya kidunia yanayokuwa furaha na starehe za watu wa dunia, kwake ni mavi, ni uchafu, na chukizo tena hayamtamanishi  tena moyoni wala mawazoni. Hayana faida tena  kwake ( WAFILIPI 3:7-8 )

                      MPE YESU LEO MAISHA YAKO AYATAWALE

Tunasoma haya katika LUKA 1:77, “Uwajulishe watu wake wokovu, katika kusamehewa dhambi zao”.   Hii ina maana kwamba ukiisha kutubu dhambi zako leo utasamehewa kwa hakika, na hivyo kupata wokovu mara moja.  Je, kweli utasamehewa?  Jibu ni Ndiyo!  Yesu mwenyewe anasema katika YOHANA 6:37, “……….Wala yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe”.  Hivyo kwa dhahiri, leo hii, dakika hii hii, utasamehewa na kupata wokovu.  Je, uko tayari kuokoka sasa na kuhesabiwa miongoni mwa wale watakaoingia mbinguni na kuishi na Mungu milele, hata wakiiaga dunia sasa hivi?  Ukiwa tayari kuifuatisha sala ifuatayo ya toba, mara tu baada ya sala hii, nitakuombea na kwa ghafla utawezeshwa kushinda dhambi.  Je, uko tayari kuifuatisha sala hii sasa?  Najua uko tayari.  Basi sema maneno haya,  “Mungu Baba, natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Naomba unisamehe na kuniosha dhambi zangu kwa damu ya Yesu iliyomwagika msalabani.  Niwezeshe kushinda dhambi kuanzia sasa.  Liandike sasa jina langu katika kitabu cha uzima mbinguni.  Asante kwa kuniokoa, katika Jina la Yesu, Amen”.  Sasa ninaomba kwa ajili yako, “Mungu Baba msamehe kiumbe wako huyu dhambi zake zote, na mpe uwezo wa kushinda dhambi kuanzia sasa na kumuokoa. Mbariki kwa baraka zote katika Jina la Yesu, Amen”.  Tayari umeokoka.  Ili uzidi kuukulia wokovu, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI!!!

                                     . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

                                                          . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .         

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

                                                         UBARIKIWE NA BWANA YE

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s