WAJIBU WA KUUFUGA ULIMI

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SOMO:  WAJIBU WaA KUUFUGA ULIMI

Neno letu la msingi katika somo letu la leo, limetoka katika YAKOBO 3:2-12. Katika mistari hii tunajifunza kuhusu “WAJIBU WA  KUUFUGA ULIMI”. Bwana  ampe kila mmoja wetu neema ya kulisikia Neno hili kwa makini na  kulitenda , ili iwe faida kwetu na kwa wengine wanaotuzunguka, katika Jina la Yesu! Tutajifunza somo hili kwa kuligawa katika vipengele vitano:-

( 1 ).  WAJIBU WA KUUFUGA ULIMI

( 2 ).  ULIMI CHANZO KIKUU CHA DHAMBI

( 3 ).  ULIMI CHANZO KIKUU CHA MAANGAMIZO NA KUPOTEZA NGUVU YA

          MUNGU.

( 4 ).  HATUA MBILI ZA KUCHUKUA ILI KUUDHIBITI ULIMI

( 5 ).  JINSI YA KUUFUGA ULIMI

( 1 ).  WAJIBU WA KUUFUGA ULIMI.

Ulimi una kazi  kubwa sana kwa mtu aliyeokoka, kwa ulimi tunawahubiri watu  na kuwaambia watubu dhambi zao na kuokoka. Kwa ulimi, tunakemea pepo wachafu na kuwaombea wagonjwa na wenye mateso mbalimbali. Kwa  ulimi tunawabariki watu katika kazi,biashara na mateso yao. Kwa ulimi tunalifundisha Neno la Mungu. Kwa ulimi tunaimba nyimbo za kumsifu Mungu na kumwabudu. Sasa basi, ni muhimu kufahamu kwamba ili ulimi utende kazi hizi  kwa mafanikio makubwa, hauna budi kuwa mtakatifu. Ulimi hauwezi kutoa Baraka hizi kwa watu na wakati huo ukatoa laana yaani maneno yasiyofaa. Baraka hizi zinaitwa pia maji matamu  na maneno yasiyofaa pia yanaitwa maji machungu. Ulimi unaotoa maji machungu hauwezi kutoa maji matamu wakati huohuo maana chemichemi katika jicho moja haiwezi kutoa maji matamu na maji machungu au maji chumvi wakati huohuo ( YAKOBO 3;10-12 ). Ili Mungu azitumie ndimi zetu, sharti ndimi zetu tuzifuge au kuzitawala kama wanyama wa kufugwa na kuhakikisha hazitoi maji machungu. Tukiziachilia ndimi zetu kufanya dhambi hatuwezi kutumiwa na Mungu kikamilifu. Mungu anatafuta watu watakatifu, wakamilifu wasiojikwaa katika kunena maana tunahesabiwa haki kwa maneno yetu ( YAKOBO 3:2; MATHAYO 12:36-37 ). Na ulimi wetu ndiyo chombo cha kutendea kazi.

( 2 ).  ULIMI CHANZO KIKUU CHA DHAMBI

SIyo rahisi kwa jitihada za kibinadamu kuufuga ulimi na kuufanya usifanye maovu, kwa sababu karibu dhambi zote zinautegemea ulimi. Ni vigumu kufanya uasherati na uzinzi bila kufanya mipango kwa kutumia ulimi. Wizi pia hutangulia mipango inayofanywa na ulimi. Uuaji na kutoa mamba na aina nyingi za mauaji, hutanguliwa kwanza na mazungumzo yanayotokana na ulimi. Kutoa na kupokea rushwa ni maatokeo ya kazi ya ulimi. Ulimi pia  una sehemu kubwa katika dhambi za kuvuta sigara, bangi, kula ugoro, madawa ya kulevya au kunywa pombe. Na dhambi zinginezo kama ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi na ulafi ( WAGALATIA 5:19-21 ), na pia uongo, masengenyo, mizaha, kiburi au majivuno na dhambi nyinginezo nyingi hutokana na kazi za ulimi.

( 3 ). ULIMI CHANZO KIKUU CHA MAANGAMIZO NA KUPOTEZA NGUVU ZA MUNGU.

Kutokana na ulimi, watu wa kawaida, Mitume, Manabii n.k, wanaangamia au wanapata mabaya na kupoteza nguvu ya Mungu. Kutokana na kazi za ulimi hatimaye Kaini alilaaniwa vikali na Mungu ( MWANZO 4:8-12 ). Kutokana na ulimi wana wa Kora walimezwa na ardhi, wakiwa hai ( HESABU 12:1-2 , 9-10 ).  Kutokana na ulimi wana wa Israeli walinung’unika na kunena maovu na kusababisha hasira kali ya Mungu kuwaka juu yao na wengi wao wakateketezwa ( HESABU 11:41 ). Kutokana na ulimi Mtume Petro alimkana Yesu mara tatu na kujiletea majonzi makuu ( MATHAYO 26:69-75 ). Kutokana na ulimi kiungo hiki kilichojaa sumu, watu wengi leo wako katika Jehanamu ya moto. Kutokana na ulimi Yuda Iskaliote alimsaliti Yesu na kujiletea maangamizi ( MATHAYO 26:14-16 ). Samson alipoteza upako juu yake kutokana na ulimi.

( 4 ). HATUA MBILI ZA KUCHUKUA ILI KUUDHIBITI ULIMI.

Je, tunauzuiaje ulimi kwa lijamu au kwa hatamu? Hatua ya kwanza, ni pale tunapotubu dhambi zetu au kuziungama  kwa ndimizetu na kumkiri Yesu kwa ndimi zetu kuwa ni Bwana au Mtawala wa maisha yetu na kuokolewa ( MITHALI 28:13 ; WAFILIPI 2:11; WARUMI 10:8-10 ). Baada ya hatua ya kwanza ya kuokolewa ndimi zetu zinaweza kuendelea kutoa maji machungu yafuatayo:-

      ( 1 ). Uongo. Uongo ni maji maji machungu mtu atakayefanya maskani pamoja na

               Mungu ni yule aliye mbali na kusema uongo au kusingizia. Kwake Ndiyo ni

               Ndiyo na Siyo ni Siyo ( ZABURI 15:1-4 ; MITHALI 25:23; ZABURI 101:6-7;

               MITHALI 19:5,9,22; MITHALI 20:17; WAKOLOSAI 3:9; WAEFESO 4:25 ).

               Ahadi zetu tunazozitoa, hata kama ni kwa hasara zetu, lazima tuzitimize

               ( 2 WAKORINTHO 1:17-19; HOSEA 4:1-2; ZABURI 15:4 ).

 

      ( 2 ).  Mizaha au utani, ni maji machungu, ni sumu. Hakuna utani au watani katika

               Wokovu. Hukumu inamngojea yeyote mwenye mizaha ( MITHALI 28:18-19;

              MITHALI 19;29; ZABURI 1;1 ).

 

      ( 3 )   Masengenyo, ni maji machungu. Kumsengenye mtu ni kumsema mtu vibaya

                Kwa lengo la kumharibia sifa na kutaka aonekane mbaya, hafai na wa

                Kudharauliwa. Anayesengenye nay eye anayefurahia masengenyo na

                Kuyapokea bila kuyakemea, wote hao hawatamuona Mungu ( ZABURI 15:1-3;

                50:16-17,20-22; MITHALI 26;20; WARUMI 1;29-32 ).

      ( 4 ).  Maneno ya kiburi, ukaidi, majivuno na dharau.-Haya yote ni maji machung

                U . Kumcha Bwana ni kuchukia kiburi, majivuni na ukaidi na uasi ( MITHALI 

                8:13 ). Amdharauye mwenzake afanya dhambi ( MITHALI 14:21 ).”Wengine

                Wakiomba pepo hawawezi kutoka, mpaka nije mimi”. “Bila mimi hakuna

                Linalowezekana kufanyika”. Haya ni maji machungu. Kuasi kauli ya Mtumishi

                Wa Mungu ni maji machungu ( HESABU 16:12 )

      ( 5 ).  Maneno mengi wakati wote.-Mtu aliyeokoka hapaswi kuwa na maneno mengi

                Wakati wote ( YAKOBO 1:19 ). Mtu mwenye maneno mengi wakati wote,

                Lazima atakuwa anaishi katika dhambi ( MITHALI 10:19 ). Maneno mengi

                Wakati wote ni maji machungu. Yesu hakuwa ni mtu wa maneno mengi wakati

                Wote (MATHAYO 27:11-14 ).

      ( 6  )Maneno yaliyojaa hasira wakati wote-Haya nayo ni maji machungu. Mtu aliye

                 Okoka , ni mtu wa amani, hatawaliwi na hasira na ugomvi ( MHUBIRI 7:9;

                WAKOLOSAI 3:7-8; YAKOBO 1;19-20 ).

       ( 7 ).  Maneno ya fitina, uchongezi na wivu-Haya nayo ni maji machungu, ni sumu

                ( WARUMI 1:29-32; 2:7-9 ).

       ( 8 ). Maneno yaliyojaa kuhesabu mabaya-Mkristo, hamhesabii mwenzake mabaya

                 tu wakati wote kana kwamba hafanyi jema hata moja. Mkristo husamehe na

                 kusahau, huwa hajishughulishi kuzoa maji yaliyomwagika. Hahesabu mabaya

                 ya mtu, bali mema ( 1WAKORINTHO 13:5; WAFILIPI 4:8 ). Ulimi unaohe

                 sabu mabaya tu ya mtu, ni ulimi unaotoa maji machungu.

       Sasa basi, katika hatua ya pili tunapaswa kujiona kuwa ni ole wetu kuwa  na ulimi   

       Wenye sumu, na kumwomba Mungu auponye ulimi wetu na kuondoa sumu yote na

       Kuutakasa ( ZABURI 120:1-2, 5 )

( 5 ).  JINSI YA KUUFUGA ULIMI

Baada ya kuchukua hatua hizo mbili, tunapaswa kufanya yafuatayo kama sehemu ya maisha yetu:-

  1. 1.      Kufanya uamuzi wa kuzitunza ndimi zetu na kuangalia lolote kabla ya kulisema ( ZABURI 39:1, 9 ).
  2. 2.      Kukaa katika neno la Mungu ili lizidi kutufanya safi kila siku                  ( YOHANA 15:3;ZABURI 119:11 )
  1. 3.      dumu katika maombi maisha yote ( MATHAYO 26:41 )

……………………………………………………………………………………………………..

Je Unataka kuzaliwa mara ya pili ( kuokoka )?

Tunazaliwaje mara ya pili au kwa roho?  Jibu, ni rahisi sana.  Jambo hili linafanyika kwa imani tu!  Kwa imani, tunakiri kwambi sisi ni wenye dhambi, kisha tunaungama dhambi zetu zote kwa kumaanisha kuziacha na kuomba kwamba tuumbwe upya katika Kristo Yesu ili tuweze kutenda matendo mema (WAEFESO 2:8-10;  MITHALI 28:13).  Tukifanya hivi, kwa ghafla tunakuwa viumbe vipya na ndani mwetu kunakuwa na asili mpya inayotuwezesha kushinda dhambi bila jitihada zozote!  Kuokoka ni muujiza wa ajabu.

Je, uko tayari kuokoka au kuzaliwa mara ya pili?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii kwa dhati. “Mungu wangu, hakika mimi ni mwenye dhambi, kwa kuzaliwa na kwa kutenda.  Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Mungu wangu, nisamehe dhambi zangu zote, na kuniumba upya katika Kristo Yesu, ili nizaliwe mara ya pili sasa, nikiwa na asili mpya inayoniwezesha kushinda dhambi.  Kwa imani, napokea  msamaha na kuamini kwamba nimezaliwa mara ya pili sasa katika Jina la Yesu.  Amen”.  Mpendwa, tayari sasa umeokoka. Ili uzidi kuwa na ushindi dhidi ya dhambi, inakupasa kuhudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu (ZABURI 119:11).  MUNGU AKUBARIKI!!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook , Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s