WAJIBU WA KUWA KIELELEZO KWAO WAAMINIO

ZACHARY KAKOBENeno la Uzima kutoka kwa  Askofu Zachary Kakobe        

Tovuti       : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube   : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SOMO:  WAJIBU WA KUWA  KIELELEZO KWAO WAAMINIO

         Hili ni somo moja  kati ya masomo mengi katika shule ya uinjilisti

Mwalimu wa ufuatiliaji, ni Mlezi wa watoto wachanga kiroho. Tabia za mwalimu wa ufuatiliaji au mlezi zina uhusiano mkubwa na tabia za watoto wake. Kwa sababu hii, kila mtendakazi au mwalimu wa ufuatiliaji, anawajibika mno kujifunza somo hili, “WAJIBU WA KUWA KIELELEZO KWA WAAMINIO,” Tutaligawa somo hili katika vipengele saba:-

       ( 1 ). JINSI WATOTO WACHANGA KIROHO WANAVYOFUATA TABIA ZA     

                MLEZI WAO.

       ( 2 ). WAJIBU WA KUWA KIELELEZO KWAO WAAMINIO

       ( 3 ). JINSI WATU WALIO VIELELEZO WANAVYOCHANGIA  KATIKA

                KUENEA KWA KWELI YA NENO           

       ( 4 ). MAENEO MUHIMU YA KUWA KIELELEZO KWAO WAAMINIO.

       ( 5 ). BARAKA ZA KUWA KIELELEZO KWAO WAAMINIO.

       ( 6 ). HASARA ZA KUTOKUWA KIELELEZO KWAO WAAMINIO.

       ( 7 ). JINSI YA KUWA KIELELEZO KWAO WAAMINIO.

( 1 ).  . JINSI WATOTO WACHANGA KIROHO WANAVYOFUATA TABIA ZA MLEZI WAO.

Katika hali ya asili, mtoto mchanga huiga  sana tabia ya mlezi wake. Lugha ya mlezi  ndiyo huwa ligha ya mtoto, na mengi mengineyo. Ikiwa mlezi ni mchafu, mtoto huyo naye huwa mchafu. Ikiwa mlezi ni mkaribishaji na mwepesi kusema “karibu” au “pole”, vivyo hivyo mtoto huiga tabia hiyo. Ikiwa mlezi ni mchapakazi, mtoto naye huiga tabia ya kuchapa kazi. Ikiwa mlezi ni mtu wa shukrani, na ni mwepesi kusema “asante”, mtot naye huwa vivyo hivyo. Mtoto mdogo humwangalia jinsi mlezi wake anavyofanya, naye hufanya vivyo hivyo. Hata kuna methali ya Kiswahili inayosema, “mtoto umleavyo, ndivyo akuavyo” Hali hii, ni sawa kabisa katika mambo ya rohoni. Watoto wachanga kiroho, huiga imani au tabia za wazazi wao. Imani au tabia za Timotheo, ilikuwa ileile iliyokuwako kwa mlezi wake Eunike; na imani au tabia ya Eunike, ilikuwa ileile iliyokuwako kwa mlezi wake  Loisi ( 2 TIMOTHEO 1:5 ). Kama mama wa mtu alivyo, ndivyo alivyo binti yake ( EZEKIELI 16:44-45 ). Isaka alimfuata baba yake Ibrahim, katika kusema uongo uleule wa mlezi wake (MWANZO 12:11-13; 20:1-2; linganisha na  MWANZO 26:6-7 ). Kwa namna hiihii , tabia za Mwalimu wa Ufuatiliaji , zina nafasi kubwa mno “kurithishwa” kwa watoto wake wachanga  wa kiroho anaowafuatilia.

( 2 ).  WAJIBU WA KUWA KIELELEZO KWAO WAAMINIO  

Kutokana na hatari ya kuwarithisha  tabia mbaya “hawa wadogo waaminio”, ndiyo maana Biblia inatoa agizo kwa kila Mwalimu wa Ufuatiliaji, kuwa kielelezi cha tabia njema kwa waaminio. Timotheo alikuwa Mwalimu wa Ufuatiliaji ( 1 WAKORINTHO 4:17; WAFILIPI 2:19 ). Katika kuhakikisha kwamba anawarithisha tabia njema wale anaowafuatilia ( 1TIMOTHEO 4:12 ). Kila Mwalimu wa Ufuatiliaji , anawajibika kuwa kielelezo cha matendo mema, ili kutenda kazi kwake kuwe na faida kubwa katika ufalme wa Mungu  (  TITO 2:7 ).

( 3 ).  JINSI WATU WALIO VIELELEZO WANAVYOCHANGIA KATIKA  KUENEA KWA NENO

Mtu mmoja tu aliye kielelezo , Yesu Kristo, alifanya wengi waaminio wamfuate, na wakatambulika katika jamii yote, hata kwa usemi wao kwamba wanasema kama Yesu        ( YOHANA 13:15; MATHAYO 28:71-73 ). Mtu mmoja anayefundisha kwa mfano au kielelezo, anaweza kubadili jamii kubwa ya watu, kuliko watu elfu kumi wanaofundisha kwa nadharia tu zinazopingana na tabia zao. Kanisa la Wathesalonike, lilikuwa na Walimu wengi wa Ufuatiliaji waliokuwa vielelezo kwao waaminio, na hivyo kulifanya neno la Mungu kuvuma kila mahali ( 1 WATHESALONIKE 1:7-8 ).  Bwana ampe kila Mwalimu wa Ufuatiliaji  kati yetu, siyo moto tu wa kuwalea na kuwafundisha  kwa nadharia watoto wachanga kiroho, bali kuwa kielelzo kwao waaminio, ili Neno la Mungu livume kila mahali katika Tanzania na hata nje ya nchi.

( 4 ).  MAENEO MUHIMU YA KUWA KIELELZO KWAO WAAMINIO 

Ni maeneo  yapi muhimu ya kuwa kielelzo  kwao wadogo  hawa  wamwaminio Yesu? Biblia inatupa jibu. Inatupasa kujitunza nafsi zetu pamoja na mafundisho yetu yote, katika usemi, mwenendo, katika upendo na imani na usafi ( 1 TIMOTHEO 4:12,16 ). Kwa namna hii ndipo tutakapojiokoa nafsi zetu na wale watakao yasikia mafundisho yetu. Inatupasa tuwe vielelezo kwa wale tunaowafuatilia  katika mahudhurio yetu Kanisani ( LUKA 2:49 ). Ikiwa sisi wenyewe hatuhudhurii  Kanisani  ibada fulani fulani,  tutawezaje kuwafundisha watoto wachanga kiroho, “umuhimu wa kuhudhuria ibada zote?”   Watoto Wachanga kiroho waaminio huangalia  sana tabia za waliu wao wa Ufuatiliaji, na kuona kwamba tabia hazo  ndiyo viwango  vya wokovu.  Wakimuona Mwalimu wao wa Ufuatiliaji hahudhurii ibada zinginezo, wao nao huona kwamba “Haitupasi kuwamo katika nyumba ya baba yetu” na mafundisho mengine huyapuuza. Tunahitajika pia kuwahi kanisani, saa ya kusali ( MATENDO 3:1 ). Wadogo hawa wamwaminio Yesu , wakiona Walimu wao wa Ufuatiliaji wanachelewa Kanisani, wao nao huiga  hivyohivyo. Inatupasa kuwa kielelezo kwao katika mavazi yetu ( WARUMI 12:2 ), utii na unyenyekevu  kwa kiongozi wetu  ( WAEBRANIA 13:17 ), maisha yetu ya maombi ( 1 WATHESALONIKE  5:17 ), imani ( 1 TIMOTHEO 4:12 ) n.k. Ikiwa sisi wenyewe tunaonesha kutokuamini juu ya uponyaji wetu, wao nao watakuwa vivyo hivyo. Ikiwa sisi bado hatujafanya malipizo ya ndoa, na tuna wake zaidi ya mmoja au mume tuliye naye siye mume wetu ( YOHANA 4:18 ), wao nao , wataona kufanya hivyo ni sawa. Ikiwa majumbani mwetu  tunasikia muziki wa dansi katika redio zetu au kipindi cha michezo na maigizo, wao nao wataona kwamba  kufanya hivyo ni sawa. Katika  kila jambo tunalolifanya au kusema , kila mmoja wetu ajiulize kwanza watoto wangu wa kiroho wakiiga kufanya au kusema  hivi, je nitakuwa nimewarithisha tendo jema? Ikiwa jibu letu la swali hili ni hapana, basi mara moja tusifanye au kulisema jambo hilo.

( 5 ). BARAKA ZA KUWA KIELELEZO KWAO WAAMINIO    

  1. 1.      Maji baridi, yanakata kiu mara moja. Vivyo hivyo, tukiwa kielelzo kwa wadogo      hawa na kukata kiu yao ya kupokea mfano kutoka kwetu, tukifanya hivyo kamwe  haitatupotea thawabu yetu ( MATHAYO 10:42 )

       2.   Tukiwa kielelezo kwao wadogo hawa waaminio, hatuwezi kamwe kuwapoteza  na hivyo tutampendeza mno Mungu wetu. Tukimpendeza Mungu wetu kwa ajili  hiyo atakuwa pamoja nasi, hatatuacha. Wakati mwingine, hata kabla ya kuomba kwetu atajibu ( MATHAYO 18:14; YOHANA 8:29; ISAYA 65:24 ). Hakika atatuponya ( 2 SAMWELI 22:20 ).

3        Tutapokea Taji ya Utukufu, ile isiyokauka siku ile atakapodhihirishwa  kwetu

Bwana Yesu ( 1 PETRO 5:3-4 ).

( 6 ).  HASARA YA KUTOKUWA KIELELEZO KWAO WAAMINIO

Kutokuwa kielelezo kwa “wadogo hawa  wamwaminio Yesu” , ni kuwakosesha , na hukumu ya kufanya hivyo, ni mbaya zaidi kuliko kufungiwa shingoni jiwe kubwa  la kusagia na kutoswa katika kilindi cha bahari ( MATHAYO 18:6 ). Kufanya hivyo, pia ni kufanya jambo lisilopendeza mbele za Mungu ( MATHAYO 18:14 ); na  kama tunafanya  yasiyompendeza, tutaingia mbingu ya nani?

( 7 ).  JINSI YA KUWA KIELELEZO KWAO WAAMINIO

  1. 1.      Kumuomba Mungu atufanye kuwa vielelezo  kwao, na Yesu mwenyewe

Atafanya  ndani yetu yale yapendezayo mbele zake ( YAKOBO 4:2; LUKA 11:10; WAEBRANIA 13:20-21 ).

  1. 2.      Kuwakamata  mbweha wote, hata wale walio wadogo waiharibuo mizabibu yetu

Inayochanua, yaani kuangalia lolote lile linaloweza kuwa jambo la kuwakosesha watoto wachanga tutakaowafuatilia, na kulitupa nje ( WIMBO ULIO BORA 2:15 ).

  1. 3.      Kulishika neno hili la imani tulilojifunza  katika somo hili, vilevile kam tulivyo

Tunazaliwaje mara ya pili au kwa roho?  Jibu, ni rahisi sana.  Jambo hili linafanyika kwa imani tu!  Kwa imani, tunakiri kwambi sisi ni wenye dhambi, kisha tunaungama dhambi zetu zote kwa kumaanisha kuziacha na kuomba kwamba tuumbwe upya katika Kristo Yesu ili tuweze kutenda matendo mema (WAEFESO 2:8-10;  MITHALI 28:13).  Tukifanya hivi, kwa ghafla tunakuwa viumbe vipya na ndani mwetu kunakuwa na asili mpya inayotuwezesha kushinda dhambi bila jitihada zozote!  Kuokoka ni muujiza wa ajabu.

Je, uko tayari kuokoka au kuzaliwa mara ya pili?  Najua uko tayari.  Basi fuatisha sala hii kwa dhati. “Mungu wangu, hakika mimi ni mwenye dhambi, kwa kuzaliwa na kwa kutenda.  Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha.  Mungu wangu, nisamehe dhambi zangu zote, na kuniumba upya katika Kristo Yesu, ili nizaliwe mara ya pili sasa, nikiwa na asili mpya inayoniwezesha kushinda dhambi.  Kwa imani, napokea  msamaha na kuamini kwamba nimezaliwa mara ya pili sasa katika Jina la Yesu.  Amen”.  Mpendwa, tayari sasa umeokoka. Ili uzidi kuwa na ushindi dhidi ya dhambi, inakupasa kuhudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu (ZABURI 119:11).  MUNGU AKUBARIKI!!!

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook,Twitter n.k,  kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s