VITU VIPYA NA VYA KALE PAMOJA NA JUYA

ZACHARY KAKOBE

Neno la Uzima kutoka kwa  Askofu Mkuu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SIKU YA KUICHAMBUA BIBLIA.

SOMO:      VITU VIPYA NA VYA KALE PAMOJA NA JUYA (MATHAYO 13:47-52)

 

Katika MATHAYO 13:47-52, tunapata mifano miwili ya mwisho ya Yesu katika SURA YA

13 ya Kitabu cha MATHAYO.  Ni makusudi ya somo la leo, kuichambua mifano hii na

kujifunza yale ambayo Yesu anayokusudia kutufundisha kwa mifano hii.  Tutaanza

kwanza na mfano wa mwenye nyumba ambaye anatoa katika hazina yake vitu vipya na

vya kale na tutamalizia na mfano wa juya lililotupwa baharini.

(1)            VITU VIPYA NA VYA KALE (MT. 13:52)

1.   MWANDISHI:Waandishi walikuwa ni waalimu wa torati au waalimu wa Neno la Mungu.  Hawa ndio walioitafsiri torati au neno la Mungu na kuwahubiri watu kwa urahisi mpaka wayafahamu wapasayo kuyatenda sawasawa na torati (NEHEMIA 1: 13; MARKO 9:11; LUKA 5:17).  Hata hivyo waliongeza katika maneno ya Mungu mafundisho yao (MATHAYO 23:2-4).

2.   MTU MWENYE NYUMBA: (MATHAYO 10:25)  Mtu mwenye Nyumba ni Yesu Kristo mwenyewe.

3.   VITU VIPYA NA VYA KALE:  Vitu vipya na vya kale katika elimu ya Ufalme wa mbinguni, ni kweli yote kutoka katika Agano la Kale na Agano Jipya.

 

MAFUNZO ANAYOTUPA YESU KATIKA MFANO HUU

Wahubiri wa leo au waalimu wa Biblia ambao ndiyo waandishi wa leo, wanapaswa kuichambua kweli yote inayohusiana na wakati huu, kutoka katika AGANO LA KALE na AGANO JIPYA kama alivyofanya mtu mwenye nyumba, kichwa cha Kanisa Yesu Kristo.  Katika MATHAYO sura ya 13 peke yake Yesu ameitumia kweli kutoka Agano la Kale katika MATHAYO. 13:14-15, 17, 32, 43.  Yesu Kristo mara nyingi katika mafundisho na maneno yake alitumia maandiko ya Agano la Kale (MATHAYO. 4:4, 7, 10 n.k. MARKO. 4:12; 7:6-7; 11:17; 12:10-11 n.k.  LUKA. l7:27; 17:32; 19:46; 20:41-44; n.k.  YOHANA  3:14; 11:34-35; n.k.).  Wako waalimu wa Biblia, au Wahubiri wa leo ambao wanatumia Agano la Kale tu katika mafundisho yao.  Hivi sivyo Yesu anavyotufundisha.  Wako wahubiri wengine hawataki kutumuia kabisa Agano la Kale na wanajisikia vibaya wakiona mtu anahubiri kutoka katika Agano la Kale.  Wao wanahubiri kwa kutumia Agano Jipya tu.  Hii pia siyo sahihi kulingana na mafundisho ya Yesu mtu mwenye nyumba.  Elimu ya Ufalme wa mbinguni ni hazina iliyo na vitu vipya na vya kale.  Pamoja na kwamba leo hatuko chini ya Agano la Kale (WAEBRANIA 8:13; 9:1-16; 10:9, 19:20), hata hivyo ziko kweli za kale au za Agano la Kale ambazo bado ni kweli za Elimu ya Ufalme wa mbinguni katika kipindi tulichonacho.  Kwa mfano, watoto wanapaswa kuwatii wazazi ili wapate heri katika Agano la Kale na Jipya (WAEFESO 6:1-3; KUTOKA 20:12 n.k.)

SABABU TANO ZA KUTUMIA AGANO LA KALE NA JIPYA KATIKA MAFUNDISHO

Kwa mhubiri au mwandishi wa leo, kuna sababu tano za kutumia Agano la Kale na Jipya katika Elimu ya Ufalme wa mbinguni:-

  1. KUONYESHA UWIANO WA MANENO YA MUNGU (WARUMI 10:6-8).
  2. KUONYESHA MAMBO YANAYOTENDEKA VILEVILE NYAKATI ZOTE         (WARUMI 2:21-24 linganisha na EZEKIELI 36:20; WARUMI 8:35-37 linganisha na         1 WAFALME 19:13-18; WARUMI 15:20-22 linganisha na ISAYA 52:15).
  3. KUTOA MAELEZO YA KUTOSHA KUHUSU KWELI FULANI (WARUMI 1:17; 4:6-8, 18-21; WARUMI 9:19-21 linganisha na ISAYA 29:16, 45:9; WARUMI 15:9-13; MATHAYO 2:4-6, 13-18 n.k.).
  4. KUIHAKIKISHA KWELI FULANI (WARUMI 3:3-4, 10-18, 23; WARUMI 4:2-16; 5:12-19; 9:7-18; 12:19-20).
  5. KUHAKIKISHA KUTIMILIZWA KWA UNABII (WARUMI 9:25-26; 10:16; 11:26-27; 15:9-13; MATHAYO 2:4-6, 13-18 n.k.).

2.         JUYA LILILOTUPWA BAHARINI   (MATHAYO 13:47-50)

Juya ni aina fulani ya wavu mrefu na mpana unaotumiwa na wavuvi.  Hutandazwa juu ya eneo kubwa la maji na samaki hunasa katika wavu huo.  Kisha hukokotwa kwa kuvutwa kutoka nchi kavu.  Juya pia huitwa jarife katika Biblia zetu za Kiswahili (ISAYA 19:8; MATHAYO 4:18; YOHANA 21:6-8).  Juya linapokokotwa na wavuvi na kuletwa nchi kavu, haliwi limenasa vitu vizuri tu bali na vibaya ambavyo havitakiwi na wavuvi.  Mawe, samaki, nyoka, vitu vichafu vilivyooza n.k; pia hunaswa katika juya.  Ni kazi ya mvuvi kuanza kutenga samaki mbali na mawe, nyoka n.k.  Hivi vibaya hutupwa maana havina thamani.  Bahari katika Biblia hufananishwa na Ulimwengu (UFUNUO 20:13).  Kila mtu ulimwenguni kwa sasa amenaswa katika juya.  Mpaka wakati huu, malaika wanalivuta juya kulileta nchi kavu.  Wakati wowote kuanzia sasa itakuwa mwisho wa dunia.  Juya liko karibu sana kufika pwani.  Malaika hapo pwani, watawatenga samaki mbali na nyoka, mawe, vitu vichafu n.k.  Je utakapofika nchi kavu utakuwa miongoni mwa samaki au mawe?  Mawe na vitu vibaya vyote ni  wale wenye mioyo migumu ambayo hailipokei Neno la Mungu na kulitenda bali wanadumu kufanya dhambi.  Vitu vibaya vyote vitatupwa katika tanuru la moto.  Nyakati za Biblia, wavuvi walikoka moto kando ya bahari kwa ajili ya kuchoma vitu vibaya na pia kuoka samaki wazuri (YOHANA 21:9).

 

MATHAYO 13:51: “Yesu aliwauliza, Mmeyafahamu hayo yote?  Wakamwambia, naam“.

HERI WEWE UKIWA MIONGONI MWA SAMAKI, ASOMAYE NA AFAHAMU.

 Usikose faida ya Neno la Mungu katika somo”HAZINA ILIYOSITIRIKA NA MFANYABIASHARA”, katika link hii https://davidcarol719.wordpress.com/hazina-iliyositirika-na-mfanyabiashara/

…………………………………………………………………………………………………………………………………..

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni?  Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).  Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27).  Kinyonge ni kipi?  Ni yule anayetenda dhambi.  Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge!  Je, wewe ni mtakatifu?  Jibu ni la!  Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13;  YOHANA 14:6).  Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni;  Mungu Baba asante kwa ujumbe huu.  Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.  Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo.  Bwana Yesu niwezeshe.  Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu.  Amen.  Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni.  Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu.  MUNGU AKUBARIKI !!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe..

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s